Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 11/10 uku. 3
  • The Bible—Accurate History, Reliable Prophecy

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • The Bible—Accurate History, Reliable Prophecy
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2010
  • Habari Zinazolingana
  • Kujifunza Kutokana na Vidio The Bible—Accurate History, Reliable Prophecy
    Huduma Yetu ya Ufalme—2000
  • Majibu ya Maswali ya Biblia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Jifunze Kutokana na Unabii wa Biblia
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2023
  • Ufalme Umesimamishwa!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2022
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—2010
km 11/10 uku. 3

The Bible—Accurate History, Reliable Prophecy

Ni uthibitisho gani unaoonyesha kwamba Biblia ni sahihi kihistoria? Ni unabii gani mbalimbali wa Biblia uliotimizwa unaotuhakikishia kwamba yale ambayo Biblia imetabiri kuhusu wakati ujao yatatimia pia? Maswali haya yanazungumziwa katika sehemu ya tatu yenye kichwa, The Bible—Accurate History, Reliable Prophecy, iliyo katika DVD inayoitwa The Bible—A Book of Fact and Prophecy. Baada ya kutazama video hiyo, unaweza kujibu maswali yafuatayo?

(1) Ni nani aliye Chanzo cha habari zenye kutegemeka za Biblia? (Dan. 2:28) (2) Biblia inaifafanuaje Misri ya kale kwa usahihi, na unabii ulio katika Isaya 19:3, 4 ulithibitikaje kuwa wa kweli? (3) Akiolojia imethibitishaje kwamba mambo yaliyoandikwa katika Biblia kuhusu Waashuru, wafalme wao, na kuharibiwa kwa taifa lao ni ya kweli? (Nah. 3:1, 7, 13) (4) Ni unabii gani mbalimbali kuhusu Babiloni uliothibitika kuwa wenye kutegemeka? (Yer. 20:4; 50:38; 51:30) (5) Ni unabii gani uliotimia kuhusu Umedi na Uajemi? (Isa. 44:28) (6) Unabii wa Danieli 7:6 na 8:5, 8 ulitimizwaje kuhusiana na Ugiriki? (7) Andiko la Danieli 7:7 lilitimizwaje wakati Roma ilipoibuka kama serikali kuu ya ulimwengu? (8) Ni Makaisari gani wanaotajwa katika Biblia? (9) Ni nini kilichowapata Wakristo chini ya utawala wa Nero? (10) Unabii katika Ufunuo 13:11 na 17:10 ulitimizwaje? (11) Mfalme wa nane ni nani? (12) Ni sehemu gani katika video hiyo zinazothibitisha ukweli wa maneno ya Mhubiri 8:9? (13) Unangoja kwa hamu kutimizwa kwa unabii gani wakati ujao? (14) Unaweza kutumiaje video hii kuwasaidia wengine waamini kwamba Mungu ndiye Chanzo cha Biblia?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki