Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w06 8/1 kur. 3-4
  • Haki ya Binadamu ya Kuheshimiwa Hukandamizwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Haki ya Binadamu ya Kuheshimiwa Hukandamizwa
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Maana ya Heshima ya Binadamu
  • Je, Wewe Wastahi Adhama Yao?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1998
  • Mheshimu Yehova kwa Kuonyesha Heshima
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2008
  • Je! Wewe Huwaheshimu Wengine Utoapo Shauri?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Wanadamu Wote Wanaweza Kuheshimiwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2006
w06 8/1 kur. 3-4

Haki ya Binadamu ya Kuheshimiwa Hukandamizwa

“Kila jambo lililotendeka kambini lilitufanya tuhisi kwamba tumedharauliwa na kukandamizwa.”—MAGDALENA KUSSEROW REUTER, ALIYEOKOKA KAMBI YA MATESO YA NAZI.

INGAWA kulikuwa na ukatili mwingi katika kambi za mateso za utawala wa Nazi wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu, huo haukuwa mwanzo wala mwisho wa ukandamizaji wa heshima ya binadamu. Iwe tunachunguza mambo ya kale au ya sasa, jambo hili linaonekana wazi: Kwa muda mrefu, watu wengi ‘wamedharauliwa na kukandamizwa.’

Hata hivyo, kukandamizwa kwa heshima ya binadamu hakuhusishi tu matendo ya kinyama ambayo yamewahi kufanywa. Mara nyingi matendo hayo hufanywa kwa njia zisizo wazi. Fikiria mtoto anayedhihakiwa kwa sababu ana kasoro fulani za mwili. Au mhamiaji anayedhihakiwa kwa sababu ya desturi fulani za “kigeni.” Au mtu fulani anayebaguliwa kwa sababu ya rangi au taifa lake. Huenda wale wanaowadhihaki wakachukulia mambo hayo kuwa mzaha, lakini wale wanaodhihakiwa hawayaoni kuwa mambo ya kuchekesha kwa kuwa yanawaumiza na kuwaaibisha.—Methali 26:18, 19.

Maana ya Heshima ya Binadamu

Kamusi moja inafafanua heshima kuwa ‘sifa au hali ya kuwa mwenye thamani, kustahiwa, au kuthaminiwa.’ Kwa hiyo, heshima ya binadamu inatia ndani jinsi tunavyojiona na jinsi wengine wanavyotuona. Ingawa kuna mambo ambayo yanaweza kuathiri jinsi tunavyojiona, jinsi wengine wanavyotuona au kututendea hutufanya tuhisi kwamba tunathaminiwa maishani.

Katika kila jamii kuna maskini, kuna watu wasio na uwezo, na wanyonge. Hata hivyo, kuwa katika hali hiyo hakumpunguzii mtu heshima. Mtazamo na matendo ya wengine ndiyo yanayoweza kumvunjia mtu heshima. Inasikitisha kwamba mara nyingi watu wa hali ya chini ndio wanaodharauliwa. Mara nyingi sana tunasikia maneno kama vile “wewe ni bure kabisa” au “hufai kitu” yakitumiwa kuwatukana wazee, maskini, au watu wenye ugonjwa wa akili au walemavu!

Kwa nini watu hawaheshimiani? Je, haki ya msingi ya kuheshimiwa itatimizwa? Makala inayofuata itatoa jibu lenye kuridhisha kutoka kwa Neno la Mungu, Biblia.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki