Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w90 9/15 uku. 23
  • Mwenendo Ambao Hupamba Fundisho la Mungu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwenendo Ambao Hupamba Fundisho la Mungu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Kundi la Kikristo na Utendaji Wake
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Kutaniko na Lijengwe
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
  • Kutimiza Huduma Yetu ya Ufalme Katika Kundi
    Huduma Yetu ya Ufalme—1991
  • Uwe Mnyoofu Katika Mambo Yote
    “Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1990
w90 9/15 uku. 23

Mwenendo Ambao Hupamba Fundisho la Mungu

Hivi majuzi, usimamizi wa kampuni moja katika Caracas, Venezuela, ulielekeza barua kwa wazee na watumishi wa huduma wa kundi la hapo karibu la Mashahidi wa Yehova. Waliandika hivi humo ndani: “Sisi tumepokea maelekezo mazuri sana juu ya watu walio katika dini yenu kuhusu kujali kwao madaraka na kufuata haki. Ndiyo sababu sasa twawafikia nyinyi. Kwa sababu kwa sasa hatuna wafanya kazi, twahitaji hima watu wawili wa kujaza vyeo vinavyofuata: mmoja awe dereva na yule mwingine awe meneja wa bohari. Tungethamini sana habari zozote ambazo mngeweza kuandaa kuhusu mtu fulani katika kundi lenu au katika moja la hapo karibu. Kwa kweli sisi hatutamani kuajiri wafanya kazi wasio Mashahidi. Tafadhali, tujulisheni hata ikiwa hakuna mtu anayepatikana, kwa kuwa tutangoja jibu lenu kabla ya kufanya uamuzi wowote.”

Baada ya kupata barua hiyo chini ya mlango wa Jumba la Ufalme, mmoja wa wazee wa kundi alizuru mwenye kampuni hiyo. Mwenyewe huyo alikuwa ameshughulika na Mashahidi wa Yehova kwa miaka 15 na akakumbuka hakupata matatizo yoyote mazito akiwa na waajiri wake Mashahidi. Aliwarejezea wao kuwa wafanya kazi wenye kuchukua mambo kwa uzito, wenye kujali madaraka, wafuataji haki, na wenye bidii ya uendelevu. Halafu akaongezea hivi: “Mimi najua kwamba nyinyi hamvumilii watenda maovu, nanyi huwatenga na ushirika. Hiyo huonyesha kwamba kundi lenu halitaki kushirikiana na watu wa jinsi hiyo.”

Mwenendo wa jinsi hiyo hupamba fundisho la Mungu. (Tito 2:10) Nao ni tokeo la tamaa halisi ya kushika kwa ukaribu kanuni za maadili zilizopangiliwa katika Biblia.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki