Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w96 12/15 kur. 3-4
  • Gospeli Kulingana na Wasomi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Gospeli Kulingana na Wasomi
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Maoni ya “Kisomi” juu ya Yesu
  • Zaidi ya Kitaaluma
  • Gospeli—Mjadala Wake Waendelea
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2000
  • Yule Yesu Halisi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2001
  • Vitabu vya Injili Vinategemeka Kadiri Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Kweli Juu ya Yesu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1996
w96 12/15 kur. 3-4

Gospeli Kulingana na Wasomi

“JE! MAKUTANO hao wanasema ya kuwa mimi ni nani?” (Luka 9:18) Yesu aliwauliza hivyo wanafunzi wake karibu mileani mbili zilizopita. Hilo swali lilibishaniwa wakati huo. Laonekana kubishaniwa hata zaidi sasa, hasa wakati wa majira ya Krismasi, ambayo yapaswa kumkazia Yesu. Watu wengi huamini kwamba Yesu alitumwa kutoka mbinguni ili kuwakomboa wanadamu. Je, hilo ndilo unalofikiri?

Wasomi fulani hutokeza maoni mengine. “Wazo la Yesu akiwa mtu aliyefundisha kwamba alikuwa Mwana wa Mungu aliyepaswa kufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu si la kweli kihistoria,” adai Marcus J. Borg, profesa wa dini na utamaduni.

Wasomi wengine wanadai kwamba Yesu halisi alikuwa tofauti na yule tunayesoma juu yake katika Biblia. Wasomi fulani wanaamini kwamba Gospeli zote ziliandikwa miongo minne au zaidi baada ya kifo cha Yesu na kwamba kufikia wakati huo utambulisho wa kweli wa Yesu ulikuwa umeongezewa. Hao wasomi wanadai kwa nguvu kwamba, tatizo halikuwa na kumbukumbu la waandikaji wa Gospeli, bali na fasiri yao. Baada ya kifo cha Yesu wanafunzi walikuja kumwona kwa njia tofauti—kuwa Mwana wa Mungu, Mwokozi, na Mesiya. Watu fulani hudai kwa ujasiri kwamba Yesu alikuwa mwenye hekima aliyekuwa akizurura, mwanamapinduzi wa kijamii. Wasomi wasema kwamba, hiyo ndiyo kweli ya gospeli.

Maoni ya “Kisomi” juu ya Yesu

Ili kulinda maoni yao ya “kisomi,” wachambuzi waonekana kuwa na hamu ya kuachia mbali chochote juu ya Yesu ambacho chaonekana kuwa chenye nguvu zinazopita za asili. Kwa kielelezo, baadhi yao husema kwamba kule kuzaliwa na bikira kulikuwa kufunika tu uana-haramu wa Yesu. Wengine wanakataa unabii mbalimbali wa Yesu kuhusu uharibifu wa Yerusalemu, wakisisitiza kwamba huo uliongezwa katika Gospeli baada ya “utimizo” wao. Baadhi yao hata wanasema kwamba maponyo ya Yesu yalikuwa ya kisaikosomatiki tu—yaliyohusisha akili na mwili. Je, wayaona maneno hayo kuwa ya kweli au ya upuzi?

Wasomi fulani hata hudai kwamba wanafunzi wa Yesu walitunga ufufuo wake ili harakati yao isipate kuangamia. Wasomi wanasababu kwamba kwa vyovyote vile, wafuasi wa Yesu hawakuwa na nguvu bila yeye, kwa hiyo wakatunga historia katika maandishi yao ili kurejesha fungu lenye kutokeza la Yesu. Kwa msingi, wasomi walikuwa wakisema kwamba, ni Ukristo, wala si Kristo, ndio uliofufuliwa. Ikiwa hilo laonekana kuwa kupotoka kwa wasomi, vipi juu ya pendekezo la mwanatheolojia Barbara Thiering kwamba Yesu hakufishwa kamwe? Yeye aamini kwamba Yesu alisalimika kutundikwa kwake mtini kisha akaendelea kuishi na kuoa mara mbili na kuzaa watoto watatu.

Madai yote hayo yenye nguvu humshusha Yesu kufikia kiwango pekee ambacho wasomi wengi watakubali: kile cha kuwa mtu mwenye hekima, Myahudi wa kandokando, mwanamapinduzi wa kijamii—chochote isipokuwa Mwana wa Mungu, aliyekuja “kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.”—Mathayo 20:28.

Wakati huu wa mwaka, huenda ukawa umesoma sehemu mbalimbali za Gospeli, kama ile sehemu juu ya kuzaliwa kwa Yesu katika hori. Au huenda ukawa umesikia hizo kanisani. Je, wewe uliyakubali masimulizi ya Gospeli kuwa yenye thamani na yenye kuaminika? Basi chunguza hali hii yenye kushtua. Katika iitwayo isivyofaa Semina ya Yesu, kikundi cha wasomi kimekutana mara mbili kila mwaka tangu 1985 ili kuamua uasilia wa maneno ya Yesu. Je, kweli Yesu alisema yale ambayo Biblia yamhesabia? Washiriki wa hiyo semina walipigia kura kila mmojawapo wa usemi wa Yesu kwa kutumia shanga zenye rangi. Ushanga mwekundu ulimaanisha kwamba taarifa kwa hakika ilisemwa na Yesu; ushanga mwekundu-mweupe ulimaanisha kwamba yawezekana Yesu alisema hilo; ushanga wa kijivu ulionyesha shaka; na ushanga mweusi ulidokeza kwamba si ya kweli.

Huenda ukahangaishwa kujua kwamba ile Semina ya Yesu imetangaza kwamba asilimia 82 ya maneno aliyohesabiwa Yesu yawezekana kuwa hayakutamkwa naye. Ni nukuu moja tu kutoka katika Gospeli ya Marko lililoonwa kuwa lenye kutumainika. Gospeli ya Luka ilisemwa kuwa imejaa propaganda sana hivi kwamba “haiwezi kurekebishwa.” Mistari yote ya Gospeli ya Yohana isipokuwa mitatu ilipata kura ya ushanga mweusi, kudokeza kwamba si ya kweli, na kile kisehemu kilichosalia kilipata ushanga wa kijivu wa shaka.

Zaidi ya Kitaaluma

Je, wakubaliana na wasomi? Je, wao wanatutolea wonyesho sahihi zaidi juu ya Yesu kuliko upatikanao katika Biblia? Maswali hayo yanahusisha mengi zaidi ya jadiliano la kisomi. Wakati huu mwakani, huenda ukakumbushwa kwamba, kulingana na Biblia, Mungu alimtuma Yesu “ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”—Yohana 3:16.

Ikiwa Yesu alikuwa mtu mwenye hekima aliyezurura tu ambaye huenda tukajua machache juu yake, hakungekuwa na sababu ya ‘kumwamini.’ Kwa upande mwingine, ikiwa wonyesho wa Biblia juu ya Yesu ni wa kweli, wokovu wetu wa milele unahusika. Kwa hiyo, twahitaji kujua—je, Biblia ina kweli juu ya Yesu?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki