Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • jy sura 22 uku. 58-uku. 59 fu. 6
  • Wanafunzi Wanne Watakuwa Wavuvi wa Watu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wanafunzi Wanne Watakuwa Wavuvi wa Watu
  • Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Habari Zinazolingana
  • Wanafunzi Wanne Waitwa
    Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Wanafunzi Wanne Waitwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Kutumika Tukiwa Wavuvi wa Watu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Alishinda Woga na Shaka
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
jy sura 22 uku. 58-uku. 59 fu. 6
Yesu anazungumza na Petro, Andrea, Yakobo, na Yohana kwenye ufuo wa Bahari ya Galilaya

SURA YA 22

Wanafunzi Wanne Watakuwa Wavuvi wa Watu

MATHAYO 4:13-22 MARKO 1:16-20 LUKA 5:1-11

  • YESU AWAITA WANAFUNZI WAANDAMANE NAYE WAKATI WOTE

  • WAVUVI WA SAMAKI WANAKUWA WAVU VI WA WATU

Baada ya watu wa Nazareti kujaribu kumuua Yesu, anahamia katika jiji la Kapernaumu, karibu na Bahari ya Galilaya, ambayo pia inaitwa “ziwa la Genesareti.” (Luka 5:1) Hilo linatimiza unabii wa kitabu cha Isaya kwamba watu wa Galilaya wanaokaa kando ya bahari wangeona nuru kuu.—Isaya 9:1, 2.

Naam, huko Galilaya, Yesu anaendelea kutangaza kwamba “Ufalme wa mbinguni umekaribia.” (Mathayo 4:17) Yesu anawakuta wanne kati ya wanafunzi wake. Hapo awali walikuwa wamesafiri pamoja naye, lakini waliporudi pamoja na Yesu kutoka Yudea, walirudia biashara yao ya kuvua samaki. (Yohana 1:35-42) Hata hivyo, sasa wanapaswa kuwa pamoja na Yesu wakati wote ili awazoeze kuendeleza huduma baada ya yeye kuondoka.

Yesu anapotembea kando ya bahari anamwona Simoni Petro, ndugu yake Andrea, na wavuvi wenzao wakitengeneza nyavu zao. Yesu anawakaribia, anaingia katika mashua ya Petro, na kumwomba asogee mbali na nchi kavu. Wanaposonga mbali kidogo na nchi kavu, Yesu anaketi na kuanza kufundisha umati uliokuwa umekusanyika ufuoni kuhusu Ufalme.

Baadaye, Yesu anamwambia Petro: “Peleka mashua mahali penye kina, kisha mshushe nyavu zenu, mvue samaki.” Petro anamjibu: “Mwalimu, tumejitahidi kuvua samaki usiku wote na hatukupata chochote, lakini nitazishusha nyavu kama ulivyoniagiza.”—Luka 5:4, 5.

Andrea, Yakobo, na Yohana wanang’ang’ana kuingiza nyavu ndani ya mashua; Petro anajiangusha mbele za Yesu

Wanashusha nyavu na kuvua samaki wengi sana hivi kwamba nyavu zinaanza kukatika! Mara moja, wanaume hao wanawapungia mkono wenzao walio katika mashua iliyo hapo karibu ili waje kuwasaidia. Baada ya muda mfupi mashua zote mbili zinajaa samaki wengi sana hivi kwamba zinaanza kuzama. Petro anapoona hivyo, anaanguka mbele za Yesu na kusema: “Bwana ondoka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi.” Yesu anamwambia: “Acha kuogopa. Kuanzia sasa utakuwa ukiwavua watu wakiwa hai.”—Luka 5:8, 10.

Yesu anawaambia Petro na Andrea: “Nifuateni, nami nitawafanya muwe wavuvi wa watu.” (Mathayo 4:19) Pia, anawaita wavuvi wengine wawili, Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo. Wao pia wanakubali bila kusitasita. Basi, wanaume hao wanne wanaacha biashara yao ya kuvua samaki na kuwa wanafunzi wa kwanza wa Yesu wanaoandamana naye wakati wote.

  • Yesu anawaita watu wa aina gani wawe wanafunzi wake wa wakati wote, nao ni akina nani?

  • Ni muujiza gani ambao unamshtua Petro?

  • Sasa wanafunzi hao wanne watakuwa wakifanya uvuvi wa aina gani?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki