Ufahamu Katika Habari
‘Utii Wao wa Kwanza’
● Mleta habari za magazeti Steve Mitchell wa gazeti “The Post” katika Palm Beach, Florida (U.S.A.), alisema hivi karibuni kwamba Mashahidi wa Yehova ni ‘‘mojayapo ya madhehebu ya kidini inayoteswa sana ulimwenguni” kwa sababu, kwa mfano, hawasaluti [hawasalimu] bendera ya taifa lo lote. ‘‘Huo si msimamo unaopendwa na watu wengi,” akasema, “lakini angaa taifa hili msingi wake ulikuwa uhuru wa kidini. Au ndivyo ilivyopaswa kuwa, je! wakumbuka?”
Mitchell alisema vilevile hivi: “Wanalipa kodi zao. Wao ni baadhi ya wananchi walio wanyofu zaidi katika Jamhuri [hii]. Walakini wanamtii Mungu kwanza, si nchi. Ijapokuwa sikubaliani na imani zao, naona sana kwamba haki yao ya kuzifuata ni sehemu kubwa ya yote yanayowakilishwa na nchi hii.”