Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 7/15 kur. 10-15
  • Kueneza Manukato ya Maarifa juu ya Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kueneza Manukato ya Maarifa juu ya Mungu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kuitia Uturi (Marashi) Njia ya
  • Manukato ya Uhai
  • Twapewa Mamlaka Kutilia Wanadamu Uturi (Marashi)
  • “Katika Msafara wa Ushindi”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Je, Wajua?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Wahudumu wa Mungu Wanathibitisha Kustahili Kwao
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1985
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2025
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 7/15 kur. 10-15

Kueneza Manukato ya Maarifa juu ya Mungu

“Asante ziwe kwa Mungu ambaye sikuzote hutuongoza katika msafara wenye shangwe ya ushindi kwa kuandamana pamoja na Kristo na kufanya harufu ya maarifa juu yake yafahamike kupitia sisi katika kila mahali!”—2 WAKORINTHO 2:14, NW.

EBU nusa, nusa! M-m-m-m! Je! wewe wayanusa manukato matamu hayo? Hapa hatumaanishi manukato ya maua yanayochanua, bali manukato ya kitamathali yanayotokana na miandiko ambayo ndiyo miteule kabisa duniani. Hii si miandiko inayotoka kwa wanadamu wa kikawaida tu bali ni koja la maua ya kitamathali lililovuviwa na Mmoja ambaye aliumba pia maua yenye harufu nzuri yaipambayo dunia. Pendeleo la kueneza manukato haya ya maarifa juu ya Mungu ni hazina kubwa. Ndiyo, ni utumishi wenye thamani kubwa sana—usiomilikiwa na watu wote, usioshirikiwa na ainabinadamu kwa ujumla.

2 Hazina hii yenye thamani ilipewa kwa wanafunzi wa Kristo walipoanzishiwa utumishi wenye utendaji kwa Yehova Mungu katika siku ya Pentekoste mwaka 33 wa Wakati wa Kawaida wetu. Wakiwa wamejawa na roho takatifu, walianza kueneza manukato ya kitamathali, wakifafanua “matendo makuu ya Mungu.” (Matendo 2:1-4, 11) Kupitia kwao manukato ya maarifa juu ya Mungu yangefikia wengine, si Wayahudi wa asili waliotahiriwa tu bali pia mataifa wasiotahiriwa, jamii za watu, na ndimi. (Matendo 10:34, 35) Wanafunzi wa kweli waliutazama utumishi huu kuwa wenye kuthaminika kuliko utajiri wote wa kimwili ambao wanadamu hurundika juu yao wenyewe.

3 Leo, ile kazi kubwa ya kueneza manukato ya maarifa juu ya Mungu inaendeshwa duniani pote—kwa kadiri kubwa kuliko iliyopata kuwako katika historia ya kibinadamu. Yahusu kuipa ushahidi ainabinadamu yote juu ya Ufalme wa Mungu uliosimamishwa chini ya Mfalme wake mwekwa, Yesu Kristo. (Mathayo 6:10; Matendo 1:8) Je! wewe wautazama utumishi wa kutangaza Mfalme na Ufalme wake kuwa hazina isiyohesabika bei? Yesu Kristo, aliyekuwa mwongozi wa mbele katika kuhubiriwa kwa habari njema za Ufalme huo, aliuthamini kwa njia hiyo, akiweka kigezo.—Mathayo 4:17; 6:19-21.

Kuitia Uturi (Marashi) Njia ya

Msafara Wenye Shangwe ya Ushindi

4 Kwa nini kutumikia Mungu ni kitu cha kuhaziniwa? Sababu moja ni kwamba hata sasa wale watumikiao Yehova wana pendeleo zuri ajabu la kuongozwa na Mungu katika msafara wenye fahari ya shangwe ya ushindi. Kulingana na New International Version, 2 Wakorintho 2:14 yasema hivi: “Asante ziwe kwa Mungu, ambaye sikuzote hutuongoza sisi katika msafara wenye shangwe ya ushindi katika Kristo na kupitia sisi huenea kila mahali yale manukato ya maarifa juu yake [“hufanya maarifa yetu juu yake yaenee kotekote katika ulimwengu kama uturi wa kupendeza!” Phillips].” Maneno hayo ya mtume Paulo yaonekana kuwa dokezo juu ya zoea fulani la kale la kuwa na misafara ya ushindi.a

5 Katika siku za jamhuri ya Kiroma, moja ya heshima kubwa kabisa ambazo Seneti ingeweza kumpa jemadari mwenye kushinda ilikuwa kumruhusu aadhimishe ushindi wake kwa kufanya msafara wa shangwe ya ushindi kwa gharama kubwa. Msafara wa Kiroma uliandamana polepole kwa kupita katika Via Triumphalis na kupanda juu kwenye ule mpando wenye kupindapinda hadi kwenye hekalu la Jupiter juu ya Kilima Capitoline. Wafalme, wana-wafalme, na majemadari waliotekwa vitani, pamoja na watoto na mahadimu wao, waliongozwa katika mwendo huo wakiwa wametiwa minyororo, mara nyingi wakiwa wamevuliwa wakawa uchi, hivyo wakishushiwa hadhi na kuaibishwa.

6 Msafara huo ulipokuwa ukipita katika jiji la Roma, umayamaya wa watu ulitupa maua mbele ya gari-vita la mshindi, na uvumba wenye kuwaka uliitia uturi (marashi) njia yote. Manukato matamu hayo yalimaanisha hali za heshima na maisha salama zaidi kwa wale askari washindi. Lakini yalimaanisha kifo kwa wale watekwa wasiosamehewa ambao wangeuawa mwishoni mwa msafara huo. Hii yatia nuru juu ya utumizi wa kiroho wa Paulo juu ya kielezi kilicho kwenye 2 Wakorintho 2:14-16. Picha ya habari hizo huonyesha Paulo na Wakristo wenzake wakiwa raia wa Mungu wenye kujitoa, “katika kuandamana na Kristo,” wote wakifuata katika msururu wa Mungu wenye ushindi na kuongozwa na Yeye katika msafara wenye fahari ya shangwe ya ushindi kwa kupita katika njia iliyotiwa uturi (marashi).

Manukato ya Uhai

au Mnuko wa Kifo

7 Kwa kueneza kotekote zile kweli za Biblia kuhusu Ufalme wa Mungu chini ya Kristo, Mashahidi wa Yehova wanaeneza, wanaonyesha, na kudhihirisha kila mahali manukato matamu ya maarifa juu ya Mungu yule mwenye neema ambaye ukweli wake umewaweka huru kutoka dini bandia. Wao hupiga miguu kwa kufuata wakiwa na shangwe ya ushindi katika utumishi wa Yehova. Matoleo yao ya utumishi wakiwa Mashahidi wake na Mfalme wake ni kama uvumba wenye kupendeza Yehova. Hivyo, sisi twaweza kuthamini jambo ambalo mtume alimaanisha aliposema: “Kwa Mungu sisi ni harufu tamu ya Kristo miongoni mwa wale wanaookolewa na miongoni mwa wale wanaoangamia; kwa hawa wa mwisho ni harufu inayotoka kwenye kifo hadi kifo, kwa wale wa kwanza ni harufu inayotoka kwenye uhai hadi uhai [“manukato ya kuhuisha ambayo huleta uhai,” The New English Bible; “manukato yanayoburudisha ya uhai wenyewe,” Phillips].”—2 Wakorintho 2:15, 16, NW.

8 Watu wafuataji haki walio na mwelekeo wa kikondoo huhisi ule utamu wa maarifa juu ya Yehova kama yaenezwavyo na Mashahidi wake. Kwa watu wa jinsi hiyo kazi ya ushahidi ina mnukio wa afya na uhai, wa ukweli ulio hai, wenye kutia uhai. Wao huwatolea asante Yehova na Mfalme wake, na hujiunga katika msafara wao wenye shangwe ya ushindi, na kupaaza sauti hivi: “Wokovu wetu ni kwa Mungu wetu, ambaye ameketi juu ya kiti cha ufalme, na kwa Mwana-Kondoo.” (Ufunuo 7:10, NW) Wao hupumua halihewa ya ukweli wa Ufalme, ambayo ni manukato ya uhai yanayoburudisha ambayo huongoza kwenye uhai. Lakini Shetani na roho waovu wake wamepotosha nguvu za kunusa za wale wanaojibakiza kwenye dini bandia, hivi kwamba wao hushika pua zao eti kuna harufu mbaya na kuukataa ukweli kimadharau. Kwa “wale wanaoangamia,” ukweli na wenye kuuchukua kwa uaminifu hueneza harufu ya kifo iongozayo kwenye kifo. Au kama vile New International Version iwekavyo wazo hilo: “Kwa mmoja sisi ni mnuko wa kifo.” Tafsiri ya Phillips hufasiri hivi: “Kwa hawa wa mwisho waonekana kama mnuko wa kifo wenye kuleta maangamizi.”

9 “Naye ni nani astahiliye kadiri ya kutosha kwa mambo haya?” ndipo mtume auliza. (2 Wakorintho 2:16, NW) Hiyo ni kusema, “naye ni nani awezaye kustahili kwa kazi kama hii?” (The Jerusalem Bible) “Naye ni nani aliye hodari kwa utumishi wa jinsi hii?” (Weymouth) Jibu la Kimaandiko ni hili: Mashahidi wa Yehova! Kwa nini? Kwa sababu watu waliojiweka wakfu walio wafuataji haki, wenye moyo mweupe, na wasiotafuta pato la ubinafsi na ambao hunena ukweli, waziwazi na bila kuridhiana na dini bandia, ndio peke yao wastahilio kwa kazi hii ya kueneza manukato ya maarifa juu ya Mungu.—Wakolosai 1:3-6, 13; 2 Timotheo 2:15.

10 Makasisi wa Jumuiya ya Wakristo, watafutao msimamo mwema pamoja na ulimwengu huu, hushindwa kustahili na kuwa hodari kwa utumishi huu usio na ubinafsi. Kwa nini? Kwa sababu wao hushindwa kutimiza takwa lililoonyeshwa na taarifa ya Paulo: “Sisi si kama wengine ambao hufanya biashara na ujumbe wa Mungu; sisi tunahubiri kwa unyofu mbele ya Mungu, kama watu tuliotumwa na Mungu, tukiwa tumeungana na Kristo.” (2 Wakorintho 2:17, HNWW) Au kama vile New International Version iwekavyo wazo hilo: “Tofauti na wengi sana, sisi hatuchuuzi neno la Mungu kwa ajili ya faida. Kinyume cha hivyo, katika Kristo sisi twanena mbele za Mungu kwa weupe wa moyo, kama watu waliotumwa kutoka kwa Mungu.”

11 Mashahidi wa Yehova hutumwa kutoka kwa Mungu, nao wanafanya kazi yao ya kutoa ushahidi wakiwa chini ya mwono wa Mungu. Ingawa wao huwaandalia watu wenye kupendezwa vitabu vyenye kuthaminika na vichapo vingine ambavyo hueleza Neno la Mungu nao hukubali misaada ya kujitolea kwa hiari kwa ajili ya kazi ya kuhubiri Ufalme ulimwenguni pote, zoea hilo si kuchuuza wala kutohoa (kupunguza thamani ya) Neno la Mungu. Kwa uhakika, misaada hiyo ni usaidizi tu wa kuelekea kueneza maarifa juu ya Mungu kwa wengine zaidi.

12 Watu wengi sana leo, kwa kujua au kwa kutojua, wamenunua namna ya Ukristo uliotoholewa, kwa kuwa huzifaa tamaa zao za ubinafsi na haizuilii mtindo-maisha wao. Wao huamini kwamba Mungu huwakubali kwa sababu ya dai lao kwamba wanampenda yeye mioyoni mwao. Hata hivyo, ionyeshwapo kwamba Neno la Mungu lahitilafiana na imani zao na mwenendo, wao hupinda Maandiko ili wakweze maoni ya kibinafsi juu ya uelewevu ufaao wa Kibiblia. (Mathayo 15:8, 9; 2 Petro 3:16) Lakini Mashahidi wa Yehova hutokeza katika Biblia ukweli ulio safi sana, usiotoholewa, hivyo wakitokeza manukato matamu yenye kukubalika kwa Mungu na kwa waabudu wake wa kweli. Hapo wao husukuma mbali mapokeo yote ya kidini na vipingamizi vyenye kuzuia kupata maarifa ya kweli juu ya Mungu.

13 Kwa kweli, kuwa katika msafara wa Mungu wenye shangwe ya ushindi kwa kuandamana pamoja na Kristo ni pendeleo lisilo na kifani lenye kuonewa shangwe si na Wakristo wapakwa-mafuta peke yao bali pia na “umati mkubwa” wa “kondoo wengine” hata sasa, kwa maana shangwe ya ushindi wa Ufalme iko karibu. (Ufunuo 7:4, 9; Yohana 10:16) Tutazamiapo visa zaidi vya shangwe za ushindi za Mfalme wetu mwenye kushinda, kila tuendako twayaeneza maarifa juu ya Mungu yatiayo uhai yakiwa kama uturi (marashi), au uvumba wenye thamani, kwa wale ambao mioyo yao yatamani sana ukweli na uadilifu. Ni pendeleo kama nini kwa wale wastahilio kwa kazi hii iliyo nzuri ajabu!—Yohana 17:3; Wakolosai 3:16, 17.

Twapewa Mamlaka Kutilia Wanadamu Uturi (Marashi)

14 Lakini je! wale waenezao uturi (marashi) wa maarifa juu ya Mungu na juu ya Ufalme wake wana uhitaji wa shahada au cheti cha mamlaka kutoka kwa wanadamu? Sivyo! Tayari sisi tumepewa utume, au tumewekwa rasmi, tukiwa Mashahidi kwa ajili ya Aliye Mkuu Kabisa katika ulimwengu wote mzima. Hivyo, hatuhitaji kusita-sita kwenda shambani kueneza manukato ya habari njema za Ufalme wa Mungu. Kumbuka kwamba Yehova hutuongoza. Huduma ya Yesu ilitekelezwa kwa kukabiliana na “maongezi ya kinyume ya watenda dhambi.” (Waebrania 12:3, NW) Hata hivyo, kumbukumbu la matendo ya Yesu ya utendaji wa shambani, kama lipatikanavyo katika Biblia, lingali la kweli, na kazi yake shambani humpongeza yeye na kuunga mkono kwamba yeye ni mhudumu wa kweli wa Yehova Mungu.

15 Mtume Paulo alikabili hali kama hiyo yenye kutatiza katika siku yake kwa kutoa hoja hii: “Je! sisi tunaanza tena kujipendekeza wenyewe? Au labda sisi, kama watu fulani, twahitaji barua za pendekezo kwenu au kutoka kwenu? Nyinyi wenyewe ndio barua yetu, iliyoandikwa juu ya mioyo yetu na kujulikana na yenye kusomwa na ainabinadamu yote. Kwa maana nyinyi mwaonyeshwa kuwa barua ya Kristo iliyoandikwa na sisi tukiwa wahudumu, iliyoandikwa si kwa wino bali kwa roho ya Mungu aliye hai, si juu ya mabamba ya mawe, bali juu ya mabamba ya kimnofu, juu ya mioyo.”—2 Wakorintho 3:1-3, NW.

16 Wenye mamlaka wa kilimwengu hawakiri utume wetu sisi Mashahidi wa Yehova. Lakini acheni kazi yetu ya kueneza manukato ya maarifa juu ya Yehova ijisemee yenyewe! Kazi hii haiwezi kufutwa, ingawa watu fulani hukataa kusoma ushuhuda huu wenye kuthibitisha huduma yetu. Makasisi huonyesha vyeti vyao vilivyotoka kwenye mashirika ya utawala wa kikasisi. Lakini, hivyo ni vijikaratasi tu, neno la binadamu. Zaidi ya kunukuu mambo ya kuwaunga mkono kutokana na Neno la Mungu, Mashahidi wa Yehova ni vyeti vya ushuhuda vya mnofu na damu. Umati mkubwa wa kondoo wengine ambao wamefikiwa kwa zile habari njema za Ufalme wamekusanywa pia kwenye upande wa kulia wa Mfalme wa Yehova. (Mathayo 25:33, 34) Wote hawa ni barua yetu ya pendekezo, barua ambayo sisi tukiwa Mashahidi wa Yehova huenda nayo kila mahali ikiwa katika mioyo na akili zetu nasi twaweza kuionyesha tukiwa na uhakika. Wale wasimamao upande wa enzi kuu ya Mungu ya ulimwengu wote mzima na kushiriki katika kutumikia Mungu kwa kuandamana na Mashahidi wa Yehova, wao wenyewe ni hati ya pendekezo isiyoweza kukosa kusomwa na kujulikana na watu wote.

17 Bila shaka, hiyo hufanya wanadini bandia wakasirike na kuona husuda. Hata hivyo, umati mkubwa unaoongezeka wa kondoo wengine ni barua ya pendekezo kutoka kwa Yesu Kristo, yule Mchungaji Mwema, anayetumia Mashahidi wa Yehova wote katika kazi yake ya uchungaji. Sisi ndio kalamu, au chombo cha kibinadamu, ambacho yeye hutumia kuandika barua hii. Barua yenyewe haiandikwi kwa wino iwezayo kufutwa, bali imeandikwa na, tena kwa, kani ya utendaji au roho ya Mungu, ambayo yafanya kazi ndani yetu. Haiko kama katika kisa cha Musa wakati sheria ya zile Amri Kumi ilipoandikwa juu ya mabamba mawili ya mawe. Barua yetu imeandikwa juu ya mabamba ya kimnofu ya mioyo ya kibinadamu, kwa kuwa huduma yetu ya kiroho hutokeza badiliko la akili na moyo katika wapokezi wa zile habari njema zenye manukato.

18 Kazi yetu ya kutumia Neno la Mungu imevutia wapokezi wenye kuzithamini habari njema na imetokeza mabadiliko mazuri ajabu. Uamuzi wao kutumikia Mungu umethibitika kuwa si msimamo wa kushtukia tu kwa sababu ya mpwito-mpwito wenye kuchochewa ndani yao na mwevanjeli mwenye sisimuko la hisia-moyo. Bali, huo ni mbadiliko wa daima wa maisha zao kwa kutegemea kweli za Biblia Takatifu zenye kueleweka wazi kabisa. Kupenda Mungu wa kweli, Yehova, huwasukuma ‘wavue utu wa kale pamoja na tamaa zao za udanganyifu na kuvaa utu mpya,’ ambao huonyesha “tunda la roho.” (Waefeso 4:20-24; Wagalatia 5:22, 23, NW) Kwa hiyo, tokeo huwa ni kuwafanya barua ya pendekezo. Hiyo husema wazi kuliko barua yoyote yenye kuandikwa kwa mkono na sisi au na tengenezo lolote lionekanalo ambalo lingeweza kututuma.

19 Kwenye 2 Wakorintho 3:4-6, NW, Paulo aendelea kusema hivi: “Sasa kupitia Kristo sisi tuna uhakika wa namna hii kuelekea Mungu. Si kwamba sisi wenyewe tunastahili kadiri ya kutosha kuhesabu kitu chochote kuwa kinatoka kwa sisi wenyewe, bali kustahili kwetu kadiri ya kutosha hutoka kwa Mungu, ambaye kwa kweli ametustahilisha kadiri ya kutosha ili tuwe wahudumu wa agano jipya.” Ingawa wale tu wa mabaki wapakwa-mafuta ndio “wahudumu wa agano jipya,” kazi yao imekuwa na matokeo juu ya umati mkubwa wa kondoo wengine, na bado itaathi-ri hesabu zisizohesabika za kondoo wengine ambao wangali watakusanywa. Huo ndio uhakika ambao Mashahidi wa Yehova wote wanao kupitia Kristo Yesu kuelekea Yehova Mungu. Kwa shukrani mabaki huutia moyo umati mkubwa wa kondoo wengine washiriki kwa moyo wote katika ile huduma ‘ya kuandika barua’ ambayo Yesu Kristo alitabiri kwenye Mathayo 24:14 na Mathayo 28:19, 20.

20 Hivyo ndivyo wamefanya, kama ionekanavyo wazi kutokana na ripoti ya Kitabu-Mwaka 1990 (cha Kiingereza) ambamo Mashahidi wa Yehova waonyeshwa wakieneza manukato ya maarifa juu ya Mungu katika nchi 212. Hesabu yao ni wahubiri watendaji zaidi ya 3,787,000, na mwaka jana tu waliingiza saa karibu 835,000,000 katika kuhubiri habari njema hizi za Ufalme. Kwenye Mlo wa Jioni wa Bwana mwaka jana, watu 9,479,064 walihudhuria. Mabaki wapakwa-mafuta na pia washiriki wa umati mkubwa wa kondoo wengine waweza kusema hivi: “Kustahili kwetu kadiri ya kutosha hutoka kwa Mungu.” Au kama vile The Jerusalem Bible ipangavyo maneno hayo: “Sifa zote za ustahili wetu huja kutoka kwa Mungu.”

21 Kwa hiyo, yaeneze kila mahali manukato matamu yenye kutia uhai ya maarifa juu ya Mungu! Ifanye halihewa ya eneo la kundi lenu ikolee manukato ya maarifa juu ya Yehova. Halafu, yeye akiwa Jemadari wa kitheokrasi mwenye shangwe ya ushindi, atakuongoza wewe katika msafara wake wenye ushindi huku Mashahidi wake wote wakisonga mbele katika hii huduma ya utukufu ya ki-siku-hizi!

[Maelezo ya Chini]

a Kwa habari zaidi, ona Insight on the Scriptures, Buku 2, kurasa 1128-9, kilichotangazwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

Wewe Ungejibuje

◻ Paulo atumia kielezi gani kwenye 2 Wakorintho 2:14-16?

◻ Kueneza manukato ya maarifa juu ya Mungu kuna tokeo gani juu ya wengine?

◻ Ni nani peke yao wastahilio kwa kazi hii, na kwa nini?

◻ Kwa nini wenye kutilia wanadamu uturi (marashi) hawahitaji barua za pendekezo la mwandiko wa mkono kwa kazi yao?

[Maswali ya Funzo]

 1. Hapa tunazungumzia manukato gani, na pendeleo la kuyaeneza lapasa kuonwaje?

 2. Ni lini wanafunzi wa Kristo walipoanza kueneza manukato ya kitamathali, na tokeo likiwa nini?

 3. Kazi ya kueneza manukato ya maarifa juu ya Mungu inaendeshwa kwa kadiri gani, na ni swali gani ambalo twahitaji kujiuliza wenyewe?

 4. Kulingana na 2 Wakorintho 2:14, sasa Mungu anawaongozaje watumishi wake duniani, na maneno ya Paulo yana dokezo juu ya zoea gani la kale?

 5, 6. (a) Ni jambo gani lililotukia wakati wa misafara ya Kiroma yenye shangwe ya ushindi, na yale manukato matamu yalimaanisha nini kwa watu mbalimbali? (b) Ni nini utumizi wa kiroho wa kielezi kilicho kwenye 2 Wakorintho 2:14-16?

 7, 8. (a) Mashahidi wa Yehova wanaenezaje yale manukato matamu ya maarifa juu ya Mungu? (b) Wakati Mashahidi waenezapo yale manukato ya kitamathali, ni nini itikio la wale wanaookolewa? (c) Itikio ni nini kutoka kwa wale wanaoangamia?

 9. Ni swali gani ambalo Paulo auliza sasa, nawe ungejibuje, na kwa nini?

 10. Kwa nini makasisi hawastahili kwa kazi ya kueneza manukato ya maarifa juu ya Mungu?

 11, 12. (a) Kwa nini Mashahidi si “wachuuzi wa neno la Mungu” kwa sababu ya kukubali misaada ya hiari? (b) Kinyume cha ile namna ya Ukristo uliotoholewa ambao hununuliwa na wengi, Mashahidi wa Yehova hutokeza nini?

 13. Ni nani, zaidi ya Wakristo wapakwa-mafuta, walio katika msafara wa Mungu wenye shangwe ya ushindi, nao wanafanya nini kila waendako?

 14. Kwa nini wale waenezao manukato ya maarifa juu ya Mungu hawahitaji cheti cha mamlaka kutoka kwa wanadamu?

 15. Mtume Paulo alionyeshaje kwamba Wakristo wa kweli hawahitaji “barua za pendekezo”?

 16. Ni barua ya aina gani ambayo Mashahidi wa Yehova hutokeza kama ushuhuda wa kuthibitisha kwamba huduma yao imetoka kwa Mungu?

 17. “Barua [yetu] ya Kristo” huandikwaje, na kwa nini Paulo asema kwamba imeandikwa juu ya mioyo?

 18. Ni tokeo gani hufanya wapokezi wa habari njema wawe barua ya pendekezo?

 19. Paulo aelezaje sifa za ustahili wa “wahudumu wa agano jipya,” na kazi yao imekuwa na tokeo gani juu ya ule umati mkubwa?

 20. (a) Ripoti ya Kitabu-Mwaka yaonyesha nini juu ya wale wanaoeneza manukato ya maarifa juu ya Mungu? (b) Sisi sote twaweza kusema nini juu ya sifa zetu za kustahili kuifanya huduma ya kuandika barua?

 21. Sisi sote twapaswa kuwa tunafanya nini, na kwa nini?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki