Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w91 4/15 kur. 2-4
  • Je! Amani ya Ulimwengu Yatazamiwa Kuwa Karibu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Amani ya Ulimwengu Yatazamiwa Kuwa Karibu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Vita Vilivyosahauliwa
  • Je! Kuna Tumaini la Amani?
  • Amani ya Kweli—Kutoka Chanzo Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Jinsi Ambavyo Amani Yaweza Kupatikana Duniani
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1980
  • Acha “Amani Ya Mungu” Ilinde Moyo Wako
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Amani Itakuja Wakati Gani Hasa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
w91 4/15 kur. 2-4

Je! Amani ya Ulimwengu Yatazamiwa Kuwa Karibu?

WAKATI wote wa historia, hakujapata kuwa ukosefu wowote wa mipango ya amani na matangazo rasmi ya amani ya namna moja au nyingine. Kwa kusikitisha, inaonekana kwamba kumekuwa vita vya wingi uo huo kuibatilisha. Kuhusu mapatano na matangazo ya amani, watu walio wengi wamejifunza kutoyategemea sana.

Hata hivyo, katika muda wa miaka michache iliyopita, wachunguzi na wachanganua habari wengi wameanza kuona kwamba jambo tofauti linatokea. Wamezusha uwezekano kwamba, yajapokuwa matatizo ya mahali pamoja wakati huu huenda ikawa hali iko tayari kwa ajili ya amani ya ulimwengu. Taasisi ya Stockholm International Peace ilisema, “Tumaini la suluhisho lenye amani la mapigano lina msingi bora kuliko katika mwaka mwingine wowote tangu mwisho wa Vita ya Ulimwengu 2.” Mleta habari kwa barua mashuhuri aliongozwa na matukio ya upesi-upesi katika Ulaya Mashariki kutangaza rasmi hivi: “Amani duniani inaonekana kuwa inawezekana zaidi sasa kuliko katika wakati wowote mwingine tangu Vita ya Ulimwengu 2.” Hata jarida The Bulletin of the Atomic Scientists lilionyesha maoni haya. Katika 1988 liligeuza ile saa yalo maarufu ya siku ya maangamizi kutoka dakika tatu kabla ya usiku wa manane hadi dakika sita kabla ya usiku wa manane, halafu katika Aprili 1990 iligeuzwa nyuma zaidi hadi dakika kumi kabla ya usiku wa manane.

Yote hayo yalitokeza matazamio mazuri na ustarehe mwingi sana kabla ya vita katika Mashariki ya Kati kutokea. Lakini hata tangu wakati huo, watu wengi husema kwamba Vita vya Maneno na kushindania kuunda silaha kati ya mataifa yenye nguvu mno vimekwisha. Wengine walikuwa wakikisia juu ya jambo la kufanya na pesa zote ambazo serikali zinatumaini kuweka kutokana na upunguo wa malipo ya kijeshi. Je! inawezekana kwamba wakati wa amani ya kudumu kwa kweli umekuja? Je! kweli mataifa yanajifunza ‘kufua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu’? (Isaya 2:4) Mambo ya hakika yanaonyesha nini?

Vita Vilivyosahauliwa

“Mwisho wa Vita vya Maneno na hali mpya ya ulegevu kati ya Mashariki na Magharibi umeshawishi wengine waamini kwamba amani imekuwa kawaida ya sasa,” laonelea The Economist la London. “Sivyo. Ikiwa ulimwengu umejiondolea chanzo kikubwa kimoja cha mkazo, bado una vidogo vidogo vingi.” Mikazo au mapigano hayo ‘madogo madogo’ ni gani?

Maabara ya Uchunguzi wa Amani ya Lentz, ambalo ni tengenezo la uchunguzi linalojiruzuku katika United States, yanaripoti kwamba tangu Septemba 1990, angalau vita 15 viliendelea vikali kuzunguka ulimwengu. Hiyo haikutia ndani mwingilio wa Iraki katika Kuwait, kwa kuwa ripoti hiyo ilihesabu vita vile tu ambavyo angalau watu elfu moja waliuawa kila mwaka hadi wakati huo. Baadhi ya vita hivyo vimekuwa vikiendelea kwa miaka 20 au zaidi. Vyote pamoja vimeondoa uhai wa 2,900,000, na wengi wa hao wamekuwa raia. Hesabu hiyo inatoa wale waliouawa katika vita vyenye umwagaji mwingi wa damu ambavyo vilikuwa vimekwisha tu mwaka uliotangulia, kama vile katika Uganda, Afghanistan, na kati ya Iran na Iraki.

Karibu watu milioni tatu wakauawa wakati ulimwengu eti una amani! Hilo lenyewe ni msiba. Hata hivyo, msiba mkubwa zaidi ni kwamba vingi vya vita hivyo vimekuwa vikiendelea kwa kweli bila kutazamwa—na bila kuombolezwa—na sehemu ile nyingine yote ya ulimwengu. Hivyo ni vile vinavyoweza kuitwa vita vilivyosahauliwa, kwa kuwa vingi vyao—mapinduzi, vita vya kindani, maasi—vinapigwa katika hili au hili la mataifa ambayo hayajasitawi sana. Kwa watu walio wengi katika mataifa yenye viwanda yaliyo na utajiri wa kiuchumi, wale nusu milioni waliouawa Sudan, au theluthi milioni waliouawa Angola, hawaonekani kwamba wanakamata kupendezwa kwao sana. Kwa kweli, kuna wale ambao hutoa hoja kwamba ulimwengu umekuwa katika kipindi cha amani kisicho na kifani tangu mwisho wa Vita ya Ulimwengu 2 kwa sababu hakujapata kuwa na vita miongoni mwa mataifa yaliyositawi na, ijapokuwa mkazo mkubwa mno na uongezeko wa silaha, yale mataifa yenye nguvu mno hayajapigana.

Je! Kuna Tumaini la Amani?

Ikiwa amani inamaanisha kutokuwa tu na vita ya nyukilia ya tufe lote, basi labda twaweza kutoa hoja kwamba mataifa ya ulimwengu tayari wamekuwa na kadiri fulani ya fanaka katika juhudi zao za amani. Sera ya Uharibifu Hakika wa Wao kwa Wao imewazuia mataifa makubwa mpaka sasa. Lakini hiyo kwa kweli ni amani? Inawezaje kuwa hivyo, wakati watu wanaishi katika hofu ya daima ya angamizano la papo hapo tena la kabisa? Tunawezaje kuongea juu ya amani wakati, kuzunguka ulimwengu, maisha ya wengi sana yanavunjwa-vunjwa, riziki yao inaharibiwa, na matumaini yao ya maisha yenye maana na yenye kutimizwa yakiwa yameondolewa na vita, vikubwa na vidogo?

Elie Wiesel mshindi wa zawadi ya Nobeli wakati mmoja aliandika hivi: “Tangu zamani za kale, watu wamekuwa wakiongea juu ya amani bila kuitimiza. Je! ni kwamba tu tunakosa ujuzi wa kutosha? Ingawa tunaongea juu ya amani, sisi hupigana. Hata nyakati nyingine sisi hupigana vita eti kwa ajili ya amani. . . . Huenda vita vikawa sehemu kubwa sana ya historia hivi kwamba haviwezi kuondolewa—kamwe.”

Je! wakati wetu ujao ni wenye kukosa raha jinsi hiyo? Au je! inawezekana kwamba ainabinadamu wamekuwa wakitafuta amani katika chanzo kisichofaa hata kidogo?

[Picha katika ukurasa wa 3]

“Kizazi hiki cha watu duniani huenda kikashuhudia mjio wa kipindi cha amani kisichobadilika katika historia ya ustaarabu.”

UPI/Bettmann Newsphotos

—Rais wa Urusi Mikhail Gorbachev, kwenye mkutano wa mazungumzo ya wakuu katika Washington, D.C., U.S.A., Mei 1990

[Hisani]

UPI/Bettmann Newsphotos

[Picha katika ukurasa wa 4]

“Ulimwengu mpya wa uhuru uko mbele yetu . . . , ulimwengu ambapo amani inadumu, ambapo biashara ina dhamiri na ambapo yoyote yanayoonekana kuwa yanawezekana kwa kweli yanawezekana.”

UPI/Bettmann Newsphotos

—Rais wa U.S. George Bush, katika mkutano wa mazungumzo ya wakuu juu ya uchumi wa ulimwengu katika Houston, Texas, U.S.A., Julai 1990

[Hisani]

UPI/Bettmann Newsphotos

“Kuta ambazo wakati mmoja zilizuia watu na mawazo zinaporomoka. Wazungu wanaamua mwisho wao wenyewe. Wanachagua uhuru. Wanachagua uhuru wa kiuchumi. Wanachagua amani.”—Tangazo rasmi la NATO kwenye mazungumzo ya wakuu katika London, England, Julai 1990

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 2]

Cover photos U.S. Naval Observatory photo (stars); NASA photo (earth)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki