Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w82 8/15 kur. 4-6
  • Maisha Unayoyachagua Sasa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maisha Unayoyachagua Sasa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • MIMI KWANZA
  • KUHARIBIKA SANA KWA JAMAA
  • UHALIFU
  • NJAA
  • UHARAMIA (UGAIDI)
  • VITA NA KUMALIZIKA KABISA KWA UHAI
  • UCHAFUAJI WA HEWA, MAJI NA NCHI NA KUMALIZIKA KABISA KWA UHAI
  • Je! Wanadamu Wanaweza Kuleta Amani na Usalama Wenye Kudumu?
    Amani na Usalama wa Kweli—Wewe Unaweza Kuupataje?
  • Ugaidi Utakoma Karibuni!
    Amkeni!—2001
  • Siku za Mwisho
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
  • Je, Ugaidi Utakwisha?
    Habari Zaidi
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
w82 8/15 kur. 4-6

Maisha Unayoyachagua Sasa

Kama mwandikaji mmoja wa Biblia alivyosema zamani za kale, haya maisha unayochagua kwa kutimiza mahitaji yako ya kimwili ya kula na kunywa ‘siku zake si nyingi na yamejaa taabu.’ (Ayubu 14:1, 2) Nyingine za taabu za maisha haya zimeonyeshwa hapa chini. Je! wewe unachagua maisha haya tu? Je! sasa unaweza kufanya uchaguzi bora, uchaguzi usiokuwa na ole zote za maisha haya tunayoendeleza kwa kupumua, kula na kunywa?

MIMI KWANZA

Imani ya kina-mimi-kwanza, inayoelezwa na wanafilosofia wa u-mimi-kwanza (ubinafsi) inasema “Kutafuta aliye namba moja.” “Una haki ya kujiamulia namna mwenendo wako ulivyo.” “Lifunike kosa la kujiona kuwa na hatia.” Ibada ya sanamu ya leo ni ibada ya Mimi, kama linavyosema Neno la Mungu: “Mungu wao ni tamaa zao za kimwili.” Pia, “pupa ni namna ya ibada ya sanamu.” (Wafilipi 3:19; Wakolosai 3:5, Today’s English Version) Dini mpya hii ya Ubinafsi ilitabiriwa kwamba ingetokea nyakati zetu: “Watu watakuwa na ubinafsi.” (2 Timotheo 3:1, 2, Habari Njema kwa Watu Wote) Wonyesho wa upendo kwa Mimi unasukuma kando upendo kwa Wewe—jirani yangu.

KUHARIBIKA SANA KWA JAMAA

Ndoa inachukuliwa kuwa jambo ovyo tu, talaka zinaongezeka ajabu, watoto wanataabika huku u-mimi-mimi ukisitawi sana. “Falsafa ile ya ‘mimi-mimi’ imeshiriki kuleta ongezeko kubwa la talaka.” (Dakt. Robert Taylor) Mzazi wa ki-siku-hizi “sasa anaweka mbele ya mambo yale mengine haki yake mwenyewe ya kujitimizia mambo ya ubinafsi.” (Gazeti Newsweek) Jamaa inaumia. Hiki Kizazi cha Ubinafsi (U-mimi-mimi) hakitaki kupata masomo kutokana na yaliyotukia siku zilizopita, kwa hiyo kitarudia kutenda makosa yale yale ambayo yametendwa zamani. “Taratibu nzima za jamii ya watu zimeendelea kuwako au zikatokomea, ikitegemea kama maisha ya jamaa yalikuwa imara au dhaifu.”​—The World Book Encyclopedia, 1978.

UHALIFU

Yesu alitabiri kungekuwako “kuongezeka kwa kutokutii sheria.” (Mathayo 24:12, NW) Kizazi chetu kinahakikisha kwamba alisema kweli. Katika mwaka wa 1979, katika Amerika, “mauaji yaliongezeka kwa asilimia 10, mashambulio kwa watu yakapanda kwa asilimia 10, kulala wanawake kinguvu kwa asilimia 13 na unyang’anyi wa kutumia nguvu kwa asilimia 12. Miezi sita ya kwanza ya mwaka wa 1980, uhalifu mbaya sana uliruka kwa asilimia 10.” (U.S. News & World Report) Ndivyo ilivyo katika mataifa yale mengine. Wafanya biashara wengi ni wanyofu; wengine wengi ni wadanganyifu, wanatumia ujanja, wanaepuka kulipa kodi, wanaibia wanunuzi fedha zao kwa werevu. Na watu wengi wanaibia wafanya biashara. Ripoti moja ilisema, “Mkora Mwamerika anayejua zaidi kuiba ni yule anayefanya kazi ya ukarani.” Ni watu wasiodhaniwa kuwa wadanganyifu.

NJAA

“Kutakuwako upungufu mwingi wa chakula,” Yesu akatabiri. (Mathayo 24:7, NW) Mwaka jana gazeti Times la Los Angeles lilitoa habari hizi: “Karibu watu milioni 450 katika ulimwengu wanakufa njaa kulingana na makadirio ya watu wenye ujuzi wa kuchunguza ugawaji wa chakula, na wengine walio kati ya milioni 800 na bilioni 1 wanakaribia kufa njaa.” Dunia inazaa chakula cha kutosha, lakini ‘wenye kujipatia faida nyingi za kibiashara kutokana nacho hawataki’ kigawanywe kwa watu wote kwa kiasi kinacholingana.

UHARAMIA (UGAIDI)

Hii ni hatari yenye kuongezeka sana, kama ilivyothibitishwa na gazeti Daily News la New York la Novemba 25,1979: “Uharamia​—yaani, kuuawa kwa watawala, kutorosha watu, kupiga sehemu fulani za nchi kwa makombora, kufanya mipango ya kushambulia watu fulani waliochaguliwa—ni matukio yaliyoongezeka sana. Mwaka wa 1972 yalikuwa 206, mwaka wa 1975 yakawa 572, mwaka wa 1977 yakawa 1,256, mwaka wa 1978 yakawa 1,511, kisha yakawa 2,662 miezi tisa ya kwanza ya mwaka [1979].” Matajiri wazidipo kuwa matajiri zaidi na maskini kuwa maskini zaidi, uharamia utaongezeka zaidi na zaidi.

VITA NA KUMALIZIKA KABISA KWA UHAI

“Ufundi wa vifaa vya kijeshi umefikia kiwango cha juu sana mpaka zile serikali zilizo na nguvu kupita zote zikawa zinasogea kwenye vita isiyoepukika ya kutumia makombora ya nyukilia.” (Dakt. Frank Barnaby, mkurugenzi wa Tengenezo la Stockholm la Uchunguzi wa Amani ya Kimataifa) “Tunaamini kwamba vita ya kutumia makombora ya nyukilia haitafaidi mtu ye yote na hata huenda ikaleta mwisho wa ukuzi wa jamii ya wanadamu.” (Mtaalamu wa Urusi mwenye kuchunguza mambo ya kijeshi) “Kwa kupenda Mungu, watoto wenu, na ustaarabu ambao ninyi ni sehemu yake, acheni wazimu huu!”​—George F. Kennan, aliyekuwa balozi wa United States (Amerika) huko Moscow.

UCHAFUAJI WA HEWA, MAJI NA NCHI NA KUMALIZIKA KABISA KWA UHAI

“Dunia inazidi sana kuchafuliwa ikawe bila uhai.” (Gazeti The Globe and Mail) “Jamii ya kibinadamu imo katika hatari ya kujiletea uchafu mwingi mpaka ijiondolee mbali isiwe usoni pa dunia.” (Gazeti The Guardian) “Uchafuaji wa hewa, maji na nchi si tatizo la nchi moja moja tu: Ni tatizo la dunia nzima. . . . Tukishindwa katika jambo hili, tutathibitisha kwamba jamii yetu wenyewe ya kibinadamu itamalizika kabisa baadaye.” (Gazeti Star la Toronto) Katika hotuba iliyotolewa na Rais Carter akiliaga taifa kwa kuacha urais, yeye alionyesha kwamba uchafuaji wa hewa, maji na nchi ni “kombora lililotegwa kwa kupimiwa saa, kombora hatari sana linaloweza kumaliza dunia sawa na vile inavyoweza kumalizwa na makombora ya nyukilia.” Je! huu sio wakati wa Mungu wa ‘kuwaharibu hao waiharibuo dunia’?​—Ufunuo 11:18.

Maisha haya ya sasa siyo watu wanayopaswa kuyachagua. Hata hivyo, watu wanachagua waendelee kuishi hivyo. Huenda wakawa ni viwete, na bado wanatamani maisha; huenda wakawa ni vipofu, na bado wanaogopa kufa. Viziwi na mabubu wanachagua maisha, na wazee na walio dhaifu-dhaifu wanayashikilia kweli kweli yasiwaponyoke. Ayubu alisema, “Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu. Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.”​—Ayubu 14:1, 2.

Maisha haya ambayo watu wengi wanachagua ni mafupi. Yamejawa na taabu. Watu wamefanya uchaguzi mbaya. Lakini je! wanaweza kufanya uchaguzi mzuri zaidi?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki