Je! Wewe Una Hamu Sana Kuuona Wakati Ambapo . . .
◻ wewe waweza kuhisi salama salimini katika nyumba yako—hata uwe ni wakati gani wa siku?
◻ hakutakuwa na uhitaji wa kufuli, makomeo, ving’ora, vitundu vya kuchungulia mlangoni, nyua za kuzungukia nyumba, walinzi, mbwa walinzi, na vilinda-usalama vinginevyo?
◻ waweza kutembea barabarani ukiwa peke yako katika usalama kamili, hata usiku?
◻ dawa za kulevya zenye kudhuru na matatizo yote yenye kuhusiana nazo yatakuwa kumbukumbu la zamani za kale?
◻ vita vyote vitakuwa vimekoma, na silaha zisifanyizwe wala zisirundikwe?
◻ hutalazimika tena kuwa na wasiwasi juu ya chakula, hewa na maji yaliyochafuzwa?
◻ ugaidi, kutekwa kwa watu nyara, na vitisho vya makombora vitaondolewa kabisa?
◻ mali za asili za dunia zitalindwa, zidumishwe, na kutumiwa kwa hekima kwa manufaa ya wote?
◻ pupa na ubinafsi hazitakuwa tena kani zenye kusukuma ainabinadamu?
◻ watoto watakapodumisha hali yao isiyo na hatia na kuwa wastahifu kwa wengine na mali zao?
◻ wanawake hawataonewa na kuchukuliwa kama wahanga wa kutendwa yasiyofaa?
◻ sheria na virekebi vitakapokuwa vya haki na kutekelezwa kwa haki kwa manufaa ya wote?
◻ serikali itakafanya maamuzi kwa msingi wa mahitaji halisi wala si kwa msingi wa siasa?
◻ uhuru na usawa hautakuwa ukihubiriwa tu bali pia ukizoewa?
◻ umaskini hautakuwako tena, bali wote watakuwa na vyote vyenye kuhitajiwa kwa afya, hali njema, na furaha yao?
◻ watoto watatakiwa na kutunzwa na wasitumiwe tena vibaya wala kuachwa peke yao?
◻ magonjwa na kifo vitakuwa vimewezwa kabisa, na kusiwe na tauni za kutisha?
◻ kila mtu ukutanaye naye atakuwa mwenye fadhili, mwenye kusaidia, na mwenye kutumainika?
◻ uhai wa kila mtu utathaminiwa kikweli, na wote waweze kupata furaha ya kudumu?
◻ dini haitakuwa tena kani ya migawanyiko, yenye kuongoza kwenye ushupavu, chuki, na vita?
◻ wote watakuwa na makao ya kutosha yenye kupendeza, na ukosefu wa nyumba uwe jambo la zamani?
Ikiwa waweza kusema ndiyo kwa lolote la hayo yaliyo juu, utapendezwa kusoma makala zifuatazo.