Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 1/1 kur. 24-25
  • Genesareti-‘Nzuri Ajabu na Yenye Kupendeza’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Genesareti-‘Nzuri Ajabu na Yenye Kupendeza’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Njoo Uzuru Bahari ya Galilaya!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Maisha Katika Nyakati za Biblia Mvuvi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Kutumika Tukiwa Wavuvi wa Watu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Wanafunzi Wanne Watakuwa Wavuvi wa Watu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 1/1 kur. 24-25

Tamasha Kutoka Bara Lililoahidiwa

Genesareti-‘Nzuri Ajabu na Yenye Kupendeza’

“KARIBU na Ziwa la Genesareti kuna nchi tambarare yenye jina lilo hilo, iliyo na uzuri wa ajabu katika sifa zayo na katika kupendeza kwayo. Kwa sababu ya udongo wayo wenye rutuba nyingi hakuna mmea wowote ambao hausitawi huko, na wenyeji hupanda kila kitu: hali ya hewa ni yenye kiasi sana hivi kwamba inafaa jamii ya mimea ya aina tofautitofauti sana. . . . Haizai tu matunda ya aina tofautitofauti zenye kushangaza; inaendelea kutokeza ugavi wa daima. . . . Inatiwa maji na chemchemi yenye uwezo mwingi wa kuongezea udongo rutuba.”

Ndivyo mwanahistoria Josephus alivyoeleza uwanda wa pembetatu ulio kwenye ukingo wa kaskazini-magharibi mwa ile ambayo kwa kawaida huitwa Bahari ya Galilaya. Picha zilizo juu huenda zikakupa wazo fulani la jinsi uwanda huo ulivyokuwa wenye mazao, mmoja ulio na udongo wenye rutuba zaidi ya zote katika Galilaya.a Eneo hilo lilikuwa lenye maana sana katika nyakati za kale hivi kwamba mwandikaji Gospeli Luka aliliita bahari yenye maji safi iliyokuwa karibu nayo “ziwa la Genesareti.”—Luka 5:1.

Alitumia maneno hayo aliposimulia kwamba Yesu alikuja kwenye eneo hilo na kupata wanaume wanne waliokuja kuwa mitume. Je! hao walikuwa wakulima waliopata riziki kutoka kwa udongo wenye rutuba nyingi, wakipanda zabibu, jozi, zeituni, au tini? La. Matunda kama hayo yalikuwa kwa wingi kwenye Uwanda wa Genesareti, lakini hao wanaume walikuwa wavuvi, na ni rahisi kuelewa ni kwa nini walikuwa wavuvi.

Yaelekea vijito vilivyopitia uwanda huo vilipeleka baharini mimea ambayo ingeandaa chakula kingi kwa samaki. Kwa hiyo maji hayo yalijaa samaki za aina mbalimbali, hilo likitokeza utendaji mwingi wa uvuvi. Petro na Andrea walikuwa wafanya biashara ya samaki huko, kama Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo mvuvi, walivyokuwa.—Mathayo 4:18-22; Luka 5:2-11.

Mara nyingi uvuvi ulifanywa kwa kutandika nyavu kutoka kwa mashua. Hilo ndilo Petro na Andrea walilokuwa wakifanya wakati Yesu alipokaribia. Wavu mrefu, ulitandikwa katika nusu-duara. Mbao zenye kuelea zilishikilia ukingo wa juu, hali vitu vizito kwenye sehemu ya chini viliweka wavu ukiwa umenyooka kuelekea chini ya bahari. Hesabu kubwa za samaki zingeweza kukamatwa katika wavu wa jinsi hiyo. Kisha ulivutwa kwenye mashua au kuburutwa hadi sehemu iliyokuwa na maji machache zaidi, ili samaki waondolewe ufuoni. Samaki waliofaa kwa chakula wangetengwa na wale wasiofaa. Angalia usahihi wa mambo hayo madogo madogo kwenye Luka 5:4-7 na Yohana 21:6-11. Je! wewe unakumbuka kwamba Yesu alitaja njia hiyo ya uvuvi katika mfano wake wa juya (wavu)? (Mathayo 13:47, 48) Kuongezea hilo, Mathayo 4:21 hukazia kwamba mvuvi mara nyingi alihitaji kutumia wakati akitengeneza nyavu zilizoraruliwa na miamba au na samaki.

Ukisafiri karibu na ukingo wa bahari wa Genesareti, labda ungeona sehemu mbili zinazosemwa kuwa mahali ambapo mambo fulani katika huduma ya Yesu yalitukia. Moja ni kile kilima chenye mimea mibichi ambacho kutoka kwacho, kulingana na mapokeo, Yesu alitoa Mahubiri yake ya Mlimani. Mahali hapo hapapingani na masimulizi ya Gospeli, kwani Yesu alikuwa karibu na Uwanda wa Genesareti alipotoa mahubiri hayo.—Mathayo 5:1–7:29. Luka 6:17–7:1.

Sehemu nyingine inayodaiwa kuwa ya kweli haipatani na mambo ya hakika ya Biblia. Utapata kanisa linalodhaniwa kuwa limejengwa mahali ambapo Yesu aliwalisha watu 4,000 kwa mikate saba na samaki wachache. (Mathayo 15:32-38; Marko 8:1-9) Badala ya kuonyesha kwamba hilo lilitukia kwenye Uwanda wa Genesareti, usimulizi wa Marko unataja “mipaka ya Dekapoli,” iliyokuwa ng’ambo ya bahari ikiwa na umbali wa kilometa 11 kutoka hapo.—Marko 7:31.

Mathayo na Marko wasema kwamba baada ya kufanya muujiza huo, Yesu alisafiri kwa mashua hadi Magadani, au Dalmanutha. (Mathayo 15:39; Marko 8:10) Wanachuo huunganisha sehemu hiyo na Magdala (Migdali), iliyokuwa kusini tu mwa Uwanda wa Genesareti, kuelekea Tiberia. Kulingana na The Macmillan Bible Atlas, Magdala “ilikuwa maarufu kwa ajili ya utendaji wake wa kutayarisha samaki.” Uvuvi mwingi wa sehemu hiyo ya ziwa kwa hakika ungefanya utendaji huo uwe wenye kutumika na wenye faida.

Kwa kupendeza, hali ya ukame katika 1985/86 ilipunguza usawa wa maji katika Bahari ya Galilaya, ikifunua sehemu nyingi kavu za ziwa hilo. Karibu na Uwanda wa Genesareti, wanaume wawili walipata mabaki ya mashua ya kale. Wanaakiolojia waliweza kuitoa mashua hiyo ya mbao ya kuvulia samaki yenye tarehe kutoka karibu na wakati Yesu alipozuru Ziwa na Uwanda wa Genesareti.

[Maelezo ya Chini]

a Ona picha kubwa zaidi yenye rangi-rangi katika 1992 Calendar of Jehovah’s Witnesses.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 24]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 24]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 25]

Garo Nalbandian

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 25]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.y

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki