Kujifunza Kutokana na Vidio The Bible—Accurate History, Reliable Prophecy
Baada ya kutazama vidio hiyo, je, unaweza kujibu maswali haya? (1) Ni nani aliye Chanzo cha habari ya Biblia yenye kutegemeka? (Dan. 2:28) (2) Biblia yaelezaje kwa usahihi Misri ya kale, na unabii ulioandikwa kwenye Isaya 19:3, 4 ulitimizwaje? (3) Akiolojia imethibitishaje simulizi la Biblia la Waashuru, wafalme wake, na mwisho wa Ashuru? (Nah. 3:1, 7, 13) (4) Ni unabii gani mbalimbali unaohusu Babiloni ambao umethibitika kuwa wenye kutegemeka? (5) Umedi na Uajemi uliathirije watu wa Mungu? (6) Danieli 8:5, 8 lilitimizwaje, na unabii huo ulikuwa umetabiriwa mapema kadiri gani? (7) Yesu alithibitikaje kuwa Mesiya wa kweli? (8) Ni serikali zipi za kisiasa za kisasa ambazo zatimiza unabii mbalimbali unaopatikana kwenye Ufunuo 13:11 na 17:11? (9) Ni mandhari gani katika vidio ambazo zathibitisha ukweli wa Mhubiri 8:9? (10) Vidio hiyo imeimarishaje itikadi yako katika ahadi za Biblia za wakati ujao? (11) Waweza kutumiaje kifaa hiki kusadikisha wengine kwamba Biblia imetoka kwa Mungu?