Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 2/1 kur. 3-4
  • Uzuri Huenda Ukawa wa Juujuu Tu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uzuri Huenda Ukawa wa Juujuu Tu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jambo Fulani Linalozidi Uzuri
  • Mitego ya Uzuri wa Kimwili
  • Uzuri wa Kiume
  • Urembo Ulio Bora Zaidi
    Amkeni!—2004
  • Uzuri wa Kweli—Wewe Unaweza Kuusitawisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Urembo
    Amkeni!—2016
  • Yaliyomo
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 2/1 kur. 3-4

Uzuri Huenda Ukawa wa Juujuu Tu

HAWA, mwanamke wa kwanza na wa pekee kuumbwa na Mungu, yaelekea alikuwa ndiye mwanamke mzuri kupita wote waliopata kuishi. Lakini yeye na mume wake, Adamu, waliasi dhidi ya Yehova. Kwa hiyo Hawa akapoteza uhusiano wake wa karibu pamoja na Mungu na akashiriki kuleta tanzia mbaya sana juu ya jamii ya kibinadamu. Baadaye, bila shaka yeye alikuwa angali na uzuri, lakini uzuri wake ulikuwa wa juujuu tu.

Kwa msingi uzuri ni zawadi ya Mungu, na watu fulani wamerithi kadiri kubwa ya uzuri huo kuliko wengine. Watu fulani huona ni laiti wangalikuwa na uzuri mwingi kuliko ule walio nao, na wengi wanatumia wakati na pesa nyingi wakijitahidi kufanya sura yoyote waliyo nayo ionekane nzuri iwezekanavyo. Lakini kama vile kielelezo cha Hawa kinavyoonyesha, uzuri tu huja kuwa wa bure usipoandamana na sifa nyinginezo. Sifa gani nyinginezo? Jambo moja lililoonwa kule nyuma katika siku za Mfalme Sulemani linatusaidia kujibu.

Jambo Fulani Linalozidi Uzuri

Kitabu cha Biblia cha Wimbo wa Sulemani kinasimulia juu ya msichana mzuri wa mashambani, Mshulami, aliyekuwa katika upenzi pamoja na mvulana mchungaji wa kwao. Uzuri wa msichana huyo ulivutia fikira za mfalme yule, naye akaagiza kwamba aletwe Yerusalemu kwa matumaini ya kumfanya mke wake. Lo, fursa kubwa kama nini kwa kijana mwanamke! Akiwa huko, yeye angeweza kutumia uzuri wake umpatie cheo cha utajiri, mamlaka, na umashuhuri katika ufalme huo. Lakini msichana huyo aliyakataa katakata matongozi yenye rairai nyingi za mfalme. Yeye aliupa kisogo umerimeti na utajiri wa Yerusalemu na kubaki mwaminifu kwa mvulana wake mchungaji. Katika kisa chake, uzuri haukuwa wa juujuu tu. Yeye hakuwa na akili haba, mtu wa kurukia fursa mara tu zijitokezapo, wala hakuwa mwenye pupa. Bali, alikuwa na uzuri wa kindani asiokuwa nao Hawa nyanya yake wa kale.​—Wimbo wa Sulemani 1:15; 4:1; 8:4, 6, 10.

Mitego ya Uzuri wa Kimwili

Ingawa ni wa kutamanika, uzuri wa kimwili unaweza kuongoza kwenye matatizo ambayo uzuri wa kindani hauyatokezi kamwe. Mathalani, karibu miaka 4,000 iliyopita Yakobo mzee wa ukoo alikuwa na binti mmoja jina lake Dina ambaye bila shaka alikuwa mrembo sana. Binti huyo alipokosa hekima kwa kushinda akiwa katika ushirika pamoja na “binti za nchi,” kijana mwanamume jina lake Shekemu alivutiwa sana naye hata akamnajisi.​—Mwanzo 34:1, 2.

Kwa kuongezea, sura nzuri ya nje, isipoambatanishwa na uzuri wa kindani, inaweza kufanya mwenye sura hiyo ajikadirie ubora mwingi kwa maringo. Mfalme Daudi alikuwa na mwana ambaye jina lake lilikuwa Absalomu, tunayesoma hivi juu yake: “Basi katika Israeli wote hapakuwa na mtu hata mmoja mwenye kusifiwa kwa uzuri wake kama huyo Absalomu.” (2 Samweli 14:25) Lakini uzuri wa kimwili wa Absalomu ulikuwa kibandiko cha kuficha sura fulani mbaya ya ndani: Yeye alikuwa mtu mbatili, mtaka makuu, na asiye na huruma. Kijana huyo aliutumia kwa ustadi uvutio wake wa kibinafsi kujifanyizia wafuasi katika Israeli halafu akatunga hila dhidi ya baba yake aliyekuwa mfalme. Mwishowe kijana huyo mwenye sura ya kupendeza sana aliuawa lakini si kabla ya kutumbukiza ufalme huo katika vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Uzuri wa Kiume

Kama vile kisa cha Absalomu kinavyoonyesha, Biblia inanena juu ya wanaume na wanawake kadhalika kuwa wazuri. Kielelezo kimoja cha mwanamume ambaye hakutegwa na uzuri wake wa kiume kilikuwa Yusufu, ndugu-nusu aliye mchanga zaidi wa Dina. (Mwanzo 30:20-24) Alipokuwa kijana, ndugu za Yusufu walimuuza kwa wivu awe mtumwa ili achukuliwe apelekwe Misri. Akiwa huko, yeye alinunuliwa na ofisa wa kijeshi jina lake Potifa, na kwa sababu ya kuwa mfuata haki na bidiiendelevu, akaja kuwa mwangalizi wa watu wa nyumba ya Potifa. Katika muda huo, “Yusufu alikuwa mtu mzuri, na mwenye uso mzuri.”​—Mwanzo 39:6.

Mke wa Potifa alisitawisha harara kwa Yusufu na bila aibu akajaribu kumtongoza. Lakini kijana huyo alionyesha kwamba alikuwa na uzuri wa kindani hali moja na uvutio wa kimwili. Yeye alikataa kutenda dhambi dhidi ya bwana wake, Potifa, naye akamkimbia mwanamke huyo. Tokeo ni kwamba, alisukumizwa jela. Kwa nini? Mke mtamaushwa wa Potifa alimshtaki kiuwongo kwamba alijaribu kumnajisi! Hata tukio hilo chungu halikumfanya Yusufu awe na nia ya kasirani-kasirani, na kielelezo chake bora akiwa chini ya ugumu mkali sana kimewatia moyo watu wenye mioyo ya kufuatia haki tangu wakati huo.

Kama inavyoonyeshwa na vielelezo hivyo, uzuri wa kindani​—uzuri wa utu hasa wakati msingi wao unapokuwa ni imani katika Mungu—​unazidi kwa mbali umaana wa sura nzuri ya kimwili. Vijana wanaofikiria ndoa wanahitaji kujua jambo hilo. Waajiri wanaotafuta wafanya kazi wamepaswa kulikumbuka. Na sisi sote tunapaswa kuzingatia akilini kwamba kama tumebarikiwa au hatukubarikiwa kuwa na uzuri wa kimwili, tunaweza kusitawisha uzuri huo wa kindani ambao umaana wao unauzidi huo mwingine kwa mbali. Lakini je! ni mambo gani yanayohusika katika uzuri huo? Nasi tunaweza kuusitawishaje? Tutazungumzia hilo katika makala inayofuata.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki