Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w82 10/1 uku. 9
  • Je! Unakumbuka?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Unakumbuka?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Unakumbuka?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Je! Wakumbuka?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Je, Unakumbuka?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2024
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
w82 10/1 uku. 9

Je! Unakumbuka?

Je! umesoma matoleo ya karibuni ya “Mnara wa Mlinzi” kwa uangalifu? Ikiwa ndivyo, bila shaka utayakumbuka mambo haya:

● Kwa sababu gani kuzungumza katika lugha si sehemu ya Ukristo leo?

Kwa sababu karama ya lugha walipewa Wakristo wa karne ya kwanza peke yao, ili kuthibitisha kwamba kibali ya Mungu ilikuwa imehama kutoka kwa mpango wa ibada wa kale wa Wayahudi mpaka kwenye kundi la Kikristo lililokuwa limeanzishwa karibuni. (1 Wakorintho 13:8; Waebrania 2:2-4)—3/15 kur. 4-6.

● “Lugha safi” inayotajwa katika Sefania 3:9 ni nini?

Ni “kielelezo cha maneno yenye uzima,” yanayomsifu Yehova na makusudi yake ya haki kupitia Kristo Yesu. (2 Timotheo 1:13) —3/15 uku. 20.

● Je! ugonjwa ni adhabu ya dhambi?

Ugonjwa unaweza kuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya dhambi kama Biblia inavyosema: “Cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.” (Wagalatia 6:7) Hilo linatimia kwa wale ‘wanaopanda’ uasherati, uvutaji wa sigara, ulevi, ulafi, na kadhalika. Hata hivyo, kisababishaji kikuu cha magonjwa yote chaweza kuonyeshwa kuwa dhambi ya Adamu. (Warumi 5:12)—4/5 kur. 5, 6.

● Ukiwa mzazi unawezaje kufikia moyo wa mtoto wako?

Tangu umri mchanga, pashana habari na watoto wako, uwape msaada unaofaa wa kirafiki, kulingana na uhitaji. Wazazi wanapaswa kushirikiana kusitawisha uhusiano wa karibu wa jamaa, wao wenyewe wakiweka mfano bora katika funzo la Biblia la kawaida, sala na huduma ya shambani. Utambue kwamba msaada wa kimungu ni wa lazima ili kufikia moyo wa mtoto wako. (2 Wakorintho 4:7; Zaburi 51:5)—6/1 kur. 22, 23.

● Je! itawezekana kwa watu wenye moyo mweupe kuja upande wa Mungu baada ya “dhiki kubwa” kuanza?

Ushuhuda wa Maandiko unajibu, Hapana. Ili mtu ye yote aokoke na kuingia ndani ya taratibu mpya ya Mungu yenye haki, lazima sasa asitawishe uhusiano unaofaa pamoja na Mungu. (Mithali 18:10; Sefania 2:3)—6/15 uku. 17.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki