Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • km 12/15 uku. 2
  • ‘Tembea kwa Imani, Si kwa Kuona’

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • ‘Tembea kwa Imani, Si kwa Kuona’
  • Huduma Yetu ya Ufalme—2015
  • Habari Zinazolingana
  • “Tupe Imani Zaidi”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2015
  • Tembea kwa Imani
    Huduma Yetu ya Ufalme—1996
  • Tembea Kwa Imani, Si Kwa Kuona!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Onyesha Imani Yako Katika Ahadi za Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2016
Pata Habari Zaidi
Huduma Yetu ya Ufalme—2015
km 12/15 uku. 2

‘Tembea kwa Imani, Si kwa Kuona’

Muda mfupi kabla ya Yerusalemu kutekwa na kuangamizwa, mtume Paulo aliwaambia Wakristo kwamba, kwa sababu walikuwa askari-jeshi wema wa Kristo, walipaswa kutarajia hali ngumu na hawakupaswa kutanguliza starehe au mapendezi yao wenyewe. (2 Tim. 2:3, 4) Kwa sababu hivi karibuni tunatarajia kuangamizwa kwa ulimwengu usiomwogopa Mungu, tunahitaji imani yenye nguvu ili tuendelee kukazia fikira mambo ya kiroho. (2 Kor. 4:18; 5:7) Tazama video ‘Tembea kwa Imani, Si kwa Kuona.’ (Tembelea jw.org/sw, tafuta kwenye MACHAPISHO> VIDEO.) Uwe makini kutambua jinsi kupenda vitu vya kimwili kulivyokuwa mtego kwa Nahamu na Abitali. Baada ya kutazama video hiyo, zungumzieni maswali yafuatayo.

(1) “Chukizo . . . likiwa limesimama katika mahali patakatifu” katika karne ya kwanza ni nini, na Wakristo walioishi Yerusalemu walipaswa kuchukua hatua gani muhimu? (Mt. 24:15, 16) (2) Kwa nini imani ilihitajika ili kulikimbia jiji hilo? (3) Walihitaji kudhabihu mambo gani ili kukimbia? (4) Kwa nini Nahamu na Abitali walichelewa kutoka? (Mt. 24:17, 18) (5) Raheli alikabili jaribu gani lingine la imani alipoondoka jijini Yerusalemu? (Mt. 10:34-37; Marko 10:29, 30) (6) Ni kwa njia gani Ethani alituwekea kielelezo kizuri cha imani na kumtegemea Yehova? (7) Wakristo walikabili hali gani ngumu walipokuwa Pela? (8) Imani ya Nahamu na Abitali ilidhoofikaje pole kwa pole? (9) Yehova aliwatunzaje Wakristo waliokuwa wakiishi Pela? (Mt. 6:33; 1 Tim. 6:6-8) (10) Ni kwa njia gani tunaweza kuwaiga Abrahamu na Sara mwisho wa mfumo huu wa mambo unapokaribia? (Ebr. 11:8-10) (11) Nahamu na Abitali walijidanganyaje kwamba ni afadhali kurudi Yerusalemu, na kwa nini walikosea kufikiri hivyo? (Luka 21:21) (12) Hali zilikuwaje Nahamu na Abitali waliporudi Yerusalemu? (13) Kwa nini tunapaswa kuimarisha imani yetu sasa—kabla ya mwisho wa mfumo huu wa mambo?—Luka 17:31, 32; 21:34-36.

Kutembea kwa imani kunamaanisha (1) kutumaini mwongozo wa Yehova, (2) kumruhusu aongoze hatua zetu, na (3) kuthamini mambo ya kiroho kuliko vitu vya kimwili. Na tuazimie kutembea kwa imani, tukiwa na uhakika kwamba “ulimwengu unapitilia mbali na pia tamaa yake, lakini yeye anayefanya mapenzi ya Mungu anadumu milele.”—1 Yoh. 2:17.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki