Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 3/15 uku. 30
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Samsoni Ashinda kwa Nguvu za Yehova!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Mtegemee Yehova Kama Samsoni Alivyofanya
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Mwanamume Mwenye Nguvu Kuliko Wote
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 3/15 uku. 30

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

■ Biblia inasema kwamba Samsoni alirarua simba “sawasawa na vile mtu anavyopasua mtoto wa kiume wa mbuzi vipande viwili.” Je, hiyo inamaanisha kwamba siku hizo ilikuwa kawaida ya watu kupasua wana-mbuzi?

Hapana, inaelekea kwamba elezo hilo lilikuwa mfano tu. Lilimaanisha kwamba Samsoni alimlemea simba kwa mikono mitupu kama kwamba simba huyo alikuwa mwana-mbuzi tu asiyeweza kujitetea.

Samsoni, ambaye alikuwa akitumikia akiwa mwamuzi katika Israeli, alisafiri kwenda Timna ili apate “nafasi dhidi ya Wafilisti.” Akiwa njiani alikutana na simba mwenye kunguruma, mchanga na mwenye nguvu. Na huenda ikawa simba huyo alimshambulia yeye. Kumbukumbu la kihistoria linasema kwamba kani ya utendaji wa Mungu ilimjilia Samsoni “hivi kwamba akampasua vipande viwili [simba huyo], sawasawa na vile mtu anavyopasua mtoto wa kiume wa mbuzi vipande viwili, tena hakukuwa kabisa na kitu mkononi mwake.”​—Waamuzi 14:4-6, NW.

Kuna wanaume wengine wawili katika kumbukumbu la Biblia walioua simba, kila mmoja akiwa peke yake, lakini ni Samsoni tu anayesemwa kuwa alifanya hivyo kwa mikono mitupu. (1 Samweli 17:36; 2 Samweli 23:20) Zaidi ya hilo, yeye ‘alimpasua vipande viwili.’ Ikiwa hiyo ilimaanisha kwamba alizipasua taya zenye nguvu za simba huyo, inaweza kufikiriwa kwamba Waisraeli fulani walikuwa na nguvu za kutosha kumfanya vivyo hivyo mwana-mbuzi. Lakini hakuna ushuhuda wa kwamba walifanya hivyo, wala sababu yoyote ambayo ingewafanya wajaribu kutenda hivyo. Kwa upande mwingine, ikiwa kwa njia fulani Samsoni alimpasua simba huyo ‘visehemu visehemu,’ ingekuwa vigumu zaidi kusemwa kwamba elezo lile linalomhusu halikuwa halisi ila kifananisho tu. Maana ni kwamba roho ya Mungu ilimpa Samsoni nguvu za ajabu za kimwili. Kwa kupewa msaada huo, simba huyo mkali hakumtisha Samsoni asiye na silaha, sawa tu na vile mwana-mbuzi asivyoweza kutisha mwanamume wa kawaida.

Baadaye mzoga wa simba huyo ulitajwa katika kitendawili, na hapo tena kikatokea kisa cha Mungu kumtia Samsoni nguvu, na pindi hii aliua watu 30 kati ya adui.​—Waamuzi 14:8-19.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki