Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w11 2/1 uku. 27
  • Je, Mashahidi wa Yehova Wanakubali Matibabu?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Mashahidi wa Yehova Wanakubali Matibabu?
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Mashahidi wa Yehova Hukubali Matibabu?
    Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi Kuhusu Mashahidi wa Yehova
  • Uchaguzi Wako wa Matibabu—Je, Ni Muhimu?
    Amkeni!—2001
  • Je, Mkristo Anaweza Kukubali Matibabu?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Je, Mashahidi wa Yehova Wanapinga Kupewa Chanjo?
    Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi Kuhusu Mashahidi wa Yehova
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
w11 2/1 uku. 27

Wasomaji Wetu Wanauliza . . .

Je, Mashahidi wa Yehova Wanakubali Matibabu?

▪ Yesu alisema kwamba “watu wenye afya hawahitaji tabibu, bali wenye kuugua ndio wanaomhitaji.” (Mathayo 9:12) Hivyo, alikuwa akionyesha kwamba si kosa kulingana na Biblia kutafuta msaada kutoka kwa wataalamu wa tiba. Hivyo, Mashahidi wa Yehova hukubali dawa na matibabu bila shida. Wanataka kuwa na afya nzuri na maisha marefu. Kwa kweli, kama Mkristo wa karne ya kwanza, Luka, baadhi ya Mashahidi wa Yehova ni madaktari.—Wakolosai 4:14.

Hata hivyo, Mashahidi wa Yehova hawakubali matibabu yanayopingana na kanuni za Biblia. Kwa mfano, hawakubali kutiwa damu, kwa sababu Biblia inazuia kutumia damu kutibu mwili. (Mwanzo 9:4; Mambo ya Walawi 17:1-14; Matendo 15:28, 29) Neno la Mungu pia linakataza matibabu yanayotia ndani kutumia “nguvu za uchawi,” au kuwasiliana na pepo.—Isaya 1:13; Wagalatia 5:19-21.

Wataalamu wengi wa tiba hutoa matibabu ambayo hayapingani na kanuni za Biblia. Mara nyingi matibabu ya aina hiyo, ambayo wengi wa Mashahidi huyakubali, ni bora zaidi yakilinganishwa na yale yaliyo kinyume cha matakwa ya Mungu.

Kwa kweli, watu wana maoni mbalimbali kuhusu afya. Matibabu yanayoweza kumfaa mtu mmoja huenda yasimsaidie mtu mwingine. Kwa hiyo, watu wanaotafuta vipimo na matibabu sahihi ya magonjwa yao wanaweza kutafuta maoni ya madaktari tofauti-tofauti.—Methali 14:15.

Si kila Shahidi atachagua matibabu yaleyale. Neno la Mungu linawaruhusu Wakristo watumie dhamiri zao ikiwa hakuna kanuni ya Biblia inayovunjwa. (Waroma 14:2-4) Hivyo basi, kila mtu anapaswa kuchunguza matibabu yanayopendekezwa na kuhakikisha kwamba hayapingani na dhamiri yake iliyozoezwa na Biblia.—Wagalatia 6:5; Waebrania 5:14.

Shahidi atafikiria kila uamuzi anaofanya kama vile dereva afanyavyo anapofika sehemu ya barabara ambapo magari mengi yanapishana. Ikiwa dereva huyo atayafuata tu magari yaliyo mbele yake na kuvuka sehemu hiyo bila kupunguza mwendo, anaweza kusababisha uharibifu mkubwa. Dereva mwenye busara atapunguza mwendo na pia kukadiria mwendo wa magari mengine kabla ya kuvuka. Vivyo hivyo, Mashahidi hawafanyi maamuzi yanayohusu matibabu haraka-haraka, wala hawafuati maoni ya watu wengine bila kufikiri. Badala yake, wanafikiria aina ya matibabu wanayoweza kuchagua na kuchunguza kanuni za Biblia kabla ya kufanya uamuzi.

Kwa kweli, Mashahidi wa Yehova wanathamini sana bidii na kujitoa kwa wale wanaotoa huduma za afya. Na pia, wanafurahia sana wataalamu hao wanapowasaidia kupata nafuu kutokana na magonjwa yao.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki