Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w93 4/15 kur. 2-4
  • Moto wa Helo Wawaka au Wafifia?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Moto wa Helo Wawaka au Wafifia?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kurudi kwa Helo
  • Maswali Ambayo Yametokezwa
  • Watu Wanauonaje Moto wa Mateso Leo?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2002
  • Ni Nani Wanaoenda Kuzimu?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Je, Moto wa Mateso Ni Halisi? Kuzimu Ni Wapi Kulingana na Biblia?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Fundisho Lililoenea
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
w93 4/15 kur. 2-4

Moto wa Helo Wawaka au Wafifia?

MWALIMU mmoja Mprotestanti Jonathan Edwards alikuwa akiihofisha mioyo ya Waamerika Wakoloni wa karne ya 18 kwa mafafanuzi yake ya waziwazi juu ya helo. Wakati mmoja alisimulia mandhari moja ambamo Mungu aliwaning’iniza watenda dhambi juu ya miali ya moto kama buibui wenye kuchukiza mno. Edwards alikemea kundi lake hivi: “Ee mtenda dhambi, unaning’inia kwenye uzi mwembamba, huku ukizungukwa na miali ya moto ya ghadhabu ya kimungu, ikiwa tayari wakati wote kuuunguza, na kuuchoma vipande vipande.”

Hata hivyo, punde tu baada ya Edwards kutoa mahubiri hayo yenye sifa mbaya, imani katika fundisho la moto wa helo ilianza kupungua.a Kitabu The Decline of Hell, cha D. P. Walker, chasema kwamba “kufikia mwongo wa nne wa karne ya 18 fundisho la mateso ya milele kwa wale waliolaaniwa milele lilikuwa likipingwa peupe.” Katika karne ya 19, imani katika fundisho la moto wa helo iliendelea kupungua, na kufikia katikati ya karne ya 20, maoni ya Edwards juu ya helo kuwa ‘tanuri la moto ambamo majeruhi walo wanateswa sana katika akili zao na katika miili yao milele’ yaliacha kuwa kichwa cha mazungumzo yenye adabu. Mwandishi mmoja wa habari Jeffrey Sheler alisema kwamba, “yale masimulizi ya helo hayakuwa yenye kuhofisha sana kama yalivyokuwa, yaliposhambuliwa na maoni ya kiakili ya ki-siku-hizi na kufifishwa na yale mambo yenye kuhofisha ya Hiroshima na yale Machinjo Makubwa.”

Wahubiri wengi walikuwa wameacha kupendezwa na mafundisho juu ya moto na kiberiti. Mahubiri yenye idili juu ya mambo yenye kuhofisha ya helo yalitoweka kutoka katika makanisa makubwa ya Jumuiya ya Wakristo. Kwa wanatheolojia wengi, helo ikawa habari ya zamani za kale sana kwa elimu yenye uzito. Miaka kadhaa iliyopita mwanahistoria wa kanisa alikuwa akifanya utafiti kwa ajili ya mhadhara wa chuo kikuu juu ya helo, na alichunguza faharisi za majarida kadhaa ya chuo. Hakuweza kupata limeorodheshwa hata mara moja. Kulingana na gazeti Newsweek, mwanahistoria huyo alimalizia hivi: “Helo ilitoweka. Na hakuna yeyote aliyeona hilo.”

Kurudi kwa Helo

Ilitoweka? Sivyo hasa. Kwa kushangaza, katika miaka ya hivi karibuni fundisho la helo limetokea tena katika mahali fulani-fulani. Utafutaji wa maoni mbalimbali uliofanywa Amerika unaonyesha kwamba idadi ya watu wanaosema kwamba wanaamini kuna helo iliongezeka kutoka asilimia 53 katika 1981 hadi asilimia 60 katika 1990. Ukiongeza kwa idadi hiyo zile harakati za kuhubiri juu ya helo za kievanjeli zenye kuenea ulimwenguni pote, inakuwa wazi kwamba kurudi kwa helo kwa uzito katika fikira za Jumuiya ya Wakristo kwelikweli ni tukio lisilo la kawaida la duniani pote.

Lakini, je, kurudi huko kunaathiri tu wahudhuriaji-kanisa, au kumewafikia makasisi pia? Jambo la kweli ni kwamba fundisho la moto wa helo kama vile lilivyofundishwa na Jonathan Edwards miaka 250 iliyopita halikutokomea kamwe katika mafundisho ya makanisa ya Jumuiya ya Wakristo yenye kushikilia maoni ya kale. Katika 1991, U.S.News & World Report lilisema hivi: “Hata miongoni mwa madhehebu fulani makubwa yanayokubali maoni mbalimbali, kuna ishara kwamba wanatheolojia wanaanza kufikiri kwa uzito zaidi kuhusu lile wazo la helo kuliko vile ambavyo wamekuwa wakifikiri katika miongo mingi iliyopita.” Kwa wazi, baada ya miaka mingi ya kupuuzwa, fundisho la moto wa helo linajulikana sana kwa mara nyingine tena na linaonwa kuwa la maana ulimwenguni pote. Hata hivyo, je lingali lenye kuhofisha?

Maswali Ambayo Yametokezwa

Mwanatheolojia W. F. Wolbrecht hakuwa na shaka lolote: “Helo ni helo, na hakuna tamaa wala wazo lolote la kibinadamu liwezalo kuipunguza hata kidogo isiwe laana ya milele.” Wahudhuriaji-kanisa wengi hawana uhakika sana. Ingawa hawatilii shaka kuwako kwa helo, bado wana maswali kuhusu asili ya helo. Mwanatheolojia mwingine anakiri hivi: “Kwangu pia, helo ni jambo halisi lisilotiliwa shaka, ambalo limetangazwa waziwazi katika ushuhuda wa Biblia, lakini asili yayo halisi ndilo tatizo.” Naam, kwa idadi yenye kuongezeka ya wanatheolojia na watu wa kawaida, swali leo si “Je, kuna helo?” tena, bali ni “Helo ni nini?”

Wewe ungejibuje? Umeambiwa nini kuhusu asili ya helo? Na kwa nini Wakristo wenye mioyo myeupe hufadhaishwa na fundisho hilo?

[Maelezo ya Chini]

a Katika Julai 8, 1741, Edwards alitoa mahubiri yenye kichwa “Sinners in the Hands of an Angry God” (Watenda Dhambi Wakiwa Mikononi mwa Mungu Mwenye Hasira).

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 2]

Cover: Doré’s illustration of Tumult and Escape for Dante’s Divine Comedy

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Kielezi cha Doré cha Devils and Virgil cha Divine Comedy ya Dante

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki