Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 2/15 uku. 23
  • Upendo wa Kidugu Ni Wenye Kutenda

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Upendo wa Kidugu Ni Wenye Kutenda
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kusifiwa kwa Ajili ya Upendo na Imani
  • Kitabu cha Biblia Namba 57—Filemoni
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • ‘Kuhimiza kwa Msingi wa Upendo’
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Filemoni—Ushuhuda wa Ukristo Wenye Matendo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1984
  • Filemoni na Onesimo—Wenye Kuungana Katika Udugu wa Kikristo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 2/15 uku. 23

Upendo wa Kidugu Ni Wenye Kutenda

Mambo Makuu Kutoka Filemoni

YESU KRISTO aliwapa wafuasi wake “amri mpya” kwamba wapendane wao kwa wao jinsi alivyowapenda. (Yohana 13:34, 35) Kwa sababu ya upendo huo, hata wangekufa mmoja kwa ajili ya mwingine. Ndiyo, upendo wa kidugu ni imara na wenye kutenda hivyo.

Mtume Paulo alikuwa na hakika kwamba upendo wa kidugu ungemchochea Filemoni, Mkristo aliyeshiriki na kundi katika Kolosai, jiji lililo katika Esia Ndogo. Upendo ulikuwa tayari umempa moyo Filemoni afungue nyumba yake ili itumiwe kama mahali pa kukutana pa Kikristo. Onesimo mtumwa wa Filemoni alikuwa ametoroka, labda akiwa ameiba fedha ili alipie safari yake ya baharini kwenda Roma, ambapo alikutana na Paulo baadaye na kuukubali Ukristo.

Alipokuwa amefungwa gerezani huko Roma 60-61 W.K. hivi, Paulo aliandika barua iliyoelekezwa hasa kwa Filemoni. Ilimsihi Filemoni ampokee kwa roho ya upendo wa kidugu Onesimo aliyekuwa anarudi. Soma barua hii, na utaona ni mfano mzuri wa shauku na busara—mmoja unaoweza kuigwa vizuri na watu wa Yehova.

Kusifiwa kwa Ajili ya Upendo na Imani

Akisema na Filemoni na wengine, kwanza Paulo alitoa sifa. (Mistari 1-7) Mtume aliendelea kusikia juu ya upendo ambao Filemoni alikuwa nao kwa ajili ya Kristo na watakatifu wote na juu ya imani yake. Hiyo ilimsukuma Paulo kumshukuru Yehova na ilimletea shangwe na faraja nyingi. Je! sisi binafsi husifu waamini wenzetu ambao ni mfano katika upendo na imani? Tunapaswa kufanya hivyo.

Himizo lenye msingi wa upendo linatakiwa sikuzote katika kushughulika na Wakristo wenzi, kama maneno ya Paulo yanavyoonyesha. (Mistari 8-14) Baada ya mfikio wake wenye busara mtume alisema kwamba ingawa yeye angeweza kumwagiza Filemoni ‘limpasalo,’ badala yake alichagua kumhimiza. Kufanya nini? Kumpokea mtumwa Onesimo kwa njia ya fadhili! Paulo angalipenda kudumisha huduma zenye mafaa za Onesimo lakini hangeweza kufanya hivyo bila idhini ya Filemoni.

Matokeo yanayoonekana kutokuwa mema mara nyingi huthibitika kuwa yenye manufaa, kama vile Paulo aonyesha baada ya hapo. (Mistari 15-21) Kwa kweli, mema yalikuwa yametokea wakati Onesimo alikuwa ametoroka. Kwa nini? Kwa sababu Filemoni angeweza kumpata tena akiwa ndugu Mkristo aliye na nia na mnyofu, si kama mtumwa asiye na nia, na yawezekana asiye mnyofu. Paulo alimwomba Filemoni amkaribishe Onesimo tena kama vile Paulo angekaribishwa. Ikiwa Onesimo alikuwa amemkosea Filemoni kwa njia yoyote, mtume angefanya malipo. Kumfanya Filemoni awe na nia ya kukubali hata zaidi, Paulo alimkumbusha kwamba yeye mwenyewe aliwiwa na mtume kwa ajili ya kuwa Mkristo. Hivyo, Paulo alikuwa na hakika kwamba Filemoni angefanya hata zaidi ya yale aliyoombwa afanye. Ni sihi yenye busara na upendo kama nini! Kwa hakika, hiyo ndiyo njia tunayopaswa kushughulika na Wakristo wenzi.

Paulo alimalizia barua yake kwa tumaini, salamu, na kuwatakia mema. (Mistari 22-25) Alitumaini kwamba kupitia sala za wengine kwa ajili yake, angefunguliwa karibuni. (Kama barua ya pili ya Paulo kwa Timotheo inavyoonyesha, sala zile zilijibiwa.) Akimaliza barua yake, Paulo alipeleka salamu na kuonyesha tamaa kwamba fadhili zisizostahiliwa za Yesu Kristo zingeweza kuwa na roho iliyoonyeshwa na Filemoni na waabudu wenzake wa Yehova.

[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 23]

Zaidi ya Mtumwa: Kuhusu kurudi kwa Onesimo mtumwa mtoro wa Filemoni, Paulo alisema hivi: “Labda . . . alitengwa nawe kwa muda, ili uwe naye tena milele; tokea sasa, si kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu katika bwana.” (Filemoni 15, 16) Katika Milki ya Kiroma, utumwa ulilazimishwa na serikali ya kifalme, na Paulo alikubali “mamlaka iliyo kuu” kama hiyo. (Warumi 13:1-7) Yeye hakutetea kuasi kwa mtumwa bali alisaidia watu mmoja mmoja hao wapate uhuru wa kiroho wakiwa Wakristo. Kupatana na shauri lake mwenyewe kwa watumwa kujitiisha kwa mabwana wao, Paulo alimtuma Onesimo arudi kwa Filemoni. (Wakolosai 3:22-24; Tito 2:9, 10) Onesimo sasa alikuwa zaidi ya mtumwa wa kilimwengu. Yeye alikuwa mwamini mwenzi mpendwa ambaye angekuwa katika ujitiisho wa kiasi kwa Filemoni akiwa mtumwa bora zaidi, mmoja aliyeongozwa na kanuni za kimungu na kuonyesha upendo wa kidugu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki