Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w82 5/1 kur. 12-13
  • Je! Wewe Unaweza Kusema na Wafu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Wewe Unaweza Kusema na Wafu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Habari Zinazolingana
  • “Kutii Ni Bora Kuliko Dhabihu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Mfalme wa Kwanza wa Israeli
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Je! Kweli Wao Wanasema na Wafu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Je, Wafu Wanaweza Kuwasaidia Walio Hai?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
w82 5/1 kur. 12-13

Neno la Mungu li Hai

Je! Wewe Unaweza Kusema na Wafu?

Kwa kuwa watu wengi sana wanasema wamezungumza na wafu, ni wazi kwamba angaa baadhi yao wamesema na mtu fulani katika ulimwengu wa viumbe wa roho. Miaka zaidi ya 3,000 iliyopita, Sauli, mfalme wa Israeli, alipatwa na jambo kama hilo. Ebu tuone tunaweza kujifunza nini kutokana nalo.

Jeshi lenye nguvu la Wafilisti lilikuwa limekuja kupigana na jeshi la Sauli la Israeli, naye aliogopa sana. Sauli alikuwa anajua sheria ya Mungu: “Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi.” (Law. 19:31) Walakini Sauli alikuwa amemwacha Yehova Mungu. Na sasa, katika wakati huu wa taabu, alikuwa anahitaji sana habari hata kwamba akamwendea mchawi katika Endori.

Mchawi huyo aliweza kutokeza mfano wa mtu ambaye yeye (mchawi huyo) aliweza kuona. Kulingana na masimulizi yake ya mfano huo, Sauli aliutambua kuwa ni “Samweli.” Samweli alikuwa nabii wa Mungu aliyekuwa amekufa.

“Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu?” akauliza mtu huyo wa kiroho aliyekuwa amefikiwa.

“Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita,” Sauli akajibu.

“Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa [Yehova] amekuacha?” roho huyo akauliza.

Baada ya kupatwa na jambo hilo baya, Sauli aliogopa sana na akaanguka chini ya ardhi akiwa na moyo mzito.​—-1 Sam. 28:3-20.

Mtu huyo aliyetoka kwa ulimwengu wa viumbe wa roho hawezi kuwa alikuwa Samweli kikweli. Samweli alikuwa amekufa, na Biblia inasema “wafu hawajui neno lo lote.” (Mhu. 9:5) Zaidi ya hayo, alipokuwa angali hai Samweli alikuwa amekataa kumwona Sauli asiye mwaminifu. (1Sam. 15:35) Hakika sasa, hata kama angalikuwa hai baada ya kufa, Samweli hangekubali mchawi afanye mpango akutane na Sauli. Kwa hiyo tunaweza kuwa na hakika kwamba mchawi hangaliweza kumlazimisha Yehova ampe Sauli ujumbe kupitia Samweli aliyekufa.

Lakini namna gani kama walio hai wangaliweza kuzungumza kikweli na wapendwa wao waliokufa, kama ambavyo watu katika mkutano huu wa kichawi wanajaribu kufanya. Kama wangaliweza, kwa hakika Mungu wa upendo hangeweza kusema hivi katika Biblia: “Asionekane kwako . . . mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa [Yehova].”​—Kum. 18:10-12.

Basi, ni nani aliyekuwa akijifanya kuwa Samweli? Mtu mwovu wa roho. Pepo wabaya, au mashetani, ni malaika waliojiunga na Shetani katika kumwasi Mungu. Ili kusitawisha uongo wa kwamba kifo ni badiliko tu la kuingia kwenye uzima mwingine, wanajifanya kuwa watu waliokufa. Walakini ukweli ni kwamba wafu hawajui lo lote kabisa, na wanangojea wakati Mungu atakapowakumbuka kwa kuwafufua. (Matendo 24:15) Kwa hiyo wewe wala mtu mwingine ye yote, huwezi kuzungumza na wafu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki