Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w80 11/1 kur. 14-19
  • Msiba Unaowaelekea Wanadini Wote wa Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Msiba Unaowaelekea Wanadini Wote wa Ulimwengu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • KUSHINDWA KWA “MIUNGU” NA “MIUNGU-WAKE”
  • ONYO JUU YA “MABAYA” YAJAYO LATOLEWA
  • “Tokeni Kwake, Enyi Watu Wangu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • “Yule Kahaba Mkuu” Akaribia Kuuawa Kwake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • “Babeli” Usio na Usalama Wahukumiwa Kuangamizwa
    Usalama Ulimwenguni Pote Chini ya “Mwana-Mfalme wa Amani”
  • Yehova Anyenyekeza Jiji Lenye Kujigamba
    Unabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
w80 11/1 kur. 14-19

Msiba Unaowaelekea Wanadini Wote wa Ulimwengu

1. Idadi ya watu wa kidini inakadiriwa kuwa nini, nako kuanguka kwa milki hiyo ya kidini kutakuwa na matokeo gani juu ya mataifa?

IDADI ya watu wa kidini wa ulimwengu ni kubwa sana. Kitabu World Almanac cha mwaka 1980 kinaionyesha kuwa juu sana kufikia 2,511,417,750. Kinatia ndani ya hesabu hii wale wanaodai kuwa Wakristo, Wayahudi, Waislamu, Wabuddha, Wabanyani, na wengineo. Wakati milki hiyo ya kidini iliyogawanyika kindani iangamizwapo, jambo hilo litawashtua wengi wa wanadamu watakaookoka. Matokeo yenye kushtua ya jambo hili yanatabiriwa katika maneno haya: “Kwa mshindo wa kutwaliwa Babeli nchi yatetemeka, na kilio chake chasikiwa katika mataifa.” “Sauti ya kilio kutoka Babeli, na ya uangamivu mkuu toka nchi ya Wakaldayo! Maana [Yehova] amwangamiza Babeli, na mawimbi yake yavuma kama maji mengi, mshindo wa sauti zao wafanya makelele; kwa maana mwenye kuangamiza amefika kwake; naam, amefika Babeli; na mashujaa wake wametwaliwa; pinde zao zimevunjika kabisa; maana [Yehova] ni Mungu wa kisasi; hakika yake yeye atalipa.”​—Yer. 50:46; 51:54-56.

2. (a) Babeli ya kale ilinena juu ya mataifa ikiwa na “sauti” ya namna gani, walakini “sauti” yake ilinyamazishwaje? (b) Ufunuo unaonyesha mfano wake wa kisasa ukiwa unapanda nani, naye atamfanya nini?

2 Kutimizwa kwa tukio hilo kutakuwa jambo lenye kushtua ulimwengu, ambalo mfano wake haujapata kusikika hata kidogo kabla ya hapo. (Yer. 51:2, 60, 64) Ikiwa Mamlaka ya Tatu ya Ulimwengu ya historia ya kale, Babeli ilisema kwa ‘sauti kuu’ yenye mamlaka. Walakini katika mwaka 539 K.W.K. “sauti” yake ilipata kunyamazishwa na mawimbi yavumayo ya washindi walioiingilia. Mfano wake wa kisasa, Babeli Mkuu, amenena kwa “sauti” yenye kutawala hata Zaidi. Ulimwengu wote umesikiliza. Kitabu cha Biblia cha Ufunuo, sura ya 17, kinamfananisha akikalia mnyama mwenye vichwa saba, mnyama huyo mwekundu sana akiwa anafananisha tengenezo la ulimwengu. Vichwa vyake saba vinafananisha zile mamlaka saba kama vile zilivyofuatana kufikia Mamlaka ya Ulimwengu ya sasa ya mwungano wa Uingereza na Amerika. (Ufu. 17:1-6) Zile pembe 10 za mnyama huyo “ni wafalme kumi.” (Ufu. 17:12) Kichwa cha tatu cha vile vichwa saba kilifananisha Milki ya Kibabeli na cha nne kilifananisha Milki ya Wamedi na Waajemi. Babeli Mkuu wa kidini amefanya ukahaba na mamlaka zote hizo saba. Amejaribu kuwapanda wote kama bibi yao. Wamekunywa mchanganyiko wa kidini uliomo ndani ya kikombe chake cha dhahabu. Wakichoshwa naye, mwishowe watamchukia na kumwangusha kutoka mgongoni mwao.

3. (a) Yehova alitangaza kwamba angeleta nini juu ya mfano wa kale wa Babeli Mkuu, na kutoka wapi? (b) Sababu gani Wamedi walionyeshwa wakiwa wenye kutokeza sana jinsi hiyo?

3 Akiongeza sababu inayoonyesha kwa nini inatupasa kutoka katika Babeli Mkuu pasipo kuchelewa, Yehova ametangaza kusudi lake la kuleta juu yake kilichofananishwa zamani na “kusanyiko la mataifa makubwa, toka nchi ya kaskazini” limshambulie. Kwa kuwa “kusanyiko” hilo lingekuwa mwungano wa jeshi chini ya mwenye amri mmoja, lingeweza vilevile kuitwa ‘taifa toka kaskazini.’ (Yer. 50:3, 8, 9) Unabii huo ulikuwa sahihi uliposema kwamba “wafalme wa Wamedi” wangekuwa wenye kutokeza sana katika “kusanyiko” hilo la mataifa. (Yer. 51:11) Waajemi hawakutajwa kama wakiwa kati ya kusanyiko hilo. Hilo halikuwa jambo lililosahauliwa bila kukusudiwa, kwa kuwa Koreshi Mkuu, aliyechukua mamlaka kuu zaidi ya “kusanyiko” hilo, alikuwa na uhusiano wa damu na Wamedi. Baada ya kuushinda ufalme wa Wamedi, sana sana alitumia askari Wamedi katika jeshi lake. Koreshi alichukua mamlaka baada ya siku za Yeremia.

4. Baada ya Babeli kuanguka, ni nani aliyekuwa wa kwanza kutawala katika mji huo, naye Danieli alikuwa sahihi namna gani alipotabiri yule ambaye angekuwa na mamlaka kuu zaidi katika milki ya Wamedi na Waajemi?

4 Baada ya Babeli kuanguka katika mwaka 539 K.W.K., Dario Mmedi aliyeanza kutawala huko alikuwa na umri wa miaka 62. (Dan. 5:30, 31) Kuhusiana na Milki ya Wamedi na Waajemi, unabii wa Danieli 8:3 ulikuwa sahihi ulipoonyesha kwamba sehemu ya Waajemi ingechukua mamlaka baadaye. Koreshi Mwajemi ndiye aliyetoa amri ya kwamba Wayahudi waliokuwa uhamishoni warudi katika nchi yao.​—Ezra 1:1-4.

5. (a) Yehova anashikamanishwa na upande gani kwa habari ya matendo ya uharibifu? (b) Yeye alitangaza kwamba angemtumia nani kama rungu lake katika kuvunja-vunja mataifa na falme?

5 Kama vile ilivyokuwa kwa habari ya kuharibiwa kwa Yerusalemu katika mwaka 607 K.W.K., uharibifu ungekuja juu ya Babeli kutoka “kaskazini.” (Eze. 1:4; 9:2; Yer. 50:41; 51:48) Kuhusiana na upande, Zaburi 75:6, 7 humshirikisha Yehova waziwazi na upande wa kaskazini isemapo hivi: “Maana siko mashariki wala magharibi, wala [kusini] itokako heshima. Bali Mungu ndiye ahukumuye; humdhili huyu na kumwinua huyu.” Mfalme Nebukadreza wa Babeli alikuja kushambulia Yerusalemu pamoja na mfalme wake mwasi, Sedekia, kutoka katika upande wa kaskazini katika mwaka 609 K.W.K. Miaka miwili baadaye “[akaaye] Sayuni” angeweza kupaza sauti hivi: “Nebukadreza mfalme wa Babeli, amenila, . . . amenimeza kama joka.” (Yer. 51:34, 35) Kwa habari ya namna Yehova alivyohusiana na uharibifu wa Yerusalemu, Yeremia anamtaja kama akisema maneno haya huko nyuma katika mwaka 614 K.W.K. kuhusu Nebukadreza akiwa chombo chake cha kufisha: “Wewe u rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunja-vunja mataifa [Yuda, Misri, Moabu, Amoni, Edomu, na mengineyo]; na kwa wewe nitaharibu falme; . . . na kwa wewe nitawavunja-vunja maliwali na maakida.”​—Yer. 51:20-23.

6. Baada ya maneno hayo yaliyotangulia kutajwa, Yehova alitangaza kwamba angewalipa nini wakaaji wa Ukaldayo?

6 Baada ya hayo, vipi, Ee Yehova? “Nami nitamlipa Babeli [si Nebukadreza], na wote wakaao ndani ya Ukaldayo, mabaya yao yote, waliyoyatenda katika Sayuni [au, Yerusalemu] mbele ya macho yenu.”​—Yer. 51:24, 59, 60.

7. Ni mwito gani wa vita ambao Yehova alielekeza juu ya Babeli katika mwaka 614 K.W.K., naye ni nani aliyeuitikia?

7 Katika siku za Nebukadreza na warithi wake, Milki ya Wamedi ilikuwa upande mwingine wa Mto Tigri katika upande wa mashariki na upande wa kaskazini wa Milki ya Babeli. Ili kutimiza unabii, Koreshi Mkuu, akiwa pamoja na Mfalme Dario Mmedi, walikuja kushambulia nchi ya Ukaldayo pamoja na mji wake mkuu, Babeli. Watekaji hao wa Babeli waliitikia mwito wa Yehova wa kupiga vita uliokuwa umekwisha tolewa katika mwaka 614 K.W.K.:

“Itwekeni bendera katika nchi, pigeni tarumbeta kati ya mataifa, yawekeni mataifa tayari juu yake; ziiteni juu yake falme za Ararati, na Mini, na Ashkenazi [upande wa kaskazini]; agizeni jemadari juu yake; wapandisheni farasi, kama tunutu. Wekeni mataifa tayari juu yake, wafalme wa Wamedi, na maliwali wake, na maakida wake, na nchi yote ya mamlaka yake. Nayo nchi yatetemeka, nayo ina utungu; maana makusudi ya [Yehova] juu ya Babeli yasimama, kuifanya nchi ya Babeli ukiwa, isikaliwe na mtu.”​—Yer. 51:27-29.

8. Yehova anamtayarisha nani kwa ajili ya utumishi wa kushambulia Babeli Mkuu, nako kuangamizwa kwake kunafika lini? Baada ya kufunguliwa kwa nani?

8 Yehova ‘alimtayarisha’ Koreshi Mkuu Mwajemi kwa kazi Yake ya kijeshi ya kushambulia Babeli ya kale. Maneno ya Yehova katika Isaya 44:28 mpaka 45:7 humtaja Koreshi kwa jina akiwa kama “Mchungaji wangu” na kama “masihi.” Yeye alifananisha “Mchungaji” Mkuu Zaidi wa Yehova, Yesu Kristo, ambaye kupitia kwake Yehova anaharibu kile kilichofananishwa na Babeli ya kale, yaani, Babeli Mkuu, milki ya ulimwengu ya dini ya uongo. Tayari kupitia kwa huyu Koreshi Mkuu Zaidi wake, Yehova amekwisha kuwatoa watu wake walio wakf katika utumwa wa Babeli Mkuu, tangu mwaka 1919 na kuendelea. Uharibifu wake kamili utakuja vilevile kupitia kwa Koreshi Mkuu Zaidi uyu huyu katika “ile dhiki iliyo kuu” inayokuja iliyotabiriwa katika Ufunuo 7:13, 14.

KUSHINDWA KWA “MIUNGU” NA “MIUNGU-WAKE”

9. Babeli ya kale ilikuwa na miungu gani, nayo njia ambayo katika hiyo ilikabiliana na mabaya yaliyoipata inafananisha nini kwa habari ya Babeli Mkuu katika wakati wa ‘dhiki kuu’?

9 Babeli ya kale ilikuwa na miungu wake, kama vile Beli, Merodaki (Marduki), Sukoth-benothi, Nebo, mungu-mke Ishtari (Ashtorethi) na mingineyo, licha ya wale makuhani wachawi. (Yer. 50:2; 51:44; 2 Fal. 17:30; Isa. 46:1, 2) Sababu gani haikuja kuiokoa Babeli? Jibu ni kwamba miungu hiyo sanamu haikuwa miungu. (1 Kor. 8:5, 6) Kushindwa kwa miungu hiyo kunafananisha kushindwa kwa miungu yote ya Babeli Mkuu kumwokoa kutokana na msiba uliokusudiwa kumpata katika ile “dhiki kubwa.” Yeye ana miungu na miungu-wake wengi. Kwa habari ya dini ya Wabanyani, inasemekana kuwa kuna miungu 330,000,000 kutia na ule utatu wa Brahma, Vishnu na Siva. (Kitabu The Americana, ukurasa 196, chapa ya 1929) Kisha kunayo miungu ya makabila ya Kiafrika pamoja na wachawi, miungu ya Wabuddha na wafuasi wa dini ya Confucius, na bila kusahau “Mungu wa utatu” wa Jumuiya ya Wakristo. Miungu hiyo haina uwezo wa kuokoa.

10. Katika mashindano yanayokuja ya uungu, ni nani atakayejithibitisha kweli kweli kuwa nao?

10 Katika mashindano yanayokuja ya Uungu, Yehova, Mungu Mwenye Nguvu Zote atakuwa akishindana na miungu na miungu-wake wa milki ya Kibabeli ya dini ya uongo. Shetani Ibilisi, mungu wa taratibu hii ya mambo asiyeonekana, hataweza kuthibitisha miungu yote ya Babeli Mkuu kuwa ndiyo miungu inayopaswa kutegemewa ilete wokovu. (Efe. 2:2; 2 Kor. 4:4, NW) Yehova peke yake ndiye atakayebaki akiwa mshindi katika uwanja huo wa mashindano akiwa ndiye Mungu mmoja aliye hai na wa kweli, Mwokozi.

11. Ni nani watakaotumiwa na Yehova katika njia yenye kuonekana katika kumwangamiza Babeli mkuu, nao Ufunuo 17:11 unasema nini juu ya chombo hicho?

11 Katika ‘shindano lijalo kati ya miungu,’ Yehova hatamtumia Yesu Kristo, Koreshi Mkuu Zaidi wake katika njia yenye kuonekana ili amwangamize Babeli Mkuu. Yeye atawaruhusu mawakili wa ile Mamlaka ya Nane ya historia ya Biblia wamshambulie Babeli Mkuu. Mamlaka hiyo ya ulimwengu ya karibuni ndicho chombo ambacho mataifa ya kilimwengu wamekifanyiza na kukitumia tangu mwaka 1919 katika kujaribu kuhifadhi amani na usalama wa ulimwengu, ambacho sasa ndicho Umoja wa Mataifa. Tengenezo hili lililofanyizwa na wanadamu sasa lina “kusanyiko” la mataifa 152 kama washiriki wake. Linafananishwa na mnyama mwekundu sana mwenye vichwa saba na pembe 10, na kwa habari yake Ufunuo17:11 wasema hivi: “Yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.” Kabla ya kuharibiwa kwake katika “vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi” katika Har-Magedoni, anairuhusu hii Mamlaka ya Nane ya Ulimwengu ijiletee ushindi mkubwa, walakini si juu yake.​—Ufu. 16:14, 16.

12. Tangu apigiwe kura atokezwe katika mwaka 1919, yule “mnyama” alimruhusu nani amwongoze, lakini kulingana na Ufunuo 17:15-17, “mnyama” huyo atamfanyaje huyo anayempanda?

12 Tangu wakati mnyama huyu mwekundu sana wa mfano alipopigiwa kura atokezwe katika mwaka wa 1919 uliofuata baada ya vita, amemruhusu yule “kahaba” wa kidini, Babeli Mkuu, ampande mgongoni mwake akiwa kama malkia na kumwongoza. (Ufu. 17:18) Katika wakati wa “dhiki kubwa” na wakati saa ya Mungu ya tukio hilo ifikapo, ishara ya kutenda yaweza kupatikana katika maneno yake katika Ufunuo 17:15-17: “Yale maji [wewe Yohana] uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha. Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto. Maana Mungu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule mnyama ufalme wao hata maneno ya Mungu yatimizwe.”

13, 14. (a) Kulingana na maarifa yake ya kimbele, Yehova anawaruhusu watawala wa kisiasa wamfanyeje huyo “kahaba”? (b) Mara tu baada ya kufanya hivyo, washindi hao waliomshinda watajaribu kufanya nini kwa habari ya Mashahidi wa Yehova, nao mwisho wa mwendo wao utakuwa nini?

13 Kama vile ilivyotabiriwa, mataifa waliopata kuwa washiriki wake waliupa kwanza Ushirika wa Mataifa na kisha mrithi wake Umoja wa Mataifa, mamlaka yenye kuogopesha ili uweze kuhifadhi amani na usalama wa ulimwengu. Yehova hakuwaongoza wafanye hivyo, walakini, akitangulia kujua, alionyesha maarifa yake ya kimbele katika Neno lake lililoandikwa, Ametabiri vilevile kwamba mataifa hayo, yakiwa yameungana kama “kusanyiko,” yangechoshwa na mzigo wa huyo kahaba, Babeli Mkuu, mwenye kujiingiza katika mambo ya siasa za mataifa yote. Wakati atakapoangushwa kutoka katika mgongo wa baraza hiyo yenye kuhifadhi amani na mwishowe kuteketezwa kwa moto, mashahidi Wakristo wa Yehova hawataogopeshwa na “mabaya” yatakayompata. Kutokana na Neno la Mungu wao wanajua kwamba wakiwa duniani wanamwakilisha Yesu Kristo, “Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme,” na ya kwamba kwa sababu hiyo, washindi wenye furaha wa Babeli Mkuu watawageukia kwa kuwaona kuwa kizuizi peke yake kinachobaki cha kuwazuia waitawale dunia yote. Mashahidi wa Yehova wametangulia kuonywa juu ya jambo hilo kwa unabii huu wa Ufunuo 17:13, 14; HNWW.

14 “Shabaha ya hawa [mataifa ya kisiasa yanayowakilishwa katika Umoja wa Mataifa] . . . ni moja, na watampa yule mnyama nguvu na mamlaka yao yote, Watapigana na Mwana-Kondoo pamoja na wale aliowaita na kuwachagua, ambao ni waaminifu, atawashinda kwa sababu yeye ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme.”

15, 16. (a) Mapambano hayo ya mwisho juu ya utawala wa dunia yatamaanisha nini? (b) Ni maono gani ya kimbele anayotupa mtume Yohana juu ya tukio hilo, kukiwa na matokeo gani?

15 Pigano hilo la kijeshi lamaanisha “vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi” katika hali ya ulimwengu iitwayo Har-Magedoni. (Ufu. 16:13-16) Wakiwa chini ya ulinzi wake Mashahidi wa Yehova watashuhudia kwa macho yao wenyewe ile “vita” ambayo maelezo yake yanatolewa katika Ufunuo 19:11-21. Katika maono ya kimbele ya mapambano hayo ya mwisho juu ya suala la utawala wa ulimwengu, mtume Mkristo Yohana anaeleza matokeo ya vita hiyo, aandikapo hivi:

16 “Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule [amiri jeshi mkuu wa Yehova, Yesu Kristo], tena na majeshi yake [ya malaika wa kimbinguni]. Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo [Mamlaka ya Ulimwengu ya mwungano wa Uingereza na Amerika] pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao walioisujudia sanamu yake [ule Umoja wa Mataifa]; hao wawili wakatupwa wangali hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti; na wale waliosalia waliuawa kwa upanga wake yeye aliyeketi juu ya yule farasi, upanga utokao katika kinywa chake. Na ndege wote [wanaotajwa katika mstari wa 17 na 18] wakashiba kwa nyama zao.”

17. Mabaya hayo yanayozipata mamlaka za kisiasa zisizomwamini Mungu yatamaliza jambo gani, kisha ni jambo gani linalozipata mamlaka zisizoonekana?

17 Kuharibiwa huko kwa sehemu zisizomwamini Mungu za hii taratibu ya mambo inayotawalwa na Ibilisi kutaimalizia ile ‘dhiki kuu’ inayotajwa katika Ufunuo 7:14. Jambo hilo litafuatwa na kufungwa na kutupwa katika shimo lisilo na mwisho kwa mtawala asiyeonekana wa ulimwengu huu, Shetani Ibilisi, pamoja na malaika zake wote walio mashetani kwa muda wa miaka 1,000 inayofuata.—Ufu. 20:1-3.

18. Neno la Mungu laonyesha nini kwa habari ya kwamba vita hiyo kubwa kuliko zote itaiacha dunia bila wakaaji?

18 Je! vita hiyo kubwa kuliko vyote katika Har-Magedoni itaiacha dunia bila uhai wo wote wa kibinadamu? Mwisho wa ulimwengu wa kale wa siku za Nuhu ulioletwa na gharika haukufutilia mbali wanadamu wote duniani, kwa kuwa wanadamu wanane waliokoka gharika hiyo ya duniani pote. (2 Pet. 2:5) Yehova, Mungu wa Nuhu, aliifanya dunia “ili ikaliwe na watu.” (Isa. 45:18) Kupitia kwa nabii Isaya, Yehova alitabiri juu ya mshindi Mwajemi, Koreshi Mkuu na kulitaja jina lake la kibinafsi, naye mkombozi huyo wa Wayahudi waliokuwa uhamishoni alitokezwa ili amfananishe Mkombozi Mkuu Zaidi, Yesu Kristo. Katika “vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi” inayokuja katika Har-Magedoni, Yesu Kristo atapata ushindi juu ya adui zote za kidunia za Yehova na watu wake, akiziua adui hizo za ufalme wa Mungu. Yesu Kristo hatafanya kazi hiyo ya kufisha kwa hasara ya kila mshiriki wa mabaki ya wafuasi wake watiwa mafuta, waliozaliwa kwa roho walio duniani, kwa kuwa kama ingekuwa hivyo ufalme wa Mungu haungepata ushindi kamili. Tena, namna gani juu ya “mkutano mkubwa” wa washiriki waaminifu wanaoshirikiana na mabaki watiwa mafuta? Ufunuo 7:9-15 wasema waziwazi kwamba huu “mkutano mkubwa” wataiokoka hiyo “dhiki iliyo kuu” inayofikia kilele chake katika Har-Magedoni.

ONYO JUU YA “MABAYA” YAJAYO LATOLEWA

19, 20. (a) Kabla ya mabaya hayo yatakayoupata ulimwengu, lazima nani apewe onyo? (b) Yehova alionyeshaje mfano wa kutolewa kwa onyo hilo katika siku za Yeremia?

19 Mabaya yatakayoupata ulimwengu yako mbele tu! Onyo juu ya jambo hilo lazima litolewe kwa Babeli Mkuu, tengenezo lile lenye kutawala ulimwengu. Ilionyeshwa namna ambavyo angepewa onyo hilo huko nyuma katika siku za Yeremia, ndiyo, katika mwaka 614 K.W.K. Juu ya hili yeye anatuambia hivi:

20 “Neno ambalo Yeremia, nabii, alimwamuru Seraya, mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa kumiliki kwake. Basi Seraya alikuwa msimamizi mkuu wa nyumba ya mfalme. Naye Yeremia akaandika katika kitabu habari ya mabaya yote yatakayoupata Babeli, maneno hayo yote yaliyoandikwa juu ya Babeli. Naye Yeremia akamwambia Seraya, Utakapofika Babeli, basi angalia uyasome maneno haya yote, ukaseme, Ee [Yehova], umenena habari za mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele. Tena itakuwa utakapokwisha kukisoma kitabu hicho utakifungia jiwe, na kukitupa katika mto Frati; nawe utasema, Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena, kwa sababu ya mabaya yote nitakayoleta juu yake; nao watachoka.”

21, 22. Tendo hilo la Seraya liliigwaje kwa njia ya unabii katika kitabu cha Ufunuo, pamoja na maneno gani yaliyoshirikishwa nalo?

21 Yale ambayo Seraya, nduguye Baruku, mwana wa Neria, aliamriwa afanye ili kuonyesha namna ambavyo Babeli wa kale ungeangushwa yalinakiliwa katika kitabu cha Ufunuo. Mwandikaji wa kitabu hicho, mtume Mkristo Yohana, anaeleza kwanza juu ya kuharibiwa kwa “kahaba” huyo wa kidini wa mataifa yote, Babeli Mkuu, na kisha anaendelea kusema hivi:

22 “Na malaika mmoja mwenye nguvu akainua jiwe, kama jiwe kubwa la kusagia, akalitupa katika bahari, akisema, Kama hivi, kwa nguvu nyingi, utatupwa Babeli, mji ule mkuu, wala hautaonekana tena kabisa. . . . wala sauti ya bwana-arusi na bibi-arusi haitasikiwa ndani yako kabisa; maana hao wafanya biashara wako walikuwa wakuu wa nchi, kwa kuwa mataifa yote walidanganywa kwa uchawi wako. Na ndani yake ilionekana damu ya manabii, na watakatifu, na ya wale wote waliouawa juu ya nchi.”​—Ufu. 18:21-24.

23. (a) Ni kwa sababu gani furaha ya washindi wa Babeli Mkuu wasiomwamini Mungu itakuwa ya kitambo tu? (b) Kwa hiyo, hao wasiomwamini Mungu watajaribu kufanya nini, kukiwa na matokeo gani?

23 Furaha watakayokuwa nayo “wafalme” au watawala wa kisiasa baada ya kumzamisha Babeli Mkuu katika bahari ya uharibifu itakuwa ya kitambo kidogo tu. Waabudu wengi wa Yehova, Mungu aliye hai watakaokuwa wameokoka watakuwa bado wakiwakabili, wao wakiwa mabaki ya watiwa mafuta wa jamii ya Yeremia na vilevile wenzao washikamanifu, ule “mkutano mkubwa” aliouona mtume Yohana katika njozi. Itakuwa lazima hatua ichukuliwe juu ya hao. Wakati watawala hao wa kisiasa watakapojaribu kufutilia mbali ibada yote duniani kwa kuwashambulia mabaki pamoja na wenzao, itakuwa sawasawa na kumshambulia Yesu Kristo, Bwana wao wa kimbinguni, aliye Koreshi Mkuu Zaidi. Tendo hilo litamaanisha kupigana vita pamoja naye katika Har-Magedoni. Vita itakayotokea wakati huo itakuwa kubwa zaidi kuliko ile vita ya silaha za nuklea ambayo sasa mataifa wanajaribu kuzuia isitokee kati yao wenyewe, kwa kuwa toka makao yasiyoonekana Yesu Kristo pamoja na jeshi lake la malaika wa kimbinguni watawaangamiza washambuliaji hao wenye kujitanguliza wa Mashahidi wa Yehova.

24. Ni nani watakaokuwa na pendeleo la kujionea kwa macho yao wenyewe hiyo ‘‘vita ya siku ile kuu,” pasipo kushiriki sehemu yo yote yake, walakini wataonaje?

24 Litakuwa pendeleo kubwa kama nini kujionea kwa macho yetu wenyewe hiyo “vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi” katika Har-Magedoni! Wakiwa chini ya ulinzi wake na bila kuwa na lazima ya kushiriki sehemu yo yote katika vita hiyo, mabaki ya jamii ya Yeremia na wenzi wao waliojitoa watalifurahia pendeleo hilo apa hapa duniani, palipo uwanja wa vita. Hivyo kutangaza kwao ile “siku ya kisasi upande wa Mungu wetu” kutathawabishwa kikamilifu; hakutakuwa kumekuwa kazi bure. (Isa. 61:2, NW) Ni nani awezaye kukadiria sasa furaha yao ya wakati huo, pamoja na ile ya malaika wote watakatifu wa mbinguni walio chini ya Kristo?

25. (a) “Mkutano mkubwa” wa waokokaji wataingizwa kwenye nafasi gani baada ya “vita” hiyo? (b) Taraja la mambo hayo yaliyo bora sana lapaswa kuwapa kitia-moyo gani sasa watu wote wa Yehova?

25 Wakiwa na nyuso zenye furaha, hawa walio mifano ya uwezo wa kuokoa wa Yehova watasonga mbele na kuingia taratibu yake mpya ya mambo katika dunia iliyosafishwa. Nafasi ya kuanza kujenga paradiso ya duniani pote itafunguliwa, iwe ya kufurahiwa milele na milele na “mkutano mkubwa” wenye uaminifu. Mataraja ya mambo haya yote yaliyo bora yapaswa kuwa kitia-moyo namna gani kwa wale wote wanaotamani sasa kuhesabiwa kati ya “watu wangu,” watu wa Yehova? Yapaswa kuwa kitia-moyo cha kutii amri yake yenye kuita “tokeni kwake” Babeli Mkuu mwenye kujitanguliza bila kuchelewa, na kisha kushikamana na kutokuwamo kwa Kikristo kwa habari ya wapenzi wake wote wa kisiasa, na kuunga mkono ufalme wa Yehova kupitia kwa Kristo bila kushindwa mpaka hiyo siku tukufu yenye ushindi ifike!

—Kutoka The Watchtower May 15, 1980.

(Huu ndio mwisho wa mfululizo wa makala za mafunzo juu ya unabii wa Yeremia.)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki