Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 3/15 kur. 23-25
  • Kaisaria na Wakristo wa Mapema

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kaisaria na Wakristo wa Mapema
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Usimamizi wa Kiroma
  • Ule Wonyesho
  • “Mapenzi ya Yehova na Yatendeke”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
  • Herode Mkuu—Mjenzi Stadi
    Amkeni!—2009
  • Kitabu Kinachotegemeka—Sehemu ya 6
    Amkeni!—2011
  • “Hazina za Nchi Takatifu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1987
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 3/15 kur. 23-25

Kaisaria na Wakristo wa Mapema

Kaisaria jiji la kale la pwani, lililowekwa msingi na Herode Mkuu muda mfupi kabla ya Yesu Kristo kuzaliwa, hivi majuzi limekuwa mahali pa uchimbuzi wenye kugundua vitu vingi vya kale. “Ndoto ya Mfalme Herode,” ambao ni wonyesho wa vitu hivyo vilivyopatikana, sasa umo katika safari ya kutalii Amerika ya Kaskazini.a

Herode alijipendekeza kwa mmaliki Mroma Kaisari Agusto ili kupata kibali chake. Hivyo, yeye akaliita jiji hilo Kaisaria (maana yake, “Mali ya Kaisari”) na kukiita kibandari chalo Sebastosi (neno la Kigiriki kwa “Agusto”). Wafanya kazi wa Herode walijenga bandari ya kustaajabisha ili iwe ya meli labda mia moja, na wakajenga hekalu lenye fahari likiwa na sanamu kubwa ya ibada ya mmaliki.

Usimamizi wa Kiroma

Kaisaria likawa kao rasmi la wakuu wa sheria za Kiroma​—wanaume waliosimamia Yudea. Kaisaria kilikuwa kitovu cha utendaji wa kisiasa na kijeshi wa Roma. Hapo ndipo Kornelio ofisa wa kijeshi na “jamaa zake na rafiki zake [wa usiri, NW]” walipata kuwa watu wa kwanza wasio Wayahudi kuukubali Ukristo. (Matendo, sura 10) Filipo mweneza-evanjeli alienda Kaisaria, vilevile mtume Petro. Baadhi ya meli ambazo mtume Paulo alitumia katika safari za utalii wake wa kimisionari zilitia nanga kwenye bandari ya Kaisaria. Na karibu mwaka 56 W.K., Paulo na Luka walikaa katika nyumba ya Filipo, ambaye yaonekana alikuwa ametulia huko na binti zake wanne wakawa pia wakitumikia Mungu.​—Matendo 8:40; 12:18, 19; 18:21, 22; 21:8, 9.

Kaisaria ndiko Paulo aliletwa aje mbele ya Feliki gavana Mroma. Huko pia ndiko Paulo alitamka maneno yake maarufu kwa kumwambia Festo: “Nataka rufani kwa Kaisari”!​—Matendo, sura 23-26.

Ule Wonyesho

Unapoingia wonyesho huu, unakabiliana na sanamu ya Tike, mungu-mke wa Kaisaria. Jina lake linamaanisha “Bahati” au “Nasibu Njema.” Hata hivyo, Wakristo wa huko hawakuitibari katika mungu-mke wa bahati bali katika Mungu wa kweli, Yehova. Pia walikuwa na imani katika Yesu Kristo, yule ambaye Mfalme Herode alikuwa amejaribu kumuua.

Katika vyumba viwili vinavyofuata, unaona jinsi wachimbuzi wa vitu vya kale walivyofukua vitu vilivyopatikana Kaisaria na jinsi bandari ilivyojengwa. Ndipo, katika chumba cha nne, unaona nakala iliyofanywa upya ya moja la mapato makubwa yaliyopatikana Kaisaria. Mwandiko pekee ndio mchoro wa maneno yanayojulikana kuwa yaliandikwa na gavana Mroma ambaye Yesu Kristo alipelekwa mbele yake. Mchoro huo unasomeka hivi: “Pontio Pilato, liwali wa Yudea.”

Pia ndani ya chumba hicho mna sarafu ndogo mbili za shaba zinazopendeza sana sana. Ya kwanza (upande wa kulia) ina mchoro huu: “Mwaka wa pili wa uhuru wa Sayuni.” Juu ya ile ya pili yapo maneno haya: “Mwaka wa nne hadi kukombolewa kwa Sayuni.” Sarafu hizo zinasemwa na wanachuo kuwa ni za 67 W.K. na 69 W.K. “Uhuru” unaotajwa ulikuwa kipindi ambacho Wayahudi walishikilia Yerusalemu, baada ya Sestio Galo kuondoa majeshi yake ya Kiroma katika mwaka 66 W.K.

Kuondoka huko kulifanya iwezekane kuikimbia Yerusalemu. Watu walioitikadi Yesu walikimbia, kwa maana alikuwa amesema waziwazi hivi: “Hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Ndipo walio katika Uyahudi na wakimbilie milimani, na walio katikati yake wakimbilie nje, na walio katika mashamba wasiuingie.” (Luka 21:20, 21) Inaonekana kwamba wenye kufanyiza sarafu hizo “za ushindi” hawakujua ni uharibifu gani uliowangojea!

Katika mwaka 70 W.K., jeshi la Kiroma lilirudi, likashinda Yerusalemu, na kuharibu hekalu. Kulingana na Yosefo, waliua zaidi ya watu milioni moja waliokuwa wamesongamana jijini kwa ajili ya sikukuu ya Kupitwa. Tito jemadari Mroma aliadhimisha ushindi huo​—na siku ya kuzaliwa kwa Domitia ndugu yake​—kwa kufanya michezo katika uwanja wa maonyesho wa Kaisaria. Huko wafungwa 2,500 walitupwa kwenye hayawani-mwitu, wakachomwa kwa moto, au wakauawa katika michezo hatari ya kupambana na adui.

Chumba kinachofuata cha wonyesho huo kina sanam ya mungu-mke wa nguvu za uzazi mwenye matiti mengi, Artemi wa Efeso. Huyo huyo ndiye yule mungu-mke ambaye waabudu wake walifanya ghasia katika Efeso wakati kuhubiri kwa Paulo kuliposababisha watu wengi waikatae ibada ya kuchukiza sana na kumfuata Yesu Kristo.​—Matendo 19:23-41.

Wonyesho mmoja wa vigae vya vyungu unaonyesha umbali ambao watu walisafiri katika karne ya kwanza kama inavyofunuliwa katika Maandiko. Katika bohari moja tu la kale, vipande vya vyungu vilipatikana mahali-mahali palipotenganishwa na umbali mkubwa sana kama vile Yugoslavia, Italia, Hispania, na labda Afrika ya Kaskazini. Kwa kuwa watu walisafiri umbali mkubwa hivyo, ni rahisi kuelewa kwamba wenye kuzuru kutoka ncha za mbali za Milki ya Roma wangaliweza kuwa katika Yerusalemu kwenye Pentekoste 33 W.K. Huko, wengi walisikia habari njema katika lugha yao wenyewe, wakawa waitikadi, na kubatizwa. Inaelekea kwamba baadhi yao walipanda meli kutoka Kaisaria wakarudi na habari njema kwenye mabara ya kwao wenyewe.​—Matendo, sura 2.

Katika chumba kinachofuata, kuna kibandiko cha umbo mstatili kinachoshikilia vipande vya bamba la marimari la karne ya tatu au ya nne. Hapo awali kiliorodhesha migawanyo au safu 24 za jamaa za kikuhani kwa utaratibu ambao zilitumikia kwenye hekalu la Yerusalemu. Hekalu hilo lilikuwa limekaa magofu kwa mamia ya miaka, lakini Wayahudi walikuwa na uhakika kwamba lingejengwa baada ya muda mfupi. Karne kadhaa baadaye walikuwa bado wakisali ya kwamba Mungu angerudisha zile safu za kikuhani katika siku yao. Lakini hekalu halikujengwa upya. Yesu alikuwa ametabiri uharibifu walo. Na kabla halijaharibiwa, mtume Paulo, aliyekuwa Myahudi na Farisayo hapo kwanza, alionyesha wazi kwamba katika nafasi ya hekalu hilo Mungu alikuwa ameweka kitu bora​—hekalu kubwa zaidi, la kiroho, lililokuwa limefanyiwa kielezi tu, likatangulia kufananishwa au kuwakilishwa na jengo hilo lililofanywa kwa mikono.​—Mathayo 23:37-24:2; Waebrania, sura 8, 9.

Karne zilipita na wenye kufanya ushinde wakatokea na kutokomea. Mwishowe magofu ya Kaisaria yakadidimia chini ya mchanga na bahari. Yakiwa humo yakangojea kufukuliwa na wachimbuzi wa kisiku-hizi, ambao magunduzi yao yametusaidia kuelewa mengi zaidi juu ya maisha katika nyakati za kale na juu ya baadhi ya mambo tunayosoma katika Neno la Mungu, Biblia.

[Maelezo ya Chini]

a Wonyesho huo umekwisha kuonyeshwa kwenye Jumba la Kuhifadhi Vitu vya Makumbusho ya Historia ya Kiasili katika Washington, Jumba la Kuhifadhi Vitu vya Makumbusho ya Historia ya Kiasili la Manispaa ya Los Angeles, na Jumba la Kuhifadhi Vitu vya Makumbusho ya Historia ya Asili katika Denver, Colorado. Mahali pengine ambapo wonyesho huo umeratibiwa kuonyeshwa ni kutia ndani Jumba la Kuhifadhi Vitu vya Makumbusho ya Sayansi la Minnesota katika Saint Paul na Jumba la Kuhifadhi Vitu vya Makumbusho ya Sayansi katika Boston, na pia Jumba la Kanada la Kuhifadhi Vitu vya Makumbusho ya Mwerevuko katika Ottawa.

[Picha katika ukurasa wa 24]

Tike, mungu-mke wa Kaisaria wa “bahati njema”

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 23]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

Kwa hisani vya Jumba la Kuhifadhi Vitu vya Makumbusho ya Historia ya Kiasili la Manispaa ya Los Angeles

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 24]

Aaron Levin

Israel Department of Antiquities and Museums; photographs from Israel Museum, Jerusalem

Kwa hisani ya Jumba la Kuhifadhi Vitu vya Makumbusho ya Historia ya Kiasili la Manispaa ya Los Angeles

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki