Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w94 2/1 uku. 19
  • ‘Jina la Yehova Ni Ngome Imara’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Jina la Yehova Ni Ngome Imara’
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wakiwa Hai Bado!
  • Nguvu za Sala
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2005
  • Maisha ya Jijini Katika Miteremko ya Vilima vya Caracas
    Amkeni!—1993
  • Imeandikwa Kwamba Nitamwona
    Amkeni!—2004
  • Tegemea Roho ya Mungu Unaposhughulika na Mabadiliko ya Maisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
w94 2/1 uku. 19

Wapiga Mbiu ya Ufalme Waripoti

‘Jina la Yehova Ni Ngome Imara’

TWAISHI katika nyakati zenye msukosuko. Maisha zetu zionekanazo kuwa zenye uthabiti zaweza kubadilika mara hiyo, na bila onyo watu fulani wamejikuta katika hatari kubwa kabla ya wao kung’amua hilo. Hatari yaweza kuja kutokana na msukosuko wa kisiasa, mshambulizi mjeuri, msiba wa asili, au ugonjwa mahututi. Hali iwe ni nini, Mkristo apaswa ageukie wapi maisha yake yakiwa hatarini?

David, mishonari aishiye kwenye mojayapo ofisi za tawi za Watch Tower Society, alijifunza jibu la swali hilo kutokana na ono lenye kuogopesha. Akiwa na mgawo wa kuwa dereva, aliondoka ofisini mapema asubuhi moja kwenda kuwachukua Wanabetheli wenye kusafiri (wajitoleaji wanaoishi nje ya ofisi ya tawi). Bado kulikuwa na giza. Alikuwa amemchukua Rosalía na alikuwa akipitia kituo cha polisi aliposikia mfyatuko wa bunduki kwa mara ya kwanza.

Kisha mambo yakatukia upesi. Alisikia sauti kama ya fataki kubwa akang’amua kwamba hewa ilikuwa ikitoka katika mojayapo magurudumu. Kwa ghafula aliona askari-jeshi akiwa amesimama katikati ya barabara akimlenga bunduki moja kwa moja. Mambo matatu yalitukia karibu mara iyo hiyo: Mfululizo wa risasi ulitoboa-toboa upande wa gari hilo aina ya Jeep, ukiyavunja madirisha; David na Rosalía waliinama; askari-jeshi huyo alifyatua bunduki kupitia kioo cha mbele cha gari kwa usawa wa jicho.

Jeep ilipokuwa ikipigwa mfululizo wa risasi, David alikanyaga breki kadiri awezavyo akiwa ameinama bado. David na Rosalía pia walifikiri kwamba wangekufa. Walisali kwa Yehova kwa sauti kubwa, wakimwomba awalinde. Rosalía alisema baadaye kwamba katika dakika hizo alijiuliza familia yake ingeitikiaje kama ingesikia kwamba amekufa!

Wakiwa Hai Bado!

Kelele kutokana na mifyatuko ya bunduki na vioo vikivunjika ilikoma hatimaye, na David akamtupia jicho Rosalía. Alipoona mviringo wa damu mgongoni pake, alikuwa na hofu. Lakini kipande cha kioo kilichoruka, wala si risasi, kilikuwa kimejipenyeza humo. Magoti ya Rosalía yalikuwa yakitoka damu kutoka kwenye mikato iliyofanywa na vioo vilivyoanguka, lakini alionekana kuwa na hali njema.

Watu wenye mavazi ya kijeshi waliokuwa na kanda nyeupe za mkono walikaribia Jeep na kuwaamuru watoke wakiwa wameinua mikono yao. Mmoja, aliyeonekana kuwa mwenye cheo cha juu zaidi, alimgeukia askari-jeshi mmoja na kusema: “Uliambiwa usiwapige raia risasi.” Askari-jeshi huyo alijaribu kujitetea akidai kwamba alisikia mifyatuko ya bunduki akafikiri ilitoka kwenye Jeep.

David alipomtambulisha Rosalía na yeye mwenyewe kuwa Mashahidi wa Yehova, itikio lilikuwa zuri. Alieleza lile alilokuwa akifanya, lakini askari-jeshi walitaka kuwazuia kifungoni bado. Yaonekana, katika alfajiri, sehemu ya jeshi ilikuwa imepindua serikali, na askari-jeshi hawa walikuwa wakitwaa kwa nguvu kituo cha polisi wakati David na Rosalía walipopita katika Jeep.

Rosalía aliudhika sana lakini aliendelea kuwa mtulivu kwa ujasiri huku David alipokuwa akiwasihi wawaachilie. Hatimaye waliruhusiwa waondoke—bila Jeep. Walilazimika kutembea hadi barabara ya karibu na kupata basi ya kwenda kwenye ofisi ya tawi, ambako Rosalía alitibiwa kwenye hospitali ndogo.

Nguvu za Sala

David alijifunza jambo fulani kutokana na ono hilo—usipunguze uzito kamwe wa nguvu za sala yenye bidii, na usisahau kamwe kwamba mara nyingi kujitambulisha mwenyewe kwa ujasiri kuwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova ni ulinzi. Laweza kihalisi kuwa jambo la kweli kwamba “jina la BWANA [Yehova, NW] ni ngome imara; mwenye haki huikimbilia, akawa salama.”—Mithali 15:29; 18:10; Wafilipi 4:6.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 19]

Fotografía de Publicaciones Capriles, Caracas, Venezuelayy

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki