Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 2/1 kur. 29-30
  • “Fadhili-Upendo Zake Zimethibitika Kuwa Kuu”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Fadhili-Upendo Zake Zimethibitika Kuwa Kuu”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Katika Jeshi na Baadaye
  • Maisha Yangu Yabadilika
  • Huduma ya Wakati Wote
  • Kutumikia kwa Moyo Wote Licha ya Majaribu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Kumtumikia Mungu Nyakati za Magumu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Je, Unaweza Kutumika Mahali Penye Uhitaji Mkubwa Zaidi wa Wahubiri?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Wakati Ambapo Damu Ilimwagwa Katika Jina la Kristo
    Amkeni!—2005
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 2/1 kur. 29-30

“Fadhili-Upendo Zake Zimethibitika Kuwa Kuu”

KAMA ILIVYOSIMULIWA NA JOSÉ VERGARA OROZCO

Je! unafikiri maisha yako yangejawa na nguvu mpya katika umri wa miaka 70? Yangu yalikuwa hivyo. Na hiyo ilikuwa miaka zaidi ya 35 iliyopita.

Kwa fadhili-upendo za Yehova, tangu 1962, nimetumikia nikiwa mhudumu painia wa kawaida katika kundi la Mashahidi wa Yehova la El Carrizal katika jimbo la Jalisco, Meksiko. Acheni niwaambie machache kuhusu malezi yangu.

NILIZALIWA katika jimbo la Michoacán, Meksiko, katika Agosti 18, 1886. Baba yangu alikuwa mshiriki wa jamii ya kitaifa ya kisiri, kwa hiyo familia yetu haikuwa inaenda kwenye Kanisa Katoliki, wala hatukushiriki katika sherehe zozote za kidini za Katoliki, au kuwa na mifano yoyote nyumbani kwetu.

Nilipokuwa na miaka 16, baba yangu aliondoka kwenda kufanya kazi katika United States, lakini akafanya mpango ili mtu fulani anifundishe biashara fulani. Hata hivyo, miaka miwili baadaye, mwanamume huyo alinipeleka Meksiko City nipate mazoezi kwenye chuo cha kijeshi. Baadaye nilianza kazi-maisha katika jeshi la Meksiko.

Katika Jeshi na Baadaye

Nilipigana katika Mapinduzi ya Meksiko ambayo yalianza katika 1910. Sisi wanaume wachanga wote chuoni tulimwunga mkono Francisco I. Madero, aliyekuwa mwanamapinduzi aliyepinga utawala wa kimabavu wa Porfirio Díaz. Tulimwunga mkono Madero hadi kifo chake katika 1913, na baada ya hapo, tukamwunga mkono Venustiano Carranza, aliyetumikia akiwa rais wa Jamhuri kuanzia 1915 hadi 1920. Tuliitwa Carranzistas

Katika pindi nne tofauti tofauti, nilijaribu bila kufanikiwa, nitoke jeshini. Mwishowe nilijitenga na nikawa mtoro. Tokeo likawa kwamba baba yangu, aliyekuwa amerudi Meksiko, alitiwa gerezani. Siku moja, nikijisingizia kuwa mpwa wake, nilimtembelea gerezani. Tuliwasiliana kwa kuandika kwenye vikaratasi vidogo ili walinzi wasitusikie. Ili kuzuia yeyote asijue niliyekuwa, niliila karatasi.

Baada ya baba yangu kufunguliwa kutoka gerezani, alinitembelea akaniomba nijisalimishe kwa mamlaka. Nilifanya hivyo, na kwa mshangao wangu Jemadari aliyehusika hakunitia kifungoni. Badala yake, alidokeza kwamba nihamie United States. Nilifuata dokezo lake nikaishi huko kuanzia 1916 hadi 1926.

Katika 1923, nilioa Mwanamke Mmeksiko aliyekuwa akiishi katika United States pia. Nilijifunza kazi ya ujenzi, tukachukua ulezi wa kisichana kidogo. Alipokuwa na umri wa miezi 17, tulirudi Meksiko tukawa wakazi wa Jalpa, Tobasco. Halafu ‘uasi wa Kristero’ ukaanza, ukaendelea kutoka 1926 hadi 1929.

Wakristero walitaka nijiunge nao. Hata hivyo, familia yangu na mimi, tulipendelea kukimbilia Aguascalientes State. Baada ya kuishi mahali mbalimbali katika jamhuri ya Meksiko, katika 1956 tulikaa Matamoros, Tamaulipas, ambako nilianza kusimamia kazi za ujenzi.

Maisha Yangu Yabadilika

Huu ndio wakati maisha yangu yalipoanza kubadilika. Binti yangu, ambaye kwa sasa alikuwa ameolewa na kuishi ng’ambo ya mpaka katika Brownsville, Texas, U. S. A., alitutembelea mara nyingi. Siku moja alisema: “Baba, familia nyingi zinakutana katika jumba la jumuiya hivi sasa. Twende tukaone ni nini kilichoko huko.” Lilikuwa kusanyiko la Mashahidi wa Yehova. Binti yangu, mkwe-mwanangu, mjukuu wangu, mke wangu, na mimi tulihudhuria siku zote nne za kusanyiko hilo.

Kuanzia mwaka huo na kuendelea, tulihudhuria mikutano ya Kikristo ya Mashahidi wa Yehova. Nilifanya maendeleo ya kiroho katika Meksiko, huku binti yangu akifanya vivyo hivyo katika United States. Upesi nilianza kuambia wafanya kazi wenzangu kweli za Biblia nilizokuwa nikijifunza. Nilipokea magazeti kumi ya kila toleo la Mnara wa Mlinzi na Amkeni! niliyogawa miongoni mwa wafanya kazi wenzangu. Watano kati ya wale walio ofisini na watatu kati ya wahandisi pamoja na baadhi ya wafanya kazi wengine walikuja kuwa Mashahidi.

Lo, ilikuwa baridi kama nini Desemba hiyo ya tarehe 19, 1959, nilipobatizwa katika mto! Kila mtu aliyebatizwa siku hiyo alikuwa mgonjwa kwa sababu ya maji baridi kweli kweli. Binti yangu alibatizwa kabla yangu, na mke wangu, ingawa hakubatizwa kamwe, alifikia hatua ya kujua kweli ya Biblia, na alikuwa mwenye kushirikiana sana.

Huduma ya Wakati Wote

Nilihisi kuwa mwenye deni kwa Mungu kwa fadhili-upendo zote za Mungu, kwa hiyo Februari 1962, nilipokuwa na umri wa miaka 75, nikaanza huduma ya wakati wote nikiwa painia. Miaka michache baadaye, katika 1968, mke wangu akafa. Nilitaka kutumikia katika nchi nyingine, lakini kwa sababu ya umri wangu, ndugu hawakuona ingefaa nifanye hivyo. Hata hivyo, katika 1970, nilipewa mgawo wa kuwa painia katika Colotlán katika jimbo la Jalisco, ambako kulikuwa na kundi dogo.

Katika Septemba 1972, mwangalizi wa mzunguko alidokeza nihamie kwenye mji mdogo wa El Carrizal, ambao uko karibu na Colotlán. Katika Novemba ya mwaka huo, kundi lilianzishwa hapo, na nikawekwa kuwa mzee. Hata ingawa ni mji ulio mbali sana na mingine, watu 31 huhudhuria mikutano ya kundi.

Ujapokuwa umri wangu, mimi bado ni mwenye nguvu katika huduma, nikijaribu sana kuwasaidia watu wasababu juu ya itikadi zao. Mathalani, katika rozari (tasbihi) Wakatoliki wenye moyo mweupe hurudia ile sala ya Atukuzwe Mariamu: ‘Atukuzwe, Mariamu, aliyejawa na neema; Bwana yu pamoja nawe.’ Sala hiyo yaongeza: ‘Mariamu Mtakatifu, Mama wa Mungu.’ Mimi huwauliza: ‘Hilo lawezaje kuwa hivyo? Ikiwa Mungu ndiye mwenye kumwokoa Mariamu, Yeye anawezaje tena kuwa mwana wake?’

Sasa nina umri wa miaka 105 na nimetumikia nikiwa mzee na painia wa kawaida katika El Carrizal, Jalisco, kwa karibu miaka 20 Ninahisi kwamba imekuwa ni mapenzi ya Yehova kwamba nimeishi miaka hiyo mingi, kwa kuwa katika njia hii naweza kulipia wakati ule niliopoteza nilipokuwa simtumikii.

Jambo moja ambalo nimejifunza ni kwamba twapaswa sikuzote kuwa na uhakika kwamba Hakimu Mkuu wetu anatuangalia kutoka kiti chake cha uadilifu na hutuandalia sisi mahitaji yetu. Kama Zaburi 117:2 isemavyo: “Maana fadhili [fadhili-upendo, NW] zake kwetu sisi ni kuu.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki