Mandhari Kutoka Bara Lililoahidiwa
Je! Wewe Utajifunza Kutokana na Majira?
YEHOVA alisema hivi wakati mmoja: ‘Muda nchi idumupo, majira ya kupanda, na mavuno, wakati wa baridi na wakati wa hari, havitakoma.’ (Mwanzo 8:22) Hivyo aliyakazia majira ya ukulima.
Wewe wajua nini juu ya majira na kuhusiana kwayo na ukulima? Hata ikiwa wewe waishi katika jiji au hufanyi ukulima wowote, yakupasa ujifunze juu ya majira ya Israeli na utendaji mbalimbali wa ukulima. Kwa nini? Kwa sababu kadiri ujuavyo mengi zaidi juu ya hayo, ndivyo utakavyoelewa zaidi Neno la Mungu.
Wakulima hulima ardhi kwa plau, hupanda mbegu, halafu huvuna na kupura nafaka zao. Lakini ili kushika ufahamu wa wazi zaidi wa mambo yasemwayo na Biblia, twapaswa kujua mengi zaidi, kutia na wakati utendaji huo ulitukia. Chukua kwa kielelezo kulima kwa plau, kama kule ambako twaona kukifanywa juu katika ardhi yenye matungazi katika ile iliyokuwa Yudea ya kale.a Wewe wafikiri picha hii ilipigwa katika mwezi gani? Kujua ni wakati gani kulima kwa plau hufanywa katika nchi yenu huenda kukafanya ukosee. Wakati wa kulima kwa plau sio ule ule katika Kizio cha Kaskazini kama ulivyo katika Kizio cha Kusini; hutofautiana pia kwenye miinuko mbalimbali kutoka usawa wa bahari na kulingana na wakati wa majira ya mvua.
Jambo hilo lingeweza kuathiri maoni yako juu ya matukio ya Biblia. Ungeweza kusoma hivi juu ya jinsi Eliya alivyomweka rasmi mrithi wake: “Akamkuta Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akilima [kwa plau, NW], mwenye jozi za ng’ombe kumi na mbili mbele yake.” (1 Wafalme 19:19) Wewe wafikiri hilo lilitukia katika mwezi gani, na nchi ingeonekanaje? Na kwenye Yohana 4:35, Yesu alisema: “Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? . . . Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.” Ingawa alitaja wakati fulani hususa, je! wewe waelewa ni lini?
Chati yaandaa muhtasari bora kabisa wa majira na utendaji wa ukulima katika Bara Lililoahidiwa. Ule mviringo wa nje waonyesha miezi ya kalenda takatifu ya Kiyahudi.b Kwa kuilinganisha na miezi yetu, waona kule kuingiana, kama vile kuingiana kwa Nisani (au, Abibu) na mwisho wa Machi na mwanzo wa Aprili. Kisehemu kifuatacho kuelekea katikati chaonyesha wakati mavuno yalipoiva, jambo ambalo lakusaidia ung’amue wakati utendaji fulani wa ukulima, kama mavuno na kupura nafaka, ulipotukia. Kitovu cha chati chakuacha wewe ulinganishe mabadiliko ya halihewa mwakani.
Itumie chati kuongeza kina cha uelewevu na uthamini wako juu ya masimulizi ya Kibiblia, kama vile vielelezo viwili ambavyo tayari vimetajwa.
Elisha alikuwa akishiriki katika shughuli kubwa ya kulima kwa plau alipoitwa awe nabii. Hiyo yaelekea kuweka wakati huo katika Tishri (Septemba-Oktoba), wakati ambapo joto kali mno la kiangazi lilikuwa limekwisha. Mvua za mapema zilikuwa zimeanza kulainisha udongo, zikiwezesha ulimaji wa plau, kufuatwa na upandaji.
Na ni lini Yesu alipoyasema maneno kwenye Yohana 4:35? Ilikuwa imebaki miezi minne ndipo mavuno yafike. Angalia kwamba mavuno ya shayiri yalianza katika Nisani (Machi-Aprili), kari-bu na wakati wa Kupitwa. Hesabu miezi minne kurudi nyuma. Hiyo yakuleta kwenye Kislevu (Novemba-Desemba). Mvua zilikuwa zikiongezeka, huko mbele kukiwa na ongezeko la mvua zaidi na halihewa yenye baridi zaidi. Kwa hiyo ni wazi kwamba Yesu alimaanisha mavuno ya kitamathali aliposema: “Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno.”
Yanayofuata ni maswali mengine kwa funzo lako la kibinafsi au kwa utumizi katika kipindi cha kupendeza cha kujifunza pamoja na familia yako:
◼ Mavuno ya kitani kuzunguka Yeriko yalikuwa katika mwezi wa Adari; kwa sababu hiyo, maelezo kwenye Yoshua 2:6 na 3:15 yathibitishaje usahihi wa Biblia?—Yoshua 4:19; 5:11.
◼ Kupura kulifuata mavuno ya nafaka, kwa hiyo ahadi iliyo kwenye Walawi 26:5 yaonyeshaje ufanisi mwingi?
◼ Ni jinsi gani 2 Samweli 21:10 yadokeza kwamba huenda Rispa akawa alikesha kwa muda mrefu juu ya wanaye wawili, walioruhusiwa kuchinjwa ili kuondoa hatia ya damu kwa watu wa Mungu?
◼ Kwa nini zile ngurumo na ile mvua itajwayo kwenye 1 Samweli 12:17 zachukuliwa kuwa itikio la kimungu?—Mithali 26:1.
◼ Ruthu alikuwa na sababu gani ya kukata shauri kwamba jinsi alivyotendewa na Boazi haikuwa itikio la muda tu?—Ruthu 1:22; 2:23.
Kwa nini usiiweke chati hii karibu wakati unapofanya usomaji wa Biblia?
KISLEVU
14, 15, Purimu
NISANI
14 Kupitwa
15-21 Keki (Mikate, UV)
Isiyochachwa ya
matunda ya kwanza
IYYARI
14 Kupitwa ya Kuchelewa,
SIVANI
6 Sikukuu ya Majuma,
(Pentekoste)
TISHRI
1 Mpulizo wa tarumbeta
10 Siku ya Upatanisho
15-21 Sikukuu ya Vibanda
22 Kusanyiko la Mambo Mazito
[Maelezo ya Chini]
a Ona pia 1990 Calendar of Jehovah’s Witnesses.
b Mwezi wa ziada (Veadari), au wenye kuongezewa katika kalenda, uliongezwa mara saba katika mrudio wa kila miaka 19.
[Mchoro/Picha katika ukurasa wa 17]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
NISANI
Machi-Aprili
Shayiri
IYYARI
Aprili-Mei
Ngano
SIVANI
Mei-Juni
Tini za Mapema
TAMMUZI
Juni-Julai
Zabibu za Kwanza
ABU
Julai-Agosti
Matunda ya Kiangazi
ELULI
Agosti-Septemba
Tende, Zabibu, Tini
TISHRI
Septemba-Oktoba
Kulima kwa Plau
HESHVAN
Oktoba-Novemba
Zeituni
KISLEVU
Novemba-Desemba
Makundi ya Kondoo Yafungiwa Wakati wa Kipupwe
TEBETHI
Desemba-Januari
Majani Yanasitawi
SHEBATI
Januari-Febuari
Michipuko ya Malozi
ADARI
Februari-Machi
Machungwa-balungi
VEADARI
Machi
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 16]
Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.
[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 17]
Garo Nalbandian
Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.