Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w92 5/1 kur. 24-25
  • Aliandalia Israeli Katika Sinai

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Aliandalia Israeli Katika Sinai
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Sinai Mlima wa Musa na wa Rehema
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Jangwa la Yuda Halizai Lakini Linasisimua
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Hupaswi Kumsahau Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
w92 5/1 kur. 24-25

Tamasha Kutoka Bara Lililoahidiwa

Aliandalia Israeli Katika Sinai

EBU wazia mamilioni ya—wanaume, wanawake, na watoto—wakielekea kuingia “jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji”!

Maneno hayo ya Mungu yanayopatikana kwenye Kumbukumbu la Torati 8:15 hukazia ile ambayo huenda ikaonekana kuwa safari yenye kuhofisha iliyokuwa mbele ya Waisraeli walipotoka Misri na kwenda kwa miguu ndani ya jangwa la Sinai. Tatizo moja kubwa: Nani angeandaa chakula na maji ya kutosha?

Waisraeli walikuwa wamekuwa katika utumwa huko nyuma katika delta ya Naili, lakini hawakukosa chochote. Michoro yenye rangi katika maziara ya kale huonyesha namna mbalimbali za mizabibu, matango, na mimea mingine, pamoja na samaki na ndege ambao wangefanyiza chakula cha namna namna. Basi, lile lalamiko la kutamani katika jangwa lilikuwa kweli kama nini: “N’nani atakayetupa nyama tule? Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu”!—Hesabu 11:4, 5; 20:5.

Baada ya Waisraeli kuvuka Bahari Nyekundu, walipata kuelewa jinsi Sinai ilivyokuwa hasa. Hawakufuata ile njia ya biashara iliyofuatwa kwa kawaida iliyokuwa upande wa kaskazini bali waligeuka kuelekea ukingo wa peninsula hiyo ya pembetatu. Kufikia wakati walipokuwa wameenda kilometa yapata 80 kupitia jangwa hilo, uhitaji wao wa maji ulionekana kuwa mkubwa. Wasingeweza kunywa maji yale waliyopata, kwa kuwa yalikuwa machungu na labda yalikuwa na magonjwa. “Tunywe nini?” wakalia. Mungu aliingilia, akigeuza maji hayo kuwa matamu.—Kutoka 15:22-25.

Angalia mandhari ya msafara wa ngamia ulio juu. Waweza kuthamini lile swali kuhusu jinsi Israeli wangeweza kuendelea kupitia jangwa hilo kuelekea Mlima Sinai. Wangeendeleaje kupata maji ya kutosha—na chakula—kwa ajili yao wenyewe na pamoja na makundi yao ya wanyama na mifugo ambayo walihitaji kudumisha wakiwa hai?—Kutoka 12:38.

Walisonga zaidi kuelekea kusini na upesi wakapata maji na chakula chenye kuburudisha katika Elimu. (Kutoka 15:27) Hata hivyo, hicho hakikuwa kituo chao. Walikuwa wakielekea “mlima wa Mungu,” Mlima Sinai. (Kutoka 3:1; 18:5; 19:2; 24:12-18) Huo ulikuwa umbali wa kilometa 120 kutoka hapo—kilometa za bara kavu lenye mawe mawe.

Kikundi hicho kikubwa mno kilipoendelea kuelekea Mlima Sinai, kilikuja karibu—na yaelekea kusimama kwenye—oasisi (chemchemi ya jangwa) kubwa iitwayo Feiran. Sehemu ndogo yalo yaonekana katika picha iliyoko kwenye ukurasa unaokabili huu.a Inapitia chini jangwani, kuelekea Bahari Nyekundu (Ghuba ya Suezi). Wangeweza kupata burudisho lililoje huko!

Ingawa jangwa la Sinai huenda kwa ujumla likafaa ule ufafanuzi wa kuwa “jangwa lile kubwa lenye kitisho,” Waisraeli wangeweza kuonea shangwe kivuli cha mitende yenye fahari na miti mingine kwenye oasisi ya Feiran. Wangepata tende tamu za kutosha, zikiandaa chakula papo hapo na ugavi ambao wangeweza kubeba pamoja nao.

Hayo yote yaliwezekana kwa sababu maji ya ardhini yalibubujika katika Feiran. Ebu wazia jinsi ungehisi ikiwa ungalikuwa katika jangwa kavu na kwa ghafula ukapata maji safi ya kunywa! Hilo laonyesha kwamba hata katika Sinai kuna mahali mahali ambapo maji hupatikana. Nyakati nyingine ni lazima kisima kichimbwe hadi kina kirefu. Wakati huo ingekuwa kazi nyingi kuvuta ndoo au mitungi ya umajimaji huo ulio muhimu, hasa ikiwa vikundi vya wanyama na mifugo vilihitaji kupewa maji. Hadi siku ya leo Wabedouini wa Sinai huvutwa na visima ambamo waweza kuchota maji kwa ajili yao wenyewe na ngamia wao.—Linganisha Mwanzo 24:11-20; 26:18-22.

Naam, zijapokuwa pindi ambazo walilalamikia hali iliyoonekana kuwa ya upungufu usioondoleka, Waisraeli walikuwa na maji na chakula. Nyakati nyingine Mungu aliandaa hayo kimuujiza. (Kutoka 16:11-18, 31; 17:2-6) Nyakati nyinginezo yaonekana aliwaongoza kwenye “mahali pa kupumzika” ambapo mahitaji yao halisi yangeweza kutoshelezwa kwa ugavi mbalimbali wa kiasili. (Hesabu 10:33-36) Kwa wakati huo wote, aliwanyoshea ule wingi uliowangojea waaminifu katika Bara Lililoahidiwa.—Kumbukumbu la Torati 11:10-15.

[Maelezo ya Chini]

a Picha hiyo inapatikana kwa ukubwa zaidi katika 1992 Calender of Jehovah’s Witnesses.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 24]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 24]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 24, 25]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 25]

Pictorial Archive (Near Eastern History) Est.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki