Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w80 7/15 uku. 10
  • Hata Ndege ‘Wanajua Wakati Wao’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Hata Ndege ‘Wanajua Wakati Wao’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Habari Zinazolingana
  • “Waangalieni kwa Makini Ndege”
    Amkeni!—2014
  • Kuchungua Mafumbo ya Uhamaji
    Amkeni!—1995
  • Wakati Ndege Wanapogonga Majengo
    Amkeni!—2009
  • Mambo Tunayojifunza Kutokana na Ndege wa Mbinguni
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
w80 7/15 uku. 10

Hata Ndege ‘Wanajua Wakati Wao’

KULIKUWAKO hali yenye kusikitisha sana kati ya Waisraeli katika wakati wa Yeremia. Mwendo wao ulitofautiana na ule wa ndege wenye kuhama. Tunasoma hivi: “[Hata] koikoi angani ajua nyakati zake zilizoamriwa; na hua na mbayuwayu na korongo huangalia wakati wa kuja kwao; bali watu wangu hawazijui amri za [Yehova].”​—Yer. 8:7.

Ijapokuwa ndege wenye kuhama kama vile koikoi, hua, mbayuwayu na korongo wanajua wakati wa kuja kwao na wakati wa kuondoka, Waisraeli hawakujali hukumu za Yehova. Kwa habari ya ndege hao wenye kuhama, kuja na kuondoka kwao ni jambo la lazima ili waendelee kuwa hai. Vivyo hivyo, hali njema pamoja na ufanisi wa Waisraeli ulitegemea juu ya kujipatanisha kwao na hukumu za Yehova. Walakini Waisraeli walishindwa katika jambo hilo, na kwa hiyo, hawakuweza kuonyesha hata busara inayoonyeshwa na ndege wasio na akili ambao hujua wakati wao wa kuhama.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki