Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w85 10/1 kur. 22-23
  • Yesu na Wanajimu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu na Wanajimu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu na Wanajimu
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Wanajimu Wamtembelea Yesu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • “Wanaume Watatu Wenye Hekima” Walikuwa Nani? Je, Walifuata “Nyota” ya Bethlehemu?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Ni Nani Aliyeituma ile “Nyota”?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
w85 10/1 kur. 22-23

Maisha na Huduma ya Yesu

Yesu na Wanajimu

HESABU fulani ya wanaume wanakuja kutoka Mashariki. Wao ni wanajimu​—watu wanaodai wanatoa fasiri kuonyesha mahali nyota zilipo. Walipokuwa nyumbani Mashariki, waliona nyota mpya, nao wakaifuata kwa mamia ya maili mpaka Yerusalemu.

Wanajimu hao wanapofika Yerusalemu, wanauliza: ‘Wapi mtoto yule aliyezaliwa awe mfalme wa Wayahudi? Tuliona nyota yake nasi tumekuja kumsujudia.’

Mfalme Herode katika Yerusalemu anaposikia hilo, anaudhika sana. Kwa hiyo anawaita makuhani wakuu na kuuliza: ‘Kristo atazaliwa wapi?’ Wakitegemeza jibu lao kwenye Maandiko, wanajibu: ‘Katika Bethlehemu.’ Ndipo Herode anaamuru wanajimu hao waletwe kwake naye anawaambia: ‘Nendeni mkamtafute mtoto huyo, na mkiisha kumpata, rudini mniambie ili niende nikamsujudie pia.’ Lakini, moyoni, Herode anataka kumpata mtoto huyo ili amuue!

Wakiisha kuondoka jambo la ajabu linatokea. Nyota waliyoona walipokuwa Mashariki inasafiri mbele yao. Kwa wazi, hiyo si nyota ya kawaida, lakini imetolewa hasa iwaelekeze. Wanajimu hao wanaifuata mpaka inaposimama pale pale juu ya nyumba ambamo Yusufu na Mariamu wanaishi.

Wanajimu hao wanapoingia ndani ya nyumba hiyo, wanamkuta Mariamu na mtoto wake mchanga, Yesu. Ndipo wote wanaposujudia. Kisha wanatoa mifuko yao ya zawadi za dhahabu, uvumba na manemane. Baadaye, wanapokaribia kurudi wakamwambie Herode aliko mtoto, wanaonywa na Mungu katika ndoto wasifanye hivyo. Kwa hiyo wanaondoka kwenda kwenye nchi yao wakipitia njia nyingine.

Unafikiri ni nani aliyetoa nyota hiyo iliyosonga katika anga iwaongoze wanajimu hao? Kumbuka, nyota hiyo haikuwaongoza moja kwa moja kwa Yesu katika Bethlehemu. Badala yake, waliongozwa mpaka Yerusalemu ambako walikutana na Herode, aliyetaka kumuua Yesu. Naye angalifanya hivyo kama Mungu hangejiingiza na kuwaonya wanajimu hao wasimwambie Herode. Adui ya Mungu, Shetani Ibilisi, ndiye aliyetaka kumuua Yesu, naye alitumia nyota hiyo ajaribu kutimiza kusudi lake. Mathayo 2:1-12; Mika 5:2.

◆ Ni nini kinachoonyesha kwamba nyota ambayo wanajimu waliona haikuwa nyota ya kawaida?

◆ Yesu alikuwa wapi wanajimu hao walipompata?

◆ Tunajuaje kwamba Shetani alitoa nyota hiyo iwaongoze wanajimu hao?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki