Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w97 7/15 uku. 3
  • Waionaje Dhambi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Waionaje Dhambi?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Wakati Dhambi Haitakuwapo Tena
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • Dhambi—Ina Ubaya?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
  • Kwa Nini Maoni ya Watu Kuhusu Dhambi Yamebadilika?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Dhambi
    Ufahamu wa Kina wa Maandiko
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
w97 7/15 uku. 3

Waionaje Dhambi?

“HAKUNA dhambi ndani yako, hakuna taabu ndani yako; wewe ndiwe ghala ya uwezo wote.” Mwanafalsafa maarufu wa Kihindu Vivekananda alitoa taarifa hiyo alipokuwa akifafanua fungu fulani kutoka kitabu kitakatifu cha Wahindu, kiitwacho Bhagavad Gita. Akitaja falsafa ya Vedanta, yeye adai hivi: “Kosa lililo kubwa zaidi ya yote ni kusema kwamba wewe u dhaifu, kwamba wewe ni mtenda-dhambi.”a

Je, hata hivyo, ni kweli, kwamba hakuna dhambi katika mwanadamu? Na ni nini, ikiwa kuna chochote, ambacho mtu hurithi, wakati wa kuzaliwa? “Vitabia vya kimwili [tu] ndivyo vinaamuliwa na urithi-tabia,” asema Nikhilananda, mwalimu wa Kihindu. Tabia nyingine zinaamuliwa na “matendo ya mtu katika maisha yake mbalimbali ya hapo awali.” Kulingana na Vivekananda, “wewe ndiwe mfanyiza wa mambo yatakayokupata hatimaye.” Dini ya Hindu haifundishi chochote juu ya dhambi iliyorithiwa.

Dhana ya dhambi iliyorithiwa pia haipo miongoni mwa Wazoroasta, Washinto, Wakonfyushasi na Wabuddha. Hata katika dini za Kiyahudi na Ukristo, ambazo zimefundisha kidesturi juu ya dhambi iliyorithiwa, mtazamo wa watu kuelekea dhambi unabadilika. Watu zaidi na zaidi leo hawajifikirii kuwa wenye dhambi.

“Utambuzi wa kisasa hautii moyo kujishutumu kiadili; hasa, hautii moyo kujishutumu kibinafsi,” asema mwanatheolojia Cornelius Plantinga, Jr. Makanisa ya Jumuiya ya Wakristo ni ya kulaumiwa kwa kiasi fulani kuhusiana na kupunguza uzito wa dhambi. “Usiende kanisani ikiwa wataka kusikia juu ya dhambi,” asema kasisi wa Chuo Kikuu cha Duke. Na kulingana na Plantinga, makanisa kwa kawaida husema juu ya dhambi kwa kuhusiana tu na masuala ya kijamii.

Kwa kukiri wazi, ole za kijamii za siku hizi ni nyingi. Jeuri, uhalifu, vita, zogo za kikabila, matumizi mabaya ya dawa, ukosefu wa ufuatiaji haki, ukandamizaji, na jeuri dhidi ya watoto, ni mambo yenye kuenea pote. Kwa hakika, karne ya 20 imetajwa kuwa mojawapo ya karne zenye umwagikaji mwingi zaidi wa damu ambayo jamii ya binadamu imepata kujua. Ongeza kwa mambo hayo maumivu na kuteseka ambako hutokana na ugonjwa, uzee, na kifo. Nani ambaye hatamani kukombolewa na matatizo makubwa mno yaliyomo ulimwenguni leo?

Basi, maoni yako ni nini juu ya dhambi? Je, dhambi inarithiwa? Je, kweli tutapata kuwa huru na maumivu na mateso? Makala ifuatayo itazungumzia maswali hayo.

[Maelezo ya Chini]

a Falsafa ya Vedanta inategemea Upanishads, vitabu ambavyo hutokea mwishoni mwa maandiko ya Kihindu, yaitwayo Vedas.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki