Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w04 6/15 uku. 3
  • Matatizo ya Kulea Watoto Leo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Matatizo ya Kulea Watoto Leo
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
  • Habari Zinazolingana
  • Kulea Watoto tangu Uchanga
    Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha
  • Zoeza Mtoto Wako Tangu Utoto Mchanga Sana
    Siri ya Furaha ya Familia
  • Wazazi, Fikieni Moyo wa Mtoto Wenu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Jinsi ya Kuwalinda Watoto Wako
    Amkeni!—2007
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2004
w04 6/15 uku. 3

Matatizo ya Kulea Watoto Leo

NI JIONI sana, na mwenye mkahawa anajitayarisha kufunga ili kwenda nyumbani. Ndipo wanawake wawili na mtoto wanapoingia na kuagiza chakula. Kwa kuwa amechoka sana, mwenye mkahawa huo anataka kuwaambia amefunga kazi, lakini anaamua kuwahudumia. Wanawake hao wawili wanapoendelea kula na kuzungumza, mtoto anakimbia huku na huku ndani ya mkahawa, akiangusha biskuti sakafuni kisha kuziponda-ponda kwa miguu. Badala ya kumkataza kufanya hivyo, mamake anatabasamu tu. Mwishowe, wateja hao wanapoondoka, mwenye mkahawa ambaye amechoka analazimika kusafisha sakafu hiyo.

Inaelekea unajua kwamba hali hii iliyo halisi huonyesha kuwa, katika familia nyingi watoto hawazoezwi vizuri. Kuna sababu mbalimbali za kutofanya hivyo. Wazazi fulani huacha watoto wao wafanye watakalo, wakifikiri kwamba watoto wanapaswa kulelewa katika mazingira yenye uhuru. Au huenda kwa sababu ya shughuli nyingi, wazazi wasiwe na wakati wa kuwatunza watoto wao kwa uangalifu na kuwapa mazoezi yanayohitajiwa. Wazazi wengine hufikiri kwamba jambo lililo muhimu zaidi ni elimu ya mtoto wao, hivyo wao humpa mtoto uhuru usio na mipaka mradi tu anafanya vizuri shuleni na anakubaliwa kujiunga na chuo maarufu.

Lakini, wengine husema kwamba maadili ya wazazi na jamii kwa ujumla yanahitaji kurekebishwa. Wanatoa hoja kwamba watoto wanafanya uhalifu wa kila aina, nayo jeuri shuleni inaendelea kuongezeka siku baada ya siku. Kwa hiyo, mkuu mmoja wa shule fulani ya sekondari huko Seoul, Jamhuri ya Korea, alikazia kwamba ni muhimu kuwazoeza watoto kuwa na tabia nzuri. Alisema: “Kusitawisha tabia nzuri hutangulia kupata ujuzi.”

Wazazi wengi wanaotaka watoto wao waende chuoni na wafanikiwe maishani, hupuuza maonyo. Ikiwa wewe ni mzazi, unataka mtoto wako awe mtu wa aina gani? Unataka awe mtu mzima mwenye maadili na mwenye kutegemeka? Je, unataka awe mtu ambaye huwajali wengine, hubadilikana na hali, na mwenye maoni yafaayo? Ikiwa ndivyo, tafadhali chunguza makala ifuatayo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki