Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 3/15 kur. 8-9
  • Ufalme wa Mungu Ni Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufalme wa Mungu Ni Nini?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Habari Zinazolingana
  • Serikali ya Mungu ya Amani
    Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani
  • Ufalme wa Mungu Ni Nini? Na Tunaonyeshaje Kwamba Tunautaka?
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Ule Ufalme—Je! Ni Jambo Halisi Kwako?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Ufalme wa Mungu—Tumaini Peke Yake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 3/15 kur. 8-9

Neno la Mungu Li Hai

Ufalme wa Mungu Ni Nini?

YESU Kristo alipokuwa duniani kazi yake kubwa ilikuwa kuhubiri na kufundisha juu ya Ufalme wa Mungu. “Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu,” akaeleza wakati mmoja, “maana kwa sababu hiyo nalitumwa.” (Luka 4:43) Kama unavyoweza kuona hapa, Yesu alituma wafuasi wake wakafanye kazi iyo hiyo ya kuhubiri Ufalme. (Mathayo 10:1, 7) Hata alifunza wafuasi wake kumpelekea Mungu sala hii: “Ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.”—Mathayo 6:9, 10.

Ufalme wa Mungu ni nini, na kwa sababu gani ni wa maana sana?

Basi, unajua mfalme ni nini. Yeye ndiye mtawala wa nchi au eneo. Kwa sababu yeye ni mfalme, serikali yake inaitwa ufalme. Ufalme wa Mungu ni serikali pia. Biblia inaeleza juu yake kwa maneno haya: “Kwa maana kwetu sisi mtoto amezaliwa, kwetu sisi mwana amepewa: na serikali itakuwa juu ya bega lake: na jina lake litaitwa . . . Mwana-Mfalme wa Amani. Juu ya ongezeko la serikali yake hakutakuwa na mwisho.”—Isaya 9:6, 7, AV.

Mwana-mfalme huyo—Mwana huyo wa Mfalme Mkuu, Yehova Mungu—ni Yesu Kristo. Mungu amemweka awe mtawala wa serikali Yake ya Ufalme. Ili uone kwamba Ufalme wa Mungu ulikuwa suala la maana wakati wa huduma ya Kristo, fikiria lililotukia siku ya kufa kwake.

Biblia inatuambia kwamba watu walimshtaki Yesu, wakisema: “Tumemwona huyu akipotosha taifa letu, na kuwazuia watu wasimpe Kaisari kodi, akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo, mfalme.” Aliposikia hayo Pontio Pilato gavana Mrumi akamuuliza Yesu: “Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? ” —Luka 23:1-3.

Yesu hakujibu ulizo la Pilato moja kwa moja bali alisema: “Ufalme wangu sio wa Ulimwengu huu.” (Yohana 18:36) Yesu alijibu hivyo kwa sababu Ufalme wake haungekuwa wa kidunia ukihusu siasa za kibinadamu. Akiwa ndiye Mfalme aliye wa Mungu, angetawala akiwa mbinguni, si akiwa mwanadamu mwenye kukalia kiti fulani cha kifalme duniani.

Je! Umeona kutokana na Isaya ni nini kitakachoongezwa na serikali ya Mungu hata kisiwe na mwisho? Ndiyo, amani. Kwa hiyo je, sasa unaweza kuona ni kwa sababu gani serikali hiyo ni ya maana sana? Hakuna serikali ya kibinadamu inayoweza kuleta amani ya kudumu; ni Ufalme wa Mungu tu unaoweza kufanya hivyo.Yesu alitumia maisha yake duniani akiambia watu kweli nzuri ajabu juu ya serikali ya Ufalme wa Mungu. Huo ndio uliokuwa ujumbe wake mkuu. Ufalme ungali ndilo suala la maana zaidi leo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki