Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • gt sura 22
  • Wanafunzi Wanne Waitwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wanafunzi Wanne Waitwa
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
  • Habari Zinazolingana
  • Wanafunzi Wanne Waitwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Wanafunzi Wanne Watakuwa Wavuvi wa Watu
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
  • Kutumika Tukiwa Wavuvi wa Watu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Alishinda Woga na Shaka
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
gt sura 22

Sura 22

Wanafunzi Wanne Waitwa

BAADA ya lile jaribio la kumuua Yesu katika Nazareti mji wa kwao, yeye ahamia mji wa Kapernaumu karibu na Bahari ya Galilaya. Jambo hilo latimiza unabii mwingine wa Isaya. Huo ndio uliotabiri kwamba watu wa Galilaya wenye kukaa karibu na bahari wangeona nuru kubwa.

Yesu aendeshapo kazi yake ya kuchukua nuru kwa kuhubiri Ufalme hapa, akuta wanne wa wanafunzi wake. Hao walikuwa wamesafiri pamoja naye mapema kidogo lakini wakarudia biashara yao ya uvuvi wa samaki waliporejea pamoja na Yesu kutoka Yudea. Yaelekea kuwa Yesu sasa awatafuta, kwa kuwa ni wakati wake kuwa na wasaidizi walio imara, na wa kudumu ambao angeweza kuzoeza waiendeshe huduma akiisha kwenda zake.

Kwa hiyo Yesu anapotembea kandokando ya ufuo wa bahari na kumwona Simoni Petro na wenzi wake wakisafisha nyavu zao, awaendea. Apanda na kuingia katika mashua ya Petro na kumwomba asonge ndani zaidi kutoka nchi kavu. Wanapoondoka na kwenda umbali fulani, Yesu aketi mashuani na kuanza kufundisha umati wakiwa ufuoni.

Baadaye, Yesu amwambia Petro hivi: “Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki.”

“Bwana Mkubwa,” Petro ajibu, “tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha, tusipate kitu; lakini kwa neno lako nitazishusha nyavu.”

Nyavu zinaposhushwa, umati mkubwa sana wa samaki wanaswa hivi kwamba nyavu zaanza kukatika. Wanaume hao wafanya haraka kuwapungia mkono wenzao walio katika mashua ya karibu ili waje wasaidie. Upesi mashua zote mbili zajaa samaki wengi sana hivi kwamba zaanza kuzama. Kuona hivyo, Petro ajitupa chini mbele ya Yesu na kusema: “Ondoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.”

“Usiogope,” Yesu ajibu. “Tangu sasa utakuwa ukivua watu.”

Yesu amwalika pia Andrea ndugu ya Petro. “Njoni mnifuate,” awahimiza, “nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.” Wavuvi wenzao Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, wapewa mwaliko uo huo, nao pia waitikia bila kusitasita. Kwa hiyo hao wanne waacha biashara yao ya kuvua samaki na kuwa wafuasi wanne wa kwanza wenye kumfuata Yesu kwa ukawaida, bila kuyumbayumba. Luka 5:1-11; Mathayo 4:13-22; Marko 1:16-20; Isaya 9:1, 2.

▪ Kwa nini Yesu awaita wanafunzi wake wamfuate, nao ni akina nani?

▪ Ni muujiza gani wamwogopesha sana Petro?

▪ Ni uvuvi wa namna gani ambao Yesu aalika wanafunzi wake wafanye?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki