Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 5/1 kur. 16-17
  • Bashani—Chanzo Chenye Rutuba

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Bashani—Chanzo Chenye Rutuba
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka Kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 5/1 kur. 16-17

Tamasha za Kutoka Bara Lililoahidiwa

Bashani—Chanzo Chenye Rutuba

NAPOSOMA Biblia, je! hujapata kuona majina ya mahali pengi ambapo huwezi kuwazia? Katika Mei na Juni, Mashahidi wa Yehova watasoma Mika hadi Zekaria. Katika kufuata ratiba hiyo, utaona Bashani imetajwa katika maandiko matatu. (Mika 7:14; Nahumu 1:4; Zekaria 11:2) Mistari hiyo na mingine iliyo ya kupendeza itakufaidi zaidi ukiweza kuona Bashani kwa jicho la akiii yako.

Bashani ilikuwa wapi? Kwa ujumla unaweza kuitambulisha na Miinuko ya Golani, ambayo huenda ukawa umepata kuiona katika ramani za nyusipepa. Bashani ilikuwa mashariki ya Bahari ya Galilaya na pia ya Bonde la Yordani ya juu. Sana-sana lilifuliza kutoka Mto Yarmuki (sehemu ya mpaka wa sasa kati ya Yordani na Siria) upande wa kaskazini hadi Mlima Hermoni.

Kabla ya Waisraeli wa kale kuingia katika Bara la Ahadi, walilazimika kushinda jeshi la Wakanaani la jitu Ogu, mfalme wa Bashani. Baada ya hapo, sehemu kubwa ya Bashani ilikaiiwa na kabila la Manase. (Kumbukumbu 3:​1-7, 11, 13; Hesabu 32:33; 34:14) Eneo hili la Kibiblia lilikuwaje? Ingawa ilikuwa na misitu katika maeneo yalo ya milima-milima, sehemu kubwa ya Bashani ilikuwa nyanda za juu zilizo tambarare kama meza.

Katika mambo mengi Bashani lilikuwa eneo la vyakula kweli kweli. Hiyo ni kwa sababu sehemu kubwa ya jimbo hilo ilikuwa bara zuri sana la kulishia mifugo. (Yeremia 50:19) Picha za kupigwa zilizoambatanishwa zinaweza kukukumbusha marejezo fulani ya Kibiblia kuhusu Bashani.a Watu wengi wamesoma juu ya ‘mafahali wa Bashani.’ (Zaburi 22:12) Ndiyo, katika nyakati za kale jimbo hili lilijulikana sana kwa ng’ombe walo, kutia na mafahali wachanga wenye nguvu nyingi. Lakini mifugo wengine walisitawi humo pia, kama vile kondoo na mbuzi waliochangia maziwa na siagi nyingi. ​—⁠ Kumbukumbu 32:14.

Huenda ukashangaa ni kitu gani kilichoongoza kwenye rutuba nyingi hivyo katika Bashani, kwa kuwa ilikuwa mashariki ya Yordani katika eneo ambalo wengi hulifikiria kuwa kavu sana. Uhakika ni kwamba, vilima vya Galilaya upande wa magharibi ni vya kimo cha chini zaidi, kwa hiyo mawingu kutoka Mediterania yangeweza kupita juu yavyo na kuleta mvua tele Bashani. Waaidha, hewa yenye unyevunyevu na vijito vilishuka chini kutoka Mlima Hermoni. Wazia mazao ambayo yangeweza kuwapo wakati unyevunyevu huo wa thamani kubwa ulipounganika na udongo wa kivolkeno wenye rutuba nyingi uliopatikana Bashani! Eneo hilo lilizaa nafaka kwa wingi sana. Muda mrefu kabla ya kuwa ghala kuu la Waroma, Bashani iliwezesha meza za Sulemani ziwe na chakula. Basi, ni kwa sababu njema kwamba uandalizi wa Mungu kwa watu wake wakombolewa ungeweza kunenwa hivi baadaye: “Na walishe katika Bashani na Gileadi, kama siku za kale.”​—⁠Mika 7:14; 1 Wafalme 4:7, 13.

Kwa kujua juu ya uzaaji huo, unaweza kuthamini uelezaji wa Nahumu wenye kugusa sana hisia juu ya mambo ambayo kukosa upendeleo wa Mungu kungeleta: “Bashani hulegea, na Karmeli [vilima vyenye ubichi-ubichi karibu na Bahari Kuu]; hulegea nalo ua la Lebanoni.”​—⁠Nahumu l:4b.

Mandhari hiyo ya ujumla juu ya Bashani inaweza kukusaidia upige picha kwa urahisi zaidi juu ya tamasha fulani za mtazamo wa karibu-karibu zilizomo katika Biblia pia. Kwa kielelezo, inaelekea kwamba wewe umesoma juu ya kuvuna nafaka, kama vile ngano iliyokua katika sehemu kubwa ya Bashani. Mavuno ya ngano yalikuja katika miezi yenye ujoto-joto ya Iyyari na Sivani (ya kalenda ya Kiyahudi, inayolingana na mwishoni mwa Aprili, Mei, na mapema Juni). Katika kipindi hiki, Siku-kuu ya Majuma (Pentekoste) ilitukia. Yakiwa sehemu ya sikukuu hiyo, malimbuko ya mavuno ya ngano yalitolewa, na wana-kondoo, mabeberu, na fahali wakadhabihiwa. Je! ingeweza kuwa wanyama hao waliletwa kutoka Bashani?​—⁠Kutoka 34:22; Walawi 23:15-18.

Wakati wa mavuno wafanya kazi walikata ngano iliyosimama kwa mundu uliojikunja kama huu wa chuma unaoonekana juu, usio na mpini wao wa mti. (Kumbukumbu 16:​9, 10; 23:25) Ndipo mabua yalipokusanywa na kupelekwa kwenye sakafu ya kupuria, ambako kitelezeo cha ubao (kilichowekwa mawe chini) kilipitishwa juu yayo ili kuvitokeza wazi viini. (Ruthu 2:​2-7, 23; 3:​3, 6; Isaya 41:15) Unapotazama picha inayohusu jambo hili, iliyopigwa katika Miinuko ya Golani, ungeweza kuifikiria ile sheria ya Mungu yenye kujaa maana: “Ng’ombe apurapo nafaka usimfunge kinywa.”​—⁠Kumbukumbu 25:4; 1 Wakorintho 9:9.

Mwisho, kumbuka kwamba Bashani ya kale ilikuwa na maeneo yenye msitu mwingi, mingi ya miti hiyo ikiwa ni oki zilizotungamana, kama zile zilizoonyeshwa kushoto. Wafoinike walifanyiza makasia kutokana na mti imara wa oki kutoka Bashani. (Ezekieli 27:6) Na bado, hata hiyo ‘miti iliyotungamana ya Bashani, ule msitu usiopenyeka,’ haingeweza kusimama dhidi ya hasira-kisasi yenye kuonyeshwa na Mungu. (Zekaria 11:2; Isaya 2:13) Kuona miti hiyo kunafanya iwe rahisi pia kuwazia ni kwa nini misitu ya jinsi hiyo ingetatiza jeshi linalokimbia. Hata mpanda-farasi aliye peke yake angeweza kunaswa katika matawi yayo, kama ilivyotukia kwa Absalomu mahali pengine.​—⁠2 Samweli 18:​8, 9.

Tunaweza kuona kwamba hata ingawa Bashani lilikuwa jimbo la Bara Lililoahidiwa ambako si matukio mengi mno yenye umaana wa Kibiblia yalitukia, tamasha za kutoka huko zinaongezea ufahamu wetu wa Biblia.

[Maelezo ya Chini]

a Ona pia 1989 Calendar of Jehouah’s Witnesses.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 16]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 17]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est |

Kisehemu cha ndani: Taasisi ya Badè ya chimbuzi wa Vitu vya Kale vya Kibiblia

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki