Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w89 6/15 uku. 29
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Habari Zinazolingana
  • Kupanga Uzazi—Maoni ya Kikristo
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Ni Nani Anayepaswa Kuamua Ukubwa wa Familia?
    Amkeni!—1996
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
w89 6/15 uku. 29

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

◼ Je! inapatana na kanuni za Biblia kwamba mume na mke Wakristo waliofunga ndoa watumie vibonge vya kupanga uzazi?

Maandiko hayasemi wazi kwamba mume na mke Wakristo wana wajibu wa kuwa na watoto au, wakiwa na watoto, wawe na wangapi. Kila mume na mke wanapaswa kuamua kama watajaribu kuelekeza ukubwa wa jamaa yao, kwa faragha na kwa njia yenye kujali daraka lao. Wakikubali kupanga uzazi, ni juu yao binafsi kuchagua pia vizuia-mimba ambavyo watatumia. Hata hivyo, wanapaswa kufikiria​—kulingana na uelewevu wao wa Biblia na dhamiri yao​—kama kutumia njia fulani kungeonyesha staha kwa utakato wa uhai.

Biblia inaonyesha kwamba uhai wa mtu huanza wakati mimba inapotungwa; Mpaji-Uhai huona uhai ambao umetungwa, “hata kiinitete” ambacho baada ya hapo kitakua katika mji wa mimba. (Zaburi 139:16, NW; Kutoka 21:22, 23a; Yeremia 1:5) Kwa sababu hiyo, hakuna jitihada inayopasa kufanywa ili kukomesha uhai uliotungwa mimba. Kufanya hivyo kungekuwa ni kutoa mimba.

Vibonge vya kupanga uzazi hutumiwa mahali pengi kuzunguka ulimwengu. Vinazuiaje mtoto asizaliwe? Kuna namna mbili za vibonge vinavyotumiwa zaidi​—kibonge cha mchanganyiko na kibonge chenye projestini tu (kibonge kidogo). Utafiti umeelewesha wazi njia za msingi ambazo vibonge hivyo vinazuia uzazi.

Kibonge cha mchanganyiko kina hormoni za estrojeni na projestini. Kulingana na Shirika la United States la Usimamizi wa Chakula na Dawa, “njia ya msingi ya kufanya kazi” kwa kibonge cha mchanganyiko ni “kuzuia yai lisiachiliwe kutoka katika vifuko vya mayai.” Inaonekana kwamba kibonge cha namna hii kinapomezwa kwa njia yenye ukawaida mzuri, karibu nyakati zote kinazuia yai lisiachiliwe kutoka katika kifuko cha mayai. Ikiwa hakuna yai lililoachiliwa, mimba haiwezi kutungwa katika mirija Fallopia. Ingawa huenda kibonge cha namna hii kikasababisha mabadiliko katika “utando wa mji wa mimba (mabadiliko ambayo yanapunguza uelekeo wa yai kuingia humo ili lianze kukua),” hii inaonwa kuwa njia ya upili tu.

Vibonge vya mchanganyiko ulio na estrojeni ya kiasi kidogo zaidi vimefanyizwa ili kupunguza madhara yanayotokana na kuvitumia. Inaonekana kwamba vibonge hivi vya mchanganyiko ulio na estrojeni ya kiasi kidogo zaidi vinaruhusu vifuko vya mayai viwe na utendaji mwingi zaidi. Dakt. Gabriel Bialy, mkuu wa Tawi la Kufanyiza Vizuia-Mimba la Taasisi za Afya ya Kitaifa, anasema: “Uthibitisho mwingi wa ushuhuda wa kisayansi unaonyesha kwamba hata kwa kutumia kibonge chenye estrojeni ya kiasi kidogo zaidi, yai linazuiwa lisiachiliwe kutoka katika vifuko vya mayai, si kwa asilimia 100, lakini yaelekea sana kwa asilimia 95 hivi. Lakini uhakika wenyewe tu wa kwamba yai linaachiliwa litoke katika vifuko vya mayai si sawa na kusema kwamba yai hilo limetungwa mimba.”

Mwanamke akikosa kumeza kibonge cha mchanganyiko kulingana na ratiba ambayo kimepangiwa, kunakuwa na uwezekano ulioongezeka wa kwamba ile njia ya upili itasaidia kuzuia mimba. Uchunguzi uliofanywa kuhusu wanawake waliokosa vibonge viwili vyenye kiasi kidogo zaidi ulipata kwamba mayai ‘yaliponyoka’ yakatoka katika vifuko vya mayai vya asilimia 36 ya wanawake hao. Jarida Contraception linaripoti kwamba katika visa hivyo “matokeo ambayo vibonge hufanyiza katika utando wa mji wa mimba na katika ute wa shingo ya mji wa mimba huenda yakaendelea kuandaa . . . ulinzi wa kuzuia mimba.”

Namna gani kibonge cha namna ile nyingine​—kile kibonge chenye projestini tu (kibonge kidogo)? Drug Evaluations (1986) kinaripoti hivi: “Kazi kubwa hasa kuhusiana na vibonge vidogo vilivyo na projestini tu si kuzuia yai lisitoke katika kifuko. Vibonge hivi vinasababisha shingo ya mji wa mimba iwe na ute mzito ambao kwa kiasi fulani hauwezi kupenywa na mbegu ya kiume; huenda vikaongezea muda ambao yai linasafiri katika mrija na pia kusababisha mfinyano wa nafasi iliyo katika utando wa mji wa mimba [jambo ambalo lingezuia ukuzi wa yai lolote lililotungwa mimba].”

Watafiti fulani wanadai kwamba kuhusiana na kibonge chenye projestini tu, “kawaida ya kuachiliwa kwa yai kutoka katika vifuko vya mayai hutukia katika zaidi ya asilimia 40 ya wenye kukitumia.” Kwa hiyo mara nyingi kibonge hiki huruhusu yai liachiliwe kutoka katika kifuko cha mayai. Ule ute mzito uliofanyika kwenye shingo ya mji wa mimba huenda ukaziba njia ya kupita kwa mbegu ya kiume na hivyo usiruhusu mimba itungwe; ikiwa sivyo, yale mazingira mazuilifu ambayo kibonge kinafanyiza katika mji wa mimba huenda yakazuia yai lililotungwa mimba lisiingie mahali palo pa ukuzi na lisisitawi kuwa mtoto.

Basi, inaweza kufahamiwa kwamba wakati vibonge vya namna zote mbili zenye kutumiwa kwa wingi zaidi vinapotumiwa kwa ukawaida ili kupanga uzazi, inaonekana kuwa katika visa vingi huzuia yai lisitungwe mimba na kwa hiyo si vya kutoa mimba. Hata hivyo, kwa kuwa kile kibonge chenye projestini tu (kibonge kidogo) huruhusu mara nyingi zaidi yai Iiachiliwe kutoka katika vifuko vya mayai, kuna uwezekano mkubwa zaidi kwamba nyakati fulani kibonge hicho huzuia uzazi kwa kuweka kipingamizi ili uhai ambao umeanza kwa kutungwa mimba usiingie mahali pao pa ukuzi katika mji wa mimba. Uchunguzi mbalimbali wa kisayansi unaonyesha kwamba kwa kawaida (kuhusiana na mji wa mimba ambao haujaathiriwa na vibonge vya kupanga uzazi) “asilimia sitini ya mayai yaliyotungwa mimba . . . hupotezwa kabla ya kipindi cha kwanza cha kukosa mwezi.” Hata ikiwa jambo hili hutukia, hiyo ni tofauti kabisa na kuchagua kutumia njia ya kupanga uzazi inayoelekea zaidi kuzuia yai lililotungwa mimba lisiingie mahali palo pa ukuzi.

Kwa sababu hiyo, kuna maadili fulani ya wazi yanayopasa kufikiriwa ikiwa mume na mke wanazungumza na tabibu juu ya kutumia vibonge vya kupanga uzazi. Wakristo wanapaswa kutatua hata masuala ya faragha na ya kibinafsi kwa njia yenye kudumisha “dhamiri iliyo safi kikamilifu” mbele za Mungu na Mpaji-Uhai wetu.​—Matendo 23:1, NW; Wagalatia 6:5.

[Maelezo ya Chini]

a Ona Mnara wa Mlinzi wa Agosti 1, 1977, kurasa 478-80 (Kiingereza).

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki