Dini na Unazi
“Hitler . . . alimfanya Mkatoliki mmoja awe Makamu wa Chansela na kuanzia karibu siku ile ya kwanza ya utawala huo Franz von Papen akawa ndiye mvumisha habari za kuvutia vyama vya Kikatoliki vyenye mzozano ili viunge mkono Milki hiyo mpya. Katika kila sehemu ya Milki von Papen alisikiwa akihimiza waaminifu wawe na utii wa kiupofu kwa Adolf Hitler.”
“Mapema katika 1933 tangazo rasmi linalofuata lilifanywa na ushirika wa baraza la I vitendo na fikira za Kikatoliki katika Ujeremani, ulioongozwa wakati huo na [Franz] von Papen: ‘Sisi Wakatoliki Wajeremani tutasimama, kwa nafsi yetu yote na masadikisho yetu kamili, nyuma ya Adolf Hitler na Serikali yake. Sisi tunavutiwa na upendo wake kwa nchi ya baba zetu, nishati zake na hekima yake ya kimwanataifa. . . . Ukatoliki wa Ujeremani . . . ni lazima ushiriki kiutendaji katika ujenzi wa Milki ya; Tatu.’”
Franz von Papen alitumika katika kuwezesha kuwe na mkataba kati ya serikali ya; Nazi aliyotumikia katika Ujeremani na Vatikani katika Roma. Mkataba huo ulitiwa sahihi Julai 20, 1933. Tangazo rasmi la pekee lilitaarifu hivi: “Kardinali na Katibu wa ] Serikali Pacelli [ambaye baadaye akawa Papa Pius 7] leo aliweka juu ya Makamu wa Chansela von Papen, ule Msalaba Mtukufu wa Daraja la Pius . . . Makamu wa Chansela I von Papen alimpa Katibu Kardinali wa Serikali Madonna moja [sanamu ya Mariamu] iliyofanyizwa kwa madini Poseleni Nyeupe ya Meissen iwe zawadi ya Serikali ya Milki. . . . Zawadi zote zilikuwa na maelezo haya ya wakfu: ‘Kumbukumbu ya Mkataba wa Milki 1933’”—Manukuu yote yametolewa katika Franz von Papen—His Life and Times, kiliehotungwa na H. W. Blood-Ryan.