Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w86 5/15 uku. 3
  • Wakati Ujao Wako Ni Nani Anayeweza Kuutabiri?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wakati Ujao Wako Ni Nani Anayeweza Kuutabiri?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Habari Zinazolingana
  • Mwongozo Unaotegemeka kwa Ajili ya Wakati Ujao
    Amkeni!—2002
  • Je, Inawezekana Kujua Wakati Ujao?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
  • Ni Nani Anayeweza Kujua Wakati Ujao?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Utabiri Fulani Hutimia Lakini Mwingi Hautimii
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
w86 5/15 uku. 3

Wakati Ujao Wako Ni Nani Anayeweza Kuutabiri?

KUJARIBU kuutabiri wakati ujao ni rahisi. Lakini kuwa sahihi katika utabiri huo si rahisi. Inakuwa kawaida kuyaona matabiri kuwa ya bure tu wakati yanapozidi-zidi kutokulingana na yalivyosemwa, kama mifano hii inavyoonyesha waziwazi.

Tangu nyakati za kale, mwanadamu amejaribu kugundua mambo yaliyoko wakati ujao. Hata leo, walio wengi kati yetu tuna tamaa ya kuchungulia yatakayotukia kesho. Utafutaji huo wa maarifa kuhusu matukio yanayokuja umeongoza mwanadamu ajaribu kutumia njia nyingi sana. Kwa mfano, mwili wa kibinadamu umechunguzwa ili hali za uso, mistari-mistari katika fuvu la kichwa, na vistari vilivyo katika kiganja cha mkono vidokeze mambo fulani. Mwanadamu amechunguza wanyama—miendo ya vipanya au nyoka, mruko wa ndege, hata njia ambayo jogoo anadondoa haraka chembe za mtama zilizowekwa chini. Wengine wametumia vitu kama matufe ya kioo, karata, majani-chai, au unga-unga wa kahawa. Njia mbalimbali zinatumiwa kwa kutegemea watu, desturi, na vipindi mbalimbali, lakini matokeo ni yale yale: kushindwa.

Hata hivyo, kuna Mmoja anayeweza kuutabiri wakati ujao kwa usahihi. Nani? Yehova Mungu. Yehova hana kifani kwa sababu ndiye ‘atangazaye mwisho tangu mwanzo.’ Mungu anaweza kutabiri upeo utakuwa nini hata kama matukio hayajakamilika. Ndiyo, Yehova anaweza kuufunua wakati ujao mbele ya macho ya mwanadamu si siku chache tu mapema bali karne nyingi kabla haujafanyika!—Isaya 46:10.

Basi, si lazima ufuatiaji wa maarifa ya kuujua wakati ujao uwe kazi bure. Neno la Mungu, Biblia, limeeleza mambo yaliyo ya maana zaidi kwetu. Linaonyesha nini hasa kuwa ndiyo mambo yaliyo mbele ya wanadamu?

[Picha katika ukurasa wa 3]

“Haiwezekani kuwe na mashine zenye kuruka zilizo nzito kuliko hewa.”—Mheshimiwa Kelvin, mhisabati, Mwingereza aliye mtaalamu wa mambo ya fisikia, na Msimamizi wa British Royal Society, karibu na mwaka 1895.a

[Maelezo ya Chini]

a Mitajo hii imetokana na kitabu The Experts Speak (Wataalamu Wasema), kilichotungwa na Christopher Cerf na Victor Navasky.

“Ili tuanze kujaribu kuelewa jinsi maisha yatakavyokuwa mwaka 1960, ni lazima tuanze kwa kutambua kwamba chakula, mavazi na makao yatakuwa na bei ya chini kama vile hewa.”—John Langdon-Davies, Mwingereza aliye mwandikaji wa habari za jarida na Mshiriki wa Royal Anthropological Institute, 1936.

“Huu ndio upumbavu mkubwa zaidi ambao tumepata kuufanya.. . . Kombora halitakoma kamwe, nami naongea kama mtaalamu wa vitu vilipukavyo.”—Admeri William Leahy, akimshauri Rais Harry Truman wa U.S. juu ya mpango wa U.S. wa kombora la atomi, mwaka 1945.

[Credit Line]

U.S. National Archives

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki