Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 6/1 kur. 3-4
  • Je, Wewe ni Mhasiriwa wa Ubaguzi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Wewe ni Mhasiriwa wa Ubaguzi?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Ubaguzi Waweza Kuumiza
  • Ubaguzi Tatizo la Ulimwenguni Pote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Ubaguzi—Je, Umekuathiri?
    Amkeni!—2020
  • Ubaguzi Utakwisha Lini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
  • Chuki na Ubaguzi—Kufichua Mizizi Yake
    Amkeni!—2009
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 6/1 kur. 3-4

Je, Wewe ni Mhasiriwa wa Ubaguzi?

JEURI ya kikabila, ubaguzi wa kijamii, upendeleo, utengaji, na mauaji ya jamii nzima-nzima yana kitu gani kwa upatano? Yote ni matokeo ya mwelekeo wa kibinadamu wenye kuenea sana—ubaguzi!

Ubaguzi ni nini? Ensaiklopedia moja huufafanua kuwa “maoni yanayofanyizwa bila kuchukua wakati au kufikiria ili kuhukumu kwa haki.” Tukiwa binadamu wasiokamilika, sisi huelekea kuwa wenye ubaguzi kwa kadiri fulani. Labda waweza kufikiria juu ya wakati fulani ambapo ulifanya maamuzi bila kuwa na mambo yote ya hakika. Biblia hutofautisha mitazamo hiyo ya kubagua na njia ambayo Yehova Mungu huhukumu. Hiyo husema: “BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.”—1 Samweli 16:7.

Ubaguzi Waweza Kuumiza

Bila shaka kila mtu amepata kuhukumiwa isivyofaa na mtu fulani wakati fulani. (Linganisha Mhubiri 7:21, 22.) Kwa ujumla, sisi sote ni wahasiriwa wa ubaguzi. Hata hivyo, yanapoondolewa haraka, yaelekea mawazo ya kubagua hayatatuumiza au yatatuumiza kidogo tu. Ni kukuza mawazo hayo ambako kwaweza kutokeza madhara. Huko kwaweza kutudanganya kuamini uwongo. Kwa kielelezo, chini ya uvutano wa ubaguzi, watu fulani huamini kikweli kwamba mtu fulani ni mwenye pupa, mvivu, mpumbavu, au mwenye kiburi kwa sababu eti yeye ni wa dini fulani, kabila, au kikundi fulani cha kitaifa.

Katika visa vingi kuhukumu huko kusikofaa huongoza kwenye kutendea wengine bila haki, vibaya, au hata kwa jeuri. Mamilioni ya watu wamepoteza uhai katika machinjo, mauaji ya jamii nzima-nzima, mauaji ya kikabila, na namna nyinginezo za ubaguzi wa kupita kiasi.

Ulimwenguni pote, serikali zimepambana na ubaguzi kwa kuhakikisha kisheria haki isiyoweza kuvunjwa ya uhuru, usalama, na usawa. Ukisoma katiba au vifungu vya sheria ya nchi yako, bila shaka utapata fungu au sahihisho lililobuniwa kulinda haki za wananchi wote, haidhuru ni wa jamii, jinsia, au dini gani. Hata hivyo, ubaguzi na upendeleo zimeenea sana ulimwenguni pote.

Je, wewe ni mhasiriwa wa ubaguzi? Je, umetiwa alama kuwa mwenye pupa, mvivu, mpumbavu, au mwenye kiburi kwa sababu tu ya jamii, umri, jinsia, taifa lako, au itikadi zako za kidini? Je, unanyimwa fursa za elimu ifaayo, kazi ya kuajiriwa, nyumba, na utumishi wa kijamii kwa sababu ya ubaguzi? Ikiwa ndivyo, waweza kukabilije hali?

[Picha katika ukurasa wa 3]

Kukuza ubaguzi akilini huchochea chuki ya kijamii

[Hisani]

Nina Berman/Sipa Press

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki