Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 2/15 kur. 19-20
  • Elimu-Maadili ya Kibiolojia na Upasuaji Usiotumia Damu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Elimu-Maadili ya Kibiolojia na Upasuaji Usiotumia Damu
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kubadilishana Maoni
  • Uhitaji Unaoongezeka wa Tiba na Upasuaji Bila Damu
    Amkeni!—2000
  • Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
    Mashahidi wa Yehova na Suala la Damu
  • Ingawa Nilikuwa Kipofu, Niliweza Kuona!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Madaktari Wafikiria Upya Upasuaji Bila Damu
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 2/15 kur. 19-20

Elimu-Maadili ya Kibiolojia na Upasuaji Usiotumia Damu

MIAKA ya majuzi imeona maendeleo yasiyo na kifani katika uwanja wa tiba. Hata hivyo, huku matatizo ya kitiba yakisuluhishwa, baadhi ya maendeleo ya kitiba yametokeza matatizo ya kielimu-maadili.

Madaktari wanalazimika kufikiria kwa uzito mambo ya kutatanisha kama vile: Je, matibabu ya kitiba ya kutumia nguvu yaachwe nyakati nyingine ili mgonjwa aweze kufa akiwa na adhama? Je, daktari apaswa kugeuza uamuzi wa mgonjwa ikiwa ahisi ni kwa faida ya mgonjwa? Utunzaji wa afya wapaswa kugawanywaje kwa haki matibabu ya gharama kubwa yasipopatikana kwa ajili ya kila mtu?

Masuala tata kama hayo yamekazia fikira uwanja wa kitiba unaoitwa elimu-maadili ya kibiolojia. Taaluma hiyo hukusudiwa kuwasaidia madaktari na wanasayansi kushughulika na madokezo ya kielimu-maadili ya utafiti wa kibiolojia na maendeleo ya kitiba. Kwa kuwa mengi ya maamuzi yaliyo magumu zaidi hutokea hospitalini, hospitali nyingi zimeanzisha halmashauri za elimu-maadili ya kibiolojia. Kwa kawaida washiriki wa halmashauri hizo—kutia na madaktari na wanasheria—huhudhuria semina mbalimbali juu ya elimu-maadili ya kibiolojia, ambapo matatizo ya kielimu-maadili katika tiba huchanganuliwa.

Maswali kadhaa ambayo huzushwa mara nyingi kwenye semina hizo ni: Madaktari wataheshimu kwa kiwango gani itikadi za Mashahidi wa Yehova ambao, hasa kwa sababu za kidini, hukataa kutiwa damu mishipani? Je, daktari amtie damu mishipani mgonjwa dhidi ya mapenzi ya huyo mgonjwa ikiwa hilo laonekana kuwa “lafaa” kitiba? Je, ingepatana na elimu-maadili kufanya hivyo bila mgonjwa kujua, kana kwamba ‘asichojua mgonjwa hakitamdhuru’?

Ili kushughulikia masuala hayo ifaavyo, madaktari wanahitaji kuwa na lengo la kuelewa maoni ya Mashahidi. Kwa upande wao, Mashahidi wa Yehova wana hamu ya kufafanua msimamo wao kwa madaktari, kwa kutambua kuwa uelewevu kati yao na madaktari waweza kuepusha mzozo.

Kubadilishana Maoni

Profesa Diego Gracia, Mhispania maarufu aliye mtaalamu wa elimu-maadili ya kibiolojia, alitaka darasa lake liwe na mazungumzo hayo. “Yafaa tu kwamba nyinyi [Mashahidi wa Yehova] mpewe fursa ya kueleza mahangaiko yenu . . . kwa sababu ya magumu ambayo mmekuwa nayo kuhusiana na utiaji-damu mishipani,” profesa huyo akasema.

Hivyo, Juni 5, 1996, wawakilishi watatu wa Mashahidi wa Yehova walialikwa kwenda Chuo Kikuu cha Complutense huko Madrid, Hispania, wakafafanue maoni yao. Madaktari na wataalamu wengine 40 walikuwapo.

Baada ya hao Mashahidi kutoa utoaji mfupi, kipindi cha maswali kikaanza. Wote waliokuwapo walikubaliana kwamba mgonjwa aliye mtu mzima apaswa kuwa na haki ya kukataa matibabu mahususi. Hilo darasa lilikubali pia kwamba mgonjwa yeyote hapaswi kutiwa damu mishipani bila ya idhini yake baada ya kuarifiwa. Hata hivyo sehemu nyingine za msimamo wa Mashahidi ziliwahangaisha.

Swali moja lilihusu fedha. Nyakati nyingine upasuaji usiotumia damu hutia ndani vifaa vya pekee, kama vile upasuaji wa leza, na vilevile dawa zenye gharama kubwa, kama vile erithropoietini, zinazotumiwa kuchochea kutokezwa kwa chembe nyekundu za damu. Daktari mmoja alijiuliza ikiwa kwa kukataa njia ya badala iliyo ya gharama ndogo zaidi (damu ya aina ileile), Mashahidi wanaweza kuwa wakitarajia huduma za afya za umma ziwape mapendeleo ya pekee.

Huku akitambua kwamba fedha ni jambo ambalo madaktari lazima wafikirie, mwakilishi Shahidi alirejezea uchunguzi mbalimbali uliochapishwa unaochanganua gharama zisizoonekana waziwazi za utiaji-damu wa aina ileile mishipani. Hizo hutia ndani gharama za kutibu hali tata zinazohusianishwa na utiaji-damu mishipani, na pia kupotezwa kwa mshahara kutokezwako na magonjwa yanayosababishwa na hali hizo tata. Alinukuu uchunguzi wa ujumla kutoka Marekani ulioonyesha kwamba kizio cha wastani cha damu, ingawa mwanzoni uligharimu dola 250 tu, kwa hakika ulitokeza gharama za dola zaidi ya 1,300—zaidi ya mara tano ya kiasi cha awali. Kwa sababu hiyo, alionyesha kwamba, mambo yote yanapofikiriwa, upasuaji usiotumia damu huwa na matokeo mazuri kiuchumi. Zaidi ya hayo, sehemu kubwa ya ile iitwayo gharama ya ziada ya upasuaji usiotumia damu ni vifaa ambavyo vyaweza kutumiwa tena.

Swali jingine lililokuwa akilini mwa madaktari kadhaa lilihusu msongo kutoka kwa kutaniko. Ingekuwaje, walijiuliza, ikiwa Shahidi angeyumbayumba na kukubali utiaji-damu mishipani? Je, angetengwa na jumuiya ya Mashahidi?

Itikio lingetegemea hali yenyewe, kwa maana kwa hakika kutotii amri ya Mungu ni jambo zito, jambo la kuchunguzwa na wazee wa kutaniko. Mashahidi wangependa kusaidia mtu yeyote ambaye amepitia hali yenye kufadhaisha ya upasuaji wenye kuhatarisha uhai na ambaye amekubali utiaji-damu mishipani. Bila shaka Shahidi huyo angehisi vibaya sana na angehangaikia uhusiano wake pamoja na Mungu. Huenda mtu kama huyo akahitaji msaada na uelewevu. Kwa kuwa msingi wa Ukristo ni upendo, wazee wangetaka, kama ilivyo katika visa vyote vya kihukumu, kusawazisha uthabiti na rehema.—Mathayo 9:12, 13; Yohana 7:24.

“Je, hamtachunguza upya msimamo wenu wa elimu-maadili karibuni?” akauliza profesa mmoja wa elimu-maadili ya kibiolojia, aliyekuwa akizuru toka Marekani. “Dini nyingine zimefanya hivyo katika miaka ya juzijuzi.”

Msimamo wa Mashahidi kuhusu utakatifu wa damu ni itikadi ya kimafundisho wala si maoni ya kielimu-maadili yawezayo kuchanganuliwa pindi kwa pindi, akaambiwa. Amri ya wazi ya Kibiblia hairuhusu kuridhiana kokote. (Matendo 15:28, 29) Kuvunja sheria hiyo ya kimungu kungekuwa jambo lisilokubalika kwa Shahidi kama vile kuruhusu ibada ya sanamu au uasherati.

Mashahidi wa Yehova huthamini sana utayari wa madaktari—kama wale waliokuwapo kwenye semina ya elimu-maadili ya kibiolojia huko Madrid—wa kustahi uamuzi wao wa kutafuta matibabu ya badala yanayopatana na masadikisho yao yanayotegemea Biblia. Bila shaka, elimu-maadili ya kibiolojia itakuwa na fungu muhimu katika kuboresha mahusiano kati ya daktari na mgonjwa na kuendeleza staha kubwa zaidi kwa mapenzi ya mgonjwa.

Kama vile tabibu maarufu Mhispania anavyoripotiwa kuwa alisema, madaktari wapaswa kukumbuka sikuzote kuwa wao “wanafanya kazi na vifaa visivyo vikamilifu na njia ziwezazo kuwa na makosa.” Kwa hiyo, wao wanahitaji ule “usadikisho kwamba upendo wapaswa sikuzote kufikia mahali ambapo ujuzi hauwezi kufika.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki