Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w06 7/15 uku. 3
  • Ufalme wa Mungu Ni Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ufalme wa Mungu Ni Nini?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Habari Zinazolingana
  • Dhambi ya Kwanza Ilikuwa Nini?
    Amkeni!—2006
  • Maisha Yalikuwaje Katika Paradiso?
    Msikilize Mungu Uishi Milele
  • Paradiso Yapotea
    Biblia—Ina Ujumbe Gani?
  • Kwa Nini Uovu Unaendelea
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2007
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
w06 7/15 uku. 3

Ufalme wa Mungu Ni Nini?

MWANADAMU alipatwa na msiba mkubwa sana mwanzoni mwa historia ya wanadamu! Malaika mmoja aliasi mamlaka ya Yule aliyemuumba. Mwasi huyo alimshawishi mwanamke wa kwanza, Hawa, ale tunda lililokatazwa. Akimrejelea Hawa na mume wake, Adamu, malaika huyo alisema: “Hakika hamtakufa. Kwa maana Mungu anajua kwamba siku ileile mtakapokula matunda yake macho yenu yatafunguliwa, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.” (Mwanzo 2:16, 17; 3:1-5) Malaika huyo mwasi anaitwa Ibilisi na Shetani.—Ufunuo 12:9.

Je, Hawa alimsikiliza Shetani? Biblia inatuambia hivi: “Mwanamke akaona kwamba mti huo ulikuwa mzuri kwa chakula na kwamba ulikuwa kitu cha kutamanika kwa macho, ndiyo, mti huo ulikuwa wenye kupendeza kuutazama. Kwa hiyo akaanza kuchukua kati ya matunda yake akala. Baadaye akampa mume wake pia alipokuwa pamoja naye, naye akaanza kula.” (Mwanzo 3:6) Naam, wenzi hao wa kwanza, Adamu na Hawa, wakajiunga na Shetani katika uasi. Hivyo, wakapoteza Paradiso nao wakawapotezea watoto wao Paradiso pia. Watoto ambao wangezaliwa wakiwa wakamilifu na wakiwa na tumaini la kuishi milele, walirithi dhambi na kifo.—Waroma 5:12.

Yehova Mungu, Mtawala wa ulimwengu wote alifanyaje? Aliamua kuandaa njia ya kusamehe dhambi. (Waroma 5:8) Pia, Yehova Mungu alianzisha serikali inayoshughulikia tatizo hilo. Serikali hiyo inaitwa “ufalme wa Mungu.” (Luka 21:31) Ufalme huo ambao ulianzishwa ili kutetea utawala wa Mungu juu ya ulimwengu wote una kusudi hususa.

Ufalme wa Mungu una kusudi gani? Baadhi ya sehemu zake ni gani, na zinalinganaje na utawala wa wanadamu? Ufalme huo ungeanza kutawala wakati gani? Maswali hayo yatajibiwa katika makala inayofuata.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki