Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 2/15 uku. 3
  • Je! Ufuataji Haki Ni wa Kikale?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Ufuataji Haki Ni wa Kikale?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Habari Zinazolingana
  • Maana Yake Nini Kuwa Mfuataji Haki?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Uwe Mnyofu Katika Mambo Yote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Uwe Mnyoofu Katika Mambo Yote
    “Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
  • Uwe Mnyoofu Katika Mambo Yote
    Jinsi ya Kudumu Katika Upendo wa Mungu
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 2/15 uku. 3

Je! Ufuataji Haki Ni wa Kikale?

KUUNGA mkono ufuataji haki uwe njia ya maisha—je! jambo hilo limekuwa la kale katika ulimwengu wa ki-siku-hizi, likaachiliwa mbali kuwa lisilo tena na mafaa au lisilo na thamani yoyote halisi? Ingeelekea kuwa hivyo. Fikiria vielelezo vichache tu vya jinsi ukosefu wa ufuataji haki umeenea sana, fikiria namna-namna za ukosefu huo, viwango ambavyo umepenya ndani, na jinsi umekuwa himila yenye hasara kubwa.

Katika miaka ya majuzi, hasara yenye kuletwa na upunjaji wa kodi katika Ujeremani Magharibi imekadiriwa kuwa dola bilioni 10 (za United States) kwa mwaka, na katika Sweden hasara ya kila mwaka inafikia dola 720 (za United States) kwa kila mtu. Kwa hiyo ikiwa wewe unaishi katika lolote la mabara mawili hayo, ukosefu wa ufuataji haki unaathiri kile ambacho wewe unalipa kwa kodi. Kudanganya juu ya malipo ya kodi ya mapato kumeenea sana katika United States hivi kwamba serikali inapoteza kiasi kinachokadiriwa kuwa dola bilioni 100 katika mapato ya kiserikali kila mwaka. Fikiria pesa zote hizo zingeweza kuwa msaada mkubwa kama nini katika kulipia ule upungufu mkubwa sana wa matumizi ya kipesa kwa serikali kuu! Zaidi ya hilo, biashara zisizo halali zinatenda serikali ya United States udanganyifu wa dola nyingine bilioni 10. Wizi wa kuchomoa-chomoa vitu madukani na wa kuiba vitu vidogo-vidogo katika United States unaletea maduka hasara ya dola bilioni 4 kwa mwaka, hiyo ikifanya bei za vitu zipande juu. Ukosefu wa ufuataji haki unaletea Waamerika hasara ya dola milioni 1 kila mwaka kwa kutoza gharama za simu za mbali katika namba za watu ambao sio waliopiga simu hizo.

Katika Kanada “majizi ya wakati,” wale ambao wanapoteza ovyo wakati wakiwa kazini, wanawaletea waajiri-kazi wao hasara ya dola bilioni 15 (za Kanada) kwa mwaka, “zaidi ya mara tatu za jumla ambayo inapotea kupitia waajiriwa-kazi wenye mikono mirefu, kupitia udokozi-dokozi, upunjaji wa bima, ubomoaji wa vitu vya wengine bila sababu, rushwa, uteketezaji wa vitu vya wenyewe na matendo mengine halisi yanayofanywa dhidi ya biashara.” Kulingana na uchunguzi mmoja wa 1986, ile himila inayotokana na wizi wa wakati katika United States ni dola bilioni 170 kila mwaka.

Mashirika yanayoendesha kazi kwa mafanikio kwa kutegemea mamilioni mengi sana ya dola yanaiba kwa pupa kutoka kwa serikali zayo yenyewe. Jinsi gani? Kwa kuziuzia vyombo vya kazi na visehemu vya vyombo hivyo kwa bei za juu mno: vikaza-misumari vya senti 12 vikiuzwa kwa dola 9,606 (za United States); transista za senti 67 zikiuzwa kwa dola 814; vifuniko-plastiki vya miguu ya vibago vya senti 17 vikiuzwa kwa dola 1,118. “Linalosemwa ni juu ya mabilioni ya dola” za hasara kwa serikali, akasema seneta mmoja wa United States.

Kuongezea yaliyo juu, vielelezo vibaya vinavyowekwa kila upande na watu mashuhuri vinavunja moyo ufuataji haki. Kama vile ambavyo huenda wewe ukawa umeona, viongozi katika mabara fulani wanasema uwongo, wanasingizia, wanaficha ubaya, na kuepa daraka lao—ndivyo, hata wanaua watu walio washindani wao wa kisiasa na kufanya ionekane kama kwamba mtu mwingine ndiye wa kulaumiwa.

Kwa hiyo, je! kuwa mfuataji haki ni jambo la kikale? Je! kumeacha kuwa njia bora zaidi ya kuendeshea mambo? Je! ufuataji haki ni bora zaidi kwa sababu tu Neno la Mungu ndilo linatuambia sisi kwamba lazima tuwe wafuataji haki? Makala inayofuata ni ya maana kwako ikiwa wewe unataka majibu kwa maswali hayo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki