Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 6/15 kur. 8-9
  • Fuata Mfano wa Hana, Fuata Mfano wa Mwanaye

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Fuata Mfano wa Hana, Fuata Mfano wa Mwanaye
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Habari Zinazolingana
  • Jinsi Hana Alivyopata Amani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Mvulana Mdogo Anamtumikia Mungu
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Hana Alisali ili Apate Mwana
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Alimmwagia Mungu Mahangaiko Yake Kupitia Sala
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 6/15 kur. 8-9

Neno la Mungu Li Hai

Fuata Mfano wa Hana, Fuata Mfano wa Mwanaye

IKIWA wewe ni mama kijana, labda watoto wako wanaishi nyumbani pamoja nawe. Lakini tazama Hana na Samweli mvulana wake. Hana anamleta kwenye hema takatifu la Yehova katika Shilo. Huko ndiko makuhani wanaishi na kutumikia Mungu. Kwa sababu gani yeye analeta mwanaye aishi huko? Je! yeye hapendi mvulana mdogo wake?

Ndiyo, Hana anapenda Samweli. Lakini alipokuwa hana mtoto alipelekea Yehova sala apate mwana, na katika sala yake aliahidi hivi: ‘Mimi nitampa Yehova huyo mtoto siku zote za maisha yake.’ (1 Samweli 1:10, 11) Kwa hiyo hivyo ndivyo Hana anavyofanya. Yeye anamtoa Samweli atumikie kwenye hema takatifu la Yehova kwa muda wote uliobaki wa maisha yake.

Hana atamkosa sana Samweli. Hata hivyo ana nia ya kumwacha aende kwa sababu anapenda Yehova Mungu na anajua kwamba mwanaye anaweza kutumiwa hapo katika utumishi wa Yehova. Ikiwa wewe ni mzazi, je! una nia ya kuacha watoto wako watumiwe katika utumishi wa Yehova?

Samweli anapoendelea kukua anahitaji mavazi makubwa zaidi. Unaweza kuona Hana akimletea joho lililo jipya zaidi ambalo amemshonea. Na mama huyu anapomtembelea kila mwaka kwa uhakika anamtia moyo Samweli abaki mwaminifu katika utumishi wake kwenye hema takatifu la Yehova. (1 Samweli 2:18, 19) Je! mfano wa Hana wa kumtia moyo na kumsaidia mwanaye abaki katika utumishi wa wakati wote si mzuri kufuatwa na wazazi leo?

Lakini mfano wa Samweli ni mzuri kufuatwa na sisi sote. Yeye alikuwa na nia ya kutumiwa katika utumishi wa Mungu. Hata kama labda alikuwa anatamani sana maisha ya nyumbani kwao nyakati nyingine na kujisikia akitaka kurudi nyumbani akawe pamoja na mamaye na babaye, aliendelea tu katika utumishi wake wa hema takatifu. Samweli alikabili pia majaribu mengine ya imani yake, yaliyo magumu zaidi.

Tazama! wana wa Eli kuhani mkuu wanachukua wasichana wale wanaotumikia kwenye mwingilio wa hema takatifu kisha wataenda kulala nao na kufanya uasherati! Samweli alipokuwa akiendelea kukua, mabaya ya namna hiyo yalikuwa yakifanywa, lakini Samweli alifanya mambo yaliyokuwa mema. (1 Samweli 2:22-26) Kwa uhakika sisi ni wenye hekima tukifuata mfano wake na kuepuka kupita katika mwendo mbaya wa wale wanaoweza kuwa karibu nasi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki