Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w84 9/1 kur. 3-4
  • Ndoto Yenye Kusumbua Inayokuhusu Wewe

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ndoto Yenye Kusumbua Inayokuhusu Wewe
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ndoto ya Mfalme Huyo
  • Maana ya Ndoto Hiyo kwa Mfalme
  • Kufumbua Fumbo la Ule Mti Mkubwa
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
  • Ufalme Unaofananishwa na Mti Mkubwa
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Ufalme Ambao Utadumu Milele
    Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia
  • Wakati Yehova Wafalme Masomo Alipofunza
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
w84 9/1 kur. 3-4

Ndoto Yenye Kusumbua Inayokuhusu Wewe

ILIMWOGOPESHA na kumvuruga akili. Bila shaka mfalme huyo aliwaza, ‘Nimekwisha kuota ndoto nyingine hapo mbele na makuhani wangu, pamoja na uchawi wao, wakaweza kuzifasiri. Wakati wangeshindwa kufunua maana ya ndoto, ningewaita wafanya miujiza wangu wanieleze. Wakati wangeshindwa, hakika wanajimu wangu wangefunua siri hiyo. Lakini ndoto hii, kwa sababu gani inasumbua sana?’

Huenda ikawa Nebukadreza wa Babuloni, mtawala wa mamlaka ya ulimwengu iliyo kuu ya karne ya sita K.W.K., aliuliza hivyo. Alishindwa kupata mtu wa kufasiri ndoto yake ngeni katika milki nzima yake, isipokuwa mmoja​—mateka wa kigeni Danieli wa Yuda. Mara nyingine kabla ya hapo, mwabudu huyo wa Mungu Yehova alikuwa amemweleza Nebukadreza ndoto ambayo hakuna mwingine aliweza kuifasiri.​—Danieli 2:1-45.

Lakini huenda ukauliza: ‘Sababu gani hili linipendeze mimi? Ndoto ni sehemu ya kawaida ya maisha ya kibinadamu. Sababu gani hii iwe tofauti na nyinginezo?’ Hii ni tofauti. Jinsi gani? Kwa sababu maana yake inakuhusu wewe na kila mwingineyo yote ambaye ameishi tangu mwaka wa 1914.

Ndoto ya Mfalme Huyo

Alipokuwa akistarehe katika bustani yake yenye orofa-orofa, Nebukadreza aliota juu ya mti mkubwa ajabu:

“Njozi za kichwa changu kitandani mwangu zilikuwa hivi; naliona, na tazama, palikuwa na mti katikati ya nchi, urefu wake mkubwa sana. Mti ule ukakua, ukawa na nguvu, urefu wake ulifika mpaka mbinguni, na kuonekana kwake mpaka mwisho wa dunia. Majani yake yalikuwa mazuri, na matunda yake mengi, na ndani yake chakula cha kuwatosha watu wote; wanyama wa kondeni walipata uvuli chini yake, na ndege wa angani walikaa katika matawi yake; kila kitu chenye mwili kilipata chakula kwake.”​—Danieli 4:10-12.

Anachoona mfalme halafu katika ndoto yake kinamshtua; malaika aitoa amri hii kwa sauti kubwa:

“Ukateni mti huu, yafyekeni matawi yake, yapukusieni mbali majani yake, na kuyatawanya matunda yake, wanyama na waondoke hapo chini yake, na ndege katika matawi yake. Walakini kiacheni kisiki cha shina lake katika ardhi, pamoja na pingu ya chuma na shaba, katika majani mororo ya kondeni; kikapate maji kwa umande wa mbinguni, na sehemu yake iwe pamoja na wanyama katika majani ya nchi; moyo wake ubadilike, usiwe moyo wa binadamu, na apewe moyo wa mnyama; nyakati saba zikapite juu yake. Hukumu hii imekuja kwa agizo la walinzi, na amri hii kwa neno la watakatifu; kusudi walio hai wapate kujua ya kuwa Aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, naye humpa amtakaye, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge.”​—Danieli 4:13-17.

Maana ya Ndoto Hiyo kwa Mfalme

Utawala wa ulimwengu ndiyo habari kuu ya ndoto ya mfalme. Ndoto hiyo ina maana mbili. Moja ilimhusu Nebukadreza. Ile nyingine inakuhusu wewe. Danieli anaeleza mti huo wenye kufika mbinguni ulifananisha nini kwa habari ya Nebukadreza: “Ni wewe, Ee mfalme, uliyekua, na kupata nguvu; maana ukuu wako umekua na kufika mpaka mbinguni, na mamlaka yako yamefika mpaka mwisho wa dunia.”​—Danieli 4:22.

Halafu, Danieli anafasiri maana ya Sehemu iliyobaki ya njozi ya mfalme huyo mwenye kiburi: Nebukadreza ataanguka kwa muda katika utawala kwa ajili ya maradhi yatakayomfanya atende sawa na mnyama mwenye kula nyasi. Jambo hilo litaendelea kwa miaka saba. Lakini mara hizo “nyakati saba” ziishapo, atarudishiwa akili yake na utawala wake pia. Hilo lilifananishwa na zile pingu mbili za chuma zenye kuzuia ambazo zilifungwa kukizunguka kisiki cha shina la mti huo. Pingu hizo zikitolewa mara moja mti huo utachipuka tena. Kusudi la hayo yote, Danieli asema, ni kuthibitisha kwamba “Aliye juu ndiye anayemiliki katika ufalme wa wanadamu, naye humpa yeye amtakaye, awaye yote.”​—Danieli 4:23-26.

Miezi 12 Danieli akiisha kufasiri ndoto ya mfalme huyo, inatimia​—ghafula Nebukadreza apoteza akili yake na kofia ya kifalme yake. Miaka saba baadaye, kwa mara nyingine maneno ya Danieli yanatimia, Nebukadreza arudiwa na akili yake na anarudishwa kwenye kiti cha kifalme chake na “enzi kupita kiasi,” hayo yakamsukuma mfalme huyo akubali hivi: “Basi mimi, Nebukadreza, namhimidi Mfalme wa mbinguni, namtukuza na kumheshimu; maana matendo yake yote ni kweli, na njia zake ni za adili; na wale waendao kwa kutakabari [kiburi, NW], yeye aweza kuwadhili [kuwashusha, NW].”​—Danieli 4:29-37.

Alijifunza. Mungu, Yehova aliye Mweza Yote, ndiye mwenye kuamua ni nani atakayetawala dunia na wakati gani. Lakini maana ya ndoto ya Nebukadreza haikuwa ihusu watu katika Babuloni peke yake. Maana yake ya kiunabii ya utawala wa ulimwengu inafika katika karne hii ya 20 na inakuhusu hata wewe.

[Blabu katika ukurasa wa 4]

Ndoto ya mfalme wa Babuloni ina maana mbili. Moja inakuhusu wewe

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki