Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w88 12/1 kur. 8-9
  • Yesu Aelekea Yerusalemu Tena

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Aelekea Yerusalemu Tena
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu Aelekea Tena Yerusalemu
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Huduma ya Yesu Huko Perea
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • “Saa Yake Ilikuwa Haijaja Bado”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Yerusalemu—“Sababu ya Shangwe”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1983
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
w88 12/1 kur. 8-9

Maisha na Huduma ya Yesu

Yesu Aelekea Yerusalemu Tena

BAADA ya muda mfupi Yesu yuko mwendoni tena, akifundisha jiji kwa jiji na kijiji kwa kijiji. Ni wazi yeye yumo katika wilaya ya Perea, ng’ambo ya Mto Yordani kutoka upande wa Yudea. Lakini mahali anakoelekea ni Yerusalemu.

Labda ile falsafa ya Kiyahudi kwamba watu wa hesabu ndogo tu ndio watastahili wokovu ndiyo inasukuma mwanamume mmoja kuuliza hivi: “Bwana, je! wale wanaookolewa ni wachache?” Kwa jibu lake, Yesu anatia kani watu wafikirie kinachohitajiwa ili kupata wokovu: “Jikazeni kisulubu [yaani, ng’ang’anieni sana, au jitieni maumivu makali sanaj ili kuingia kupitia ule mlango mwembamba.”

Jitihada kama hiyo ya kisulubu inahitajiwa kwa haraka “kwa sababu wengi,” Yesu anaendelea kusema, “watatafuta kuingia lakini hawataweza.” Kwa nini hawataweza? Yeye anaeleza kwamba ‘mara mwenye nyumba akiisha kuwa ameinuka na kutia kufuli kwenye mlango na watu wanasimama nje na kupiga hodi, wakisema, “Bwana, utufungulie,” yeye atasema: “Mimi sijui nyinyi ni wa kutoka wapi. Ondokeni mbali kutoka kwangu, nyinyi nyote wafanya kazi wa ukosefu wa uadilifu.”’

Inaonekana kuwa wanaofungiwa nje kwa kufuli wanakuja wakati unaowafaa wao wenyewe tu. Lakini kufikia hapo mlango wa fursa unakuwa umefungwa na kutiliwa komeo. Ili waingie ingaliwapasa kuja mapema kidogo, hata ingawa huenda ikawa wakati huo usingalikuwa mzuri kwao kufanya hivyo. Kweli kweli, tokeo la kuhuzunisha linangojea wale wanaoahirisha kufanya ibada ya Yehova iwe ndilo kusudi lao kuu maishani!

Wayahudi ambao Yesu anatumwa kwao akawahudumie wameshindwa, kwa sehemu kubwa zaidi, kushika fursa nzuri sana waliyo nayo ya kukubali uandalizi wa Mungu kwa ajili ya wokovu. Kwa hiyo Yesu anasema watalia machozi na kusaga meno yao wakati watatupwa nje. Kwa upande ule mwingine, watu kutoka “sehemu za mashariki na za magharibi, na kutoka kaskazini na kusini,” ndiyo, kutoka mataifa yote, “wataegemea kwenye meza katika ufalme wa Mungu.”

Hivyo, kama vile Yesu anavyoendelea kusema: “Kuna wale walio wa mwisho [wati wadharauliwa wasio Wayahudi, na pia Wayahudi wenye kukandamizwa] ambao watakuwa wa kwanza, na kuna wale walio wa kwanza [Wayahudi waliopendelewa kufanikiwa kwa vitu vya kimwili na kwa njia ye kidini] ambao watakUwa wa mwisho.” Kuwe wa mwisho kunamaanisha kwamba wakosa-shukrani hao wenye kujikokota kwa mwendo wa pole mno hawatakuwa kamwe katika Ufalme wa Mungu.

Sasa Mafarisayo wanamjia Yesu na kusema: “Nenda nje na ushike njia ya kutoka hapa.kwa sababu Herode [Antipa] anataka kuua wewe.” Huenda ikawa Herode mwenyewe ndiye aliyeanzisha uvumi huo ili kusababisha Yesu akimbie kutoka eneo hilo. Huenda ikawa Herode aliogopa kuhusika katika kifo cha mnabii mwingine wa Mungu kama vile alivyohusika katika kuua Yohana Mbatizaji. Lakini Yesu anaambia Mafarisayo hao: “Nendeni mkaambie mbweha huyo, ‘Tazama! Mimi natupa nje roho waovu na kufanya uponyaji leo na kesho, na siku ya tatu nitakuwa nimemalizika.”’

Baada ya kumaliza kazi yake huko, Yesu anaendelea na safari yake kuelekea Yerusalemu kwa sababu, kama vile yeye anavyoeleza, “hairuhusiki mnabii kuharibiwa nje ya Yerusalemu.” Kwa nini inapasa kutarajiwa kwamba Yesu angeuawa katika Yerusalemu? Kwa sababu Yerusalemu ndilo jiji kuu, ilimo mahakama kuu ya Sanhedrini yenye washiriki 71 na ambamo dhabihu za wanyama hutolewa. Kwa hiyo, lingekuwa jambo lisiloruhusika “MwanaKondoo wa Mungu” kuuawa mahali pengine isipokuwa katika Yerusalemu.

“Yerusalemu, Yerusalemu, muuaji wa wanabii na mpigaji-mawe wa wale waliotumwa waende kwake,” Yesu anaomboleza, “ni mara nyingi kadiri gani mimi nimetaka kukusanya watoto wako pamoja kwa namna ambayo kuku hukusanya otamio la vifaranga chini ya mabawa yake, lakini nyinyi watu hamkutaka hilo! Tazameni! Nyinyi mmeachiwa ukiwa nyumba yenu.” Kwa kumkataa Mwana wa Mungu, taifa hilo lilihukumiwa maangamizi!

Yesu anapoendelea kuelekea Yerusalemu, yeye anaalikwa kwenye nyumba ya mtawala mmoja wa Mafarisayo. Ni Sabato, na watu wanamtazama kwa ukaribu, kwa kuwa hapo pana mwanamume aliye na ugonjwa wa kujazana-jazana maji mwilini, labda katika mikono na miguu yake. Yesu anasema kwa Mafarisayo na wastadi wa Sheria waliopo, akiuliza: “Je! ni jambo la kisheria siku ya sabato kuponya au sivyo?”

Hakuna mtu anayesema neno. Kwa hiyo Yesu anaponya mwanamume huyo na kumwambia aende zake. Ndipo yeye anapouliza: “Ni nani kati ya nyinyi, ikiwa mwana au ng’ombe dume wake anatumbukia ndani ya kisima, ambaye hatamvuta nje mara hiyo siku ya sabato?” Hapo tena, hakuna mtu anayesema neno kwa kujibu. Luka 13:22–14:6; Yohana 1:29, NW.

◆ Yesu anaonyesha ni nini kinachohitajiwa ili kupata wokovu, na kwa nini wengi wanafungiwa nje kwa kufuli?

◆ Walio “wa mwisho” wanaokuwa wa kwanza ni akina nani, na walio “wa kwanza” wanaokuwa wa mwisho ni akina nani?

◆ Inawezekana ni kwa nini ilisemwa kwamba Herode alitaka kuua Yesu?

◆ Kwa nini hairuhusiki mnabii kuuawa nje ya Yerusalemu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki