Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w78 4/15 uku. 24
  • Maswali Kutoka Kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka Kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Habari Zinazolingana
  • Bashani—Chanzo Chenye Rutuba
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Kifo cha Taifa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Mambo Makuu Katika Kitabu cha Yoeli na cha Amosi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Ng’ombe Waendapo Likizo!
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
w78 4/15 uku. 24

Maswali Kutoka Kwa Wasomaji

● Ni nini maana ya unabii wa Amosi unaotajwa kuwahusu “ng’ombe wa Bashani”?

Unabii huo unapatikana katika Amosi 4:1-3 nao unasema hivi: “Lisikieni neno hili, enyi ng’ombe wa Bashani, mnaokaa juu ya mlima wa Samaria, mnaowaonea maskini, na kuwaponda wahitaji; mnaowaambia bwana zao, Haya! leteni, tunywe. Bwana [Yehova] ameapa kwa utakatifu wake, ya kuwa, tazama, siku zitawajilia, watakapowaondoa ninyi kwa kulabu, na mabaki yenu kwa ndoana. Nanyi mtatoka kwenye mahali palipobomolewa, kila mwanamke moja kwa moja mbele yake.”

Hao “ng’ombe wa Bashani” ni wanawake wa Samaria waliochochea waume wao wawapunje na kuwaonea maskini ili wao wenyewe waendelee kuishi katika anasa. Waliwaomba “bwana” zao, au waume wao, wawatafutie vitu walivyotaka ili wawe na maisha ya anasa. Lakini, Aliye Juu Zaidi hakupendelea uovu huo. Yeye ni mtakatifu na ni safi, kwa hiyo aliapa kwa utakatifu wake kwamba angechukua hatua juu ya hao “ng’ombe wa Bashani.” Wangeondolewa Samaria kwa jeuri nyingi kama kwamba wamevutwa kwa kulabu, nao mabaki wenye kuokoka wangeondolewa kama kwamba wamevutwa kwa ndoana. Adui wangewaondoa wanawake hao kwa kuwapitisha mahali palipobomolewa katika kuta za mji ulioshindwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki