Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w93 8/1 uku. 3
  • “Yaonekana Hatuwezi Kuwasiliana Hata Kidogo!”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Yaonekana Hatuwezi Kuwasiliana Hata Kidogo!”
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kabla na Baadaye—Kanuni za Biblia Zilimfanya Abadilike Sana
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • ‘Alimkumbuka Muumba Wake Katika Siku za Ujana Wake’
    Amkeni!—1994
  • Yule Malaika Mkuu Mikaeli Ni Nani?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Yule Malaika Mkuu Mikaeli Ni Nani?
    Biblia Inafundisha Nini Hasa?
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1993
w93 8/1 uku. 3

“Yaonekana Hatuwezi Kuwasiliana Hata Kidogo!”

MICHAEL, aliye wakili, alipaswa kuwa mwasilianaji mwenye nguvu. Kazi yake ilitaka hivyo. Lakini baada ya miaka 16 ya ndoa, Michael alilazimika kutambua kwamba alipokuja nyumbani kwa mke wake, Adrian, ilionekana kana kwamba stadi zake za kuwasiliana zilitoweka. “Kulalamika, kuchambua-chambua, kusingizia mambo,” Michael akumbuka, “sikuzote Adrian na mimi tulikuwa tunabishana, na nikafikiri hilo lingetumaliza kabisa. Nilijiuliza kama hiyo ilikuwa ndiyo ndoa, shambulio la daima la kutoridhika na uchokozi. Kama hilo lingekuwa ndilo fungu letu kwa maisha yetu yote pamoja, nilitaka kutoroka ndoa hiyo—bila mchezo. Nisingeweza hata kidogo kukabili miaka 20, 30, 40 ya aina hiyo ya uchokozi na mkazo wa daima.”

Maoni ya moyoni kama hayo kwa kweli si ya Michael na Adrian peke yao. Ni ya halisi kwa wenzi wengi ambao uhusiano wao hubadilika-badilika kati ya hali ya kupigana na muda mfupi wa kutopigana. Mazungumzo sahili zaidi hulipuka kuwa vita vya maneno. Wao “wanasikia” mambo yasiyosemwa. Wanasema mambo yasiyomaanishwa. Wanashambulia na kushtaki, na kisha kuingia katika hali ya unyamavu wenye kinyongo. Hawatengani, na bado wao si “mwili mmoja.” (Mwanzo 2:24) Uhusiano umesimama. Kurudi nyuma kungemaanisha kutengana; kuendelea mbele kungemaanisha kukabili hitilafu moja kwa moja. Ili kuepuka maumivu ya kuchagua lolote kati ya mambo hayo mawili, wenzi hao huamua kutokaribiana kihisiamoyo.

Wenzi hao wanahitaji ‘kupata mwelekezo wenye ustadi’ katika ndoa yao. (Mithali 1:5, New World Translation) Mwelekezo huo unapatikana katika Neno la Mungu, Biblia. Barua ya pili ya Paulo kwa Timotheo inathibitisha kwamba Biblia “lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza.” (2 Timotheo 3:16) Hivyo ndivyo hali ilivyo katika kusuluhisha mvunjiko wa uwasiliano katika ndoa, kama vile tutakavyoona.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki