HAZINA ZA NENO LA MUNGU | METHALI 12-16
Hekima Ni Bora Kuliko Dhahabu
Makala Iliyochapishwa
Kwa nini hekima kutoka kwa Mungu ina thamani kubwa? Kwa sababu inawakomboa wenye hekima kutokana na njia mbaya na kuwahifadhi hai. Inamsaidia mtu kuwa na mtazamo, maneno, na matendo mazuri.
Hekima inatulinda tusiwe na kiburi
Mtu mwenye hekima anatambua kwamba Yehova ni Chanzo cha hekima yote
Wale waliofanikiwa au walio na mapendeleo wanapaswa kujilinda wasiwe na kiburi na majivuno
Hekima humsaidia mtu kusema maneno yanayofaa
Mtu mwenye hekima anatumia utambuzi kufahamu mambo mazuri ya wengine na huzungumza vizuri kuwahusu
Maneno yenye hekima yana manufaa na ni matamu kama asali, si maneno makali au ya uchokozi