Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 4/1 uku. 31
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Watu Walioandika Kumhusu Yesu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • “Watu Wasio na Elimu na wa Kawaida Tu”
    “Kutoa Ushahidi Kamili” Kuhusu Ufalme wa Mungu
  • Wale Walioitwa Wawe Wanafunzi wa Yesu
    Jifunze Kutoka kwa Mwalimu Mkuu
  • Kitabu Cha Biblia 41—Marko
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 4/1 uku. 31

Maswali Kutoka kwa Wasomaji

◼ Yohana 18:15 yataja mwanafunzi mwenye kujulikana na kuhani mkuu. Je! mwanafunzi huyu huyu ndiye hapo mapema kidogo aliyekimbia “yu uchi,” kama isemwavyo kwenye Marko 14:51, 52?

Sivyo, yaonekana kwamba mtu huyo mwenye kujulikana na kuhani mkuu alikuwa mtume Yohana, hali ni mwanafunzi Marko aliyekimbia “yu uchi.”

Kwa kuchukua masimulizi haya kadiri yalivyofuata katika muda, twaanza kwenye bustani ya Gethsemane. Mitume walitenda kwa hofu Yesu Kristo alipokamatwa. “Wakamwacha, wakakimbia wote.” Mstari ule ule ufuatao katika usimulizi wa Marko waweka utofauti: “Na kijana mmoja alimfuata, amejitanda mwili wake nguo ya kitani; wakamkamata; naye akaiacha ile nguo ya kitani, akakimbia yu uchi.”—Marko 14:50-52.

Hivyo, itikio la kwanza la mitume wale 11 latofautishwa na lile la mwanafunzi huyu asiyetajwa jina, basi ni jambo la akili kukata shauri kwamba yeye hakuwa mmoja wa mitume. Tukio hili limeandikwa katika Gospeli ile tu iliyoandikwa na mwanafunzi wa mapema Yohana Marko, binamu ya Barnaba. Kwa hiyo, kuna sababu ya kuwa na maoni ya kwamba Marko ndiye aliyekuwa “kijana mmoja” aliyeanza kumfuata Yesu mkamatwa lakini akakimbia bila vazi lake la kujifunika wakati lile kundi lenye ghasia lilipojaribu kukamata yeye pia.—Matendo 4:36; 12:12, 25; Wakolosai 4:10.

Wakati fulani usiku huo, mtume Petro pia alimfuata Yesu, kwa umbali ulio salama. Katika maana hii pana ufanano; yule mwanafunzi kijana (Marko) alianza kumfuata Yesu lakini akasimama, hali baadaye wawili wa mitume waliokuwa wamekimbia walianza kumfuata Bwana-Mkubwa wao mkamatwa. Katika Gospeli ya mtume Yohana, twasoma hivi: “[Sasa, NW] wakamfuata Yesu, Petro na mwanafunzi mwingine. Na, mwanafunzi huyo alikuwa amejulikana na Kuhani Mkuu, akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani Mkuu.”—Yohana 18:15.

Mtume Yohana atumia jina “Yohana” kwa kurejezea Yohana Mbatizaji lakini hajirejezei mwenyewe kamwe kwa jina. Mathalani, yeye aandika juu ya “yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya.” Vivyo hivyo: “Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema kweli.” (Yohana 19:35; 21:24) Angalia pia Yohana 13:23: “Palikuwapo mmoja wa wanafunzi wake, ameegama kifuani pa Yesu, ambaye Yesu alimpenda.” Hiyo ilikuwa muda mfupi tu kabla ya kukamatwa kwa Yesu. Baadaye siku hiyo Yesu mtundikwa alichagua mwanafunzi mmoja, ambaye Yohana amtaja kwa maneno kama hayo: “Alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao.”—Yohana 19:26, 27; linganisha Yohana 21:7, 20.

Kitabia hiki hiki cha kutojitaja jina chaonekana wazi kwenye Yohana 18:15. Zaidi ya hilo, Yohana na Petro  wahusianishwa katika ule usimulizi wa baada ya ufufuo kwenye Yohana 20:2-8. Vionyeshi hivi vyadokeza kwamba mtume Yohana ndiye aliyekuwa “amejulikana na Kuhani Mkuu.” Biblia haiandai habari za msingi juu ya jinsi yule mtume Mgalilaya (Yohana) angaliweza kuwa alipata kumjua, na kupata kujulikana na, kuhani mkuu. Lakini kujulikana kwake na watu wa nyumba ya kuhani mkuu kuliwezesha Yohana kumpita mtunza-milango na kuingia ndani ya ua na kupata ruhusa ya kuingiza Petro pia.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki