Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w98 6/1 kur. 3-4
  • Jihadhari na Wadhihaki!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jihadhari na Wadhihaki!
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Kila Kitu Bado Kiko Vilevile?
  • Weka Siku ya Yehova Karibu Akilini
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1997
  • “Siku Kuu ya Yehova Iko Karibu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Ngoja kwa Subira
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Siku za Mwisho—Za Nini?
    Amkeni!—2008
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
w98 6/1 kur. 3-4

Jihadhari na Wadhihaki!

Leo, matabiri ni mengi, na biashara ya udadisi wa mambo juu ya wakati ujao inasitawi. “Mwaka wa 2000 ukaribiapo zaidi,” lasema gazeti The Daily Telegraph la London, “jambo fulani lisilo la kawaida na ambalo bado si lisilotarajiwa kabisa, linatukia. Maelfu ya watu ulimwenguni pote wanaona maono ya kiajabu na yenye kuogofya juu ya wakati ujao.” Kwa watazamaji wengi, upendezi huo mkubwa katika wakati ujao ni kurudia tu mabadiliko yaliyotumainiwa hapo awali ambayo hayakutokea.

MAGARI ya kukokotwa kwa farasi yalipoongezeka katika karne ya 19, mwanamume mmoja alitabiri kwamba majiji ya Ulaya hatimaye yangejawa na mbolea ya farasi. Bila shaka, utabiri wake ulithibitika kuwa usio wa kweli. Hivyo, linapokazia jinsi ambavyo matabiri hukosa kuwa kweli, gazeti The Times la London lilitaarifu hivi: “Wakati ujao ni mzigo tu wa mbolea ya farasi.”

Wengine huwadhihaki wale wenye kuona hatari iliyoko mbele. Kwa mfano, profesa mmoja wa biashara kwenye chuo kikuu cha Marekani aliwatolea mwito wale wenye kuonya juu ya kuharibiwa kwa mazingira waseme kama huo mwelekeo ungekuwa mbaya zaidi. Kama ilivyoripotiwa katika gazeti la New Scientist, huyo profesa adai kwamba “ubora wa maisha yetu unaendelea kuwa mzuri zaidi na utaendelea hivyo kwa wakati usio dhahiri.”

Katikati ya vurugu ya madai na madai ya kukinza, watu wengi huamini kwamba, kimsingi kila kitu kitabaki bila kubadilika. Wakidhihaki wazo lolote la uingiliaji-kati wa kimungu katika mambo ya kibinadamu, wao huonyesha mtazamo kama ule wa wadhihaki katika karne ya kwanza W.K.

Je, Kila Kitu Bado Kiko Vilevile?

Barua ya pili ya mtume Mkristo Petro iliyopuliziwa, ambayo iliandikwa wapata mwaka wa 64 W.K., ilionya hivi: “Katika siku za mwisho watakuja wadhihaki pamoja na dhihaka zao, wakiendelea kulingana na tamaa zao wenyewe.”—2 Petro 3:3.

Wadhihaki hutafuta kufanya kitu wanachodhihaki kionekane kuwa chenye kuchekesha. Mtu ambaye ashindwa na dhihaka huenda akawa anaangukia mtego wa ubinafsi, kwa sababu mara nyingi mdhihaki hutaka wale wenye kusikiliza wakubaliane na maoni yake. Labda baadhi ya wadhihaki ambao Petro alionya dhidi yao walikuwa hivyo, “wakiendelea kulingana na tamaa zao wenyewe.” Katika kuwatahadharisha wasomaji wake, mtume alitumia namna ya usemi wenye mkazo. Alionya juu ya kuja kwa “wadhihaki pamoja na dhihaka zao.”  

Wadhihaki hao wa karne ya kwanza walishuku uhalisi wa ‘kuwapo kwa Kristo kulikoahidiwa,’ wakiuliza hivi: “Kuko wapi kuwapo kwake huku kulikoahidiwa? Kwani, kutoka siku baba zetu wa zamani walipolala katika kifo, mambo yote yanaendelea sawasawa kabisa kama kutoka mwanzo wa kuumba.” (2 Petro 3:4) Hali ilionekana hivyo kwao. Hata hivyo, huko nyuma mwaka wa 33 W.K., Yesu alikuwa ametabiri msiba mkubwa ambao ungepata jiji la Yerusalemu. “Siku zitakuja juu yako,” akatangaza, “wakati maadui wako watakapojenga kukuzunguka wewe boma lenye miti iliyochongoka nao watakuzunguka na kukutaabisha kutoka kila upande, nao watabwaga kwenye ardhi wewe na watoto wako walio ndani yako, nao hawataacha jiwe juu ya jiwe katika wewe.” Waliodhihaki onyo hilo walikosea kama nini! Mwaka wa 70 W.K., majeshi ya Roma yalizingira Yerusalemu na kuharibu jiji, na wakazi wake wengi wakapoteza maisha yao. Kwa nini walio wengi wa wakazi wa hilo jiji hawakuwa tayari kwa msiba huo? Kwa sababu hawakuwa wamefahamu kwamba Mungu alikuwa amewakagua kupitia Mwana wake, Yesu.—Luka 19:43, 44.

Mtume Petro hurejezea uingiliaji-kati wa Mungu Mweza Yote wakati ujao. “Siku ya Yehova itakuja kama mwizi,” Petro aonya. (2 Petro 3:10) Wakati huo Mungu atawaondoa tufeni pote watu wasiomwogopa na kuwaacha wale wenye kuhukumiwa kuwa waadilifu. Kama vile jarida hili limeeleza mara nyingi, “kuwapo” kwa Kristo Yesu kulianza mwaka wa 1914. Lakini kuchukua hatua akiwa Mfishaji wa Mungu ili aondoe uovu bado ni wakati ujao. Kwa sababu hiyo, onyo la mtume la kujihadhari na wadhihaki latumika sasa kwa hima kubwa zaidi.

Huenda ukawa tayari umengoja kwa muda mrefu uingiliaji-kati wa kimungu katika mambo ya mwanadamu. Ni nini kitakachokusaidia uendelee kungoja kwa subira bila kupata kuwa windo la wadhihaki? Tafadhali endelea kusoma.

[Blabu katika ukurasa wa 4]

“Siku zitakuja juu yako wakati maadui wako . . . watakuzunguka na kukutaabisha kutoka kila upande, . . . nao hawataacha jiwe juu ya jiwe katika wewe.” Hilo halikuwa onyo la kudhihakiwa. Majeshi ya Roma yaliharibu Yerusalemu, na watu wengi walipoteza maisha yao.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki