Mkutano wa Kila Mwaka
Oktoba 7, 1995
MKUTANO WA KILA MWAKA wa washiriki wa Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania utafanywa siku ya Oktoba 7, 1995, katika Jumba la Kusanyiko la Mashahidi wa Yehova, 2932 Kennedy Boulevard, Jersey City, New Jersey. Mkutano wa utangulizi wa washirika pekee yao utafanywa saa 3:30 asubuhi, ukifuatwa na mkutano wa ujumla wa kila mwaka saa 4:00 asubuhi.
Washiriki wa Shirika hilo wanapaswa kuijulisha Ofisi ya Mwandishi sasa juu ya badiliko lolote la anwani zao lililotokea mwaka uliopita ili barua zile za kawaida za ujulisho na za uwakilishaji ziweze kuwafikia wakati wa mwezi wa Julai.
Barua za uwakilishaji, watakazopelekewa washiriki pamoja na ujulisho wa mkutano wa kila mwaka, zinapasa kurudishwa ili ziifikie Ofisi ya Mwandishi wa Sosaiti kabla ya Agosti 1. Inampasa kila mshiriki ajaze mambo yote yaliyo katika barua ya wawakilishaji na kuirudisha haraka, akitaarifu kama atakuwapo ama hatakuwapo mkutanoni yeye binafsi. Habari zenye kutajwa katika kila barua ya uwakilishaji zinapasa kuwa wazi, kwa kuwa ndizo zitakazotegemewa katika kujua ni akina nani watakaokuwapo binafsi.
Inatarajiwa kwamba kipindi kizima, kutia ndani mkutano ule rasmi na ripoti mbalimbali, kitamalizwa ifikapo saa 7:00 alasiri au muda mfupi baada ya hapo. Hakutakuwa na kipindi cha alasiri. Kwa sababu nafasi ni ndogo, itawezekana kuingia kwa kuwa na tikiti tu. Hakutakuwa na mpango wa kuunganisha majumba mengine kwa simu ili kuusikia mkutano wa kila mwaka.