Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • mwb16 Aprili uku. 3
  • Watie Moyo na Kuwaimarisha Wengine kwa Maneno Yenye Fadhili

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Watie Moyo na Kuwaimarisha Wengine kwa Maneno Yenye Fadhili
  • Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo (2016)
  • Habari Zinazolingana
  • Ukamilifu wa Ayubu—Kwa Sababu Gani Unastaajabisha Sana?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1986
  • Ayubu Alivumilia—Hata Sisi Twaweza!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Kitabu Cha Biblia Namba 18—Yobu
    “Kila Andiko, Lenye Pumzi ya Mungu, Lafaa”
  • “Sitaukana Utimilifu Wangu!”
    Igeni Imani Yao
Pata Habari Zaidi
Daftari la Mkutano wa Huduma na Maisha Yetu ya Kikristo (2016)
mwb16 Aprili uku. 3

HAZINA ZA NENO LA MUNGU | AYUBU 16-20

Watie Moyo na Kuwaimarisha Wengine kwa Maneno Yenye Fadhili

Maneno ya mshauri yanapaswa kuwaimarisha wengine

16:4, 5

  • Ayubu alishuka moyo na kuteseka sana, hivyo, alihitaji msaada na kutiwa moyo

  • Wafariji watatu wa Ayubu hawakumfariji. Badala yake, walimshutumu na kumwongezea mahangaiko

Maneno yasiyo ya fadhili ya Bildadi yalimfanya Ayubu alie kwa dhiki

19:2, 25

  • Ayubu alimlilia Mungu ili apate kitulizo, hata kama kingehusisha kifo

  • Ayubu alikazia fikira tumaini la ufufuo na akaendelea kuwa mwaminifu

Elifazi akizungumza na Ayubu huku Bildadi na Sofari wakitazama

WASHTAKI WA AYUBU

Elifazi

Elifazi:

  • Huenda alitoka Temani katika nchi ya Edomu. Andiko la Yeremia 49:7 linasema kwamba Temani lilikuwa kitovu cha hekima katika nchi ya Edomu

  • Yaelekea kwamba Elifazi ndiye aliyekuwa mwenye umri mkubwa na mashuhuri kuliko “wafariji” wengine, hivyo alikuwa wa kwanza kuzungumza. Alipata nafasi tatu za kuzungumza na alizungumza kwa muda mrefu kuliko wengine

Shutuma za Uwongo:

  • Alimdhihaki Ayubu kwa sababu ya utimilifu wake na alidai kwamba Mungu hawaamini watumishi wake (Ayu 4, 5)

  • Alisema kwamba Ayubu alikuwa mwenye kimbelembele na mwovu na kudai kwamba Ayubu hamwogopi Mungu (Ayu 15)

  • Alimshutumu Ayubu kwamba alikuwa mwenye pupa na asiyetenda haki na akadai kwamba Mungu huwaona wanadamu kuwa hawana faida (Ayu 22)

Bildadi

Bildadi:

  • Mzao wa Shua. Huenda aliishi karibu na Mto Efrati

  • Alikuwa wa pili kuzungumza. Alizungumza mara tatu na alitumia muda mfupi, lakini maneno yake yalikuwa yenye kuumiza kuliko ya Elifazi

Shutuma za Uwongo:

  • Alidai kwamba wana wa Ayubu walikuwa wametenda dhambi, hivyo walistahili kufa na alidokeza kwamba Ayubu hakumwogopa Mungu (Ayu 8)

  • Alidai kwamba Ayubu alikuwa mkosaji (Ayu 18)

  • Alidai kwamba utimilifu wa mwanadamu ni bure (Ayu 25)

Sofari

Sofari:

  • Mnaamathi ambaye huenda alitoka kaskazini-magharibi ya Arabia

  • Alikuwa wa tatu kuzungumza na alimshutumu Ayubu vikali kuliko hao wengine. Alizungumza mara mbili tu

Shutuma za Uwongo:

  • Alimshutumu Ayubu kwa maongezi matupu na kumwambia aondolee mbali uovu wake (Ayu 11)

  • Alidai kwamba Ayubu alikuwa mwovu na alifurahia kutenda dhambi (Ayu 20)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki